Unapokuwa na mtoto kuwa mwangalifu unapoanza mahusiano mapya

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
56,962
210,582
Alice alikua jirani yangu huku Kwamtogole, nilipomfahamu Alice alikua mwajiriwa katika Taasisi ya Serikali. Alifika Dar akitokea mkoani baada ya mjomba wake kumsaidia kupata ajira hii kabla hajastaafu. Elimu ya Alice ni kidato cha sita.

Alice alikutana na Bill aliyemuahidi ndoa, baada ya Alice kupata ujauzito, Bill alionyesha rangi zake za kweli. Alikua na mahusiano mengine mengi. Alice aligundua kuwa maisha ya ndoa na Bill ni ndoto.

Baada ya kujifungua ilibidi ahame kutoka kwa mjomba na kupata chumba na sebule huku Kwamtogole. Alitafuta dada wa kazi na maisha mengine yaliendelea.

Mshahara wa Alice haukua mkubwa sana, kila mwisho wa mwezi ilikua kuacha kulipia hiki ili upunguze deni hili. Kuanzia mshahara wa dada, mtungi wa gas, bill ya maziwa, kodi ya nyumba, chakula nk.

Bury ya Alice ilififia, hata yeye mwenyewe hakumbuki ni lini alinunua nguo mpya. Pamoja na hayo yote Alice alikua na amani moyoni. Alikwenda kanisani na kucheka na majirani vizuri tu.

Mtoto wa Alice akiwa na miaka mitano, Alice alikutana na Robert. Robert alikua mwajiriwa serikalini na alikua na ahueni sana ya maisha. Alishajenga nyumba yake Kimara na usafiri alikua nao. Alichokosa Robert ni mke.

Baada ya makubaliano ya kuhamia kwa Robert yalipokamilika Alice alirudisha funguo za chumba na sebule na kuhamia Kimara kwa Robert.

Miezi mitatu tu baada ya kuwa mkazi wa Kimara, Alice aliona rangi kamili za Robert, nwanaume mwenye gubu. Alice alianza kuwa mlevi. Kila akitoka kazini alinunua kichupa cha konyagi, baada ya kuwapikia chakula Robert na mtoto alianza kunywa.

Katika gubu la Robert, alianza kuingia chumbani kwa mtoto wa Alice usiku na kumfanyia mambo machafu akimtisha mtoto kuwa akimwambia mama yake atawafukuza na watalala barabarani. Kale katoto kakurwa za kulala barabarani siku za mvua alikaa kimya.

Maisha yaliendelea mpaka yule mtoto alipopata mfadhili kutoka kanisani aliyejitolea kumsomesha shule ya boda. Robert hakupenda kabisa kijana aondoke lakini hakuwa na sababu za msingi katika pingamizi.

Alice alipata maradhi na kufariki, mtoto wake alilia kwa huzuni. Mwisho alihitimu elimu yake na kuanza maisha yake na hakutaka kujua habari za Robert kabisa.

Kuingia kwenye mahusiano ukiwa na mtoto uwe mwangalifu sana.
 

Mnyuke Jr

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
4,466
6,264
Ubarikiwe kwa kuwakumbusha single mother wote, wasijione wanyonge mbele ya jamii ila watulie na watapata watu sahihi wa kuingia nao kwenye mahusiano sahihi
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,358
10,417
Huwa tunasikia tu visa vya Mama wa kambo kunyanyasa watoto. Hii ya Bwana Mkubwa Robert imevuka viwango vya manyanyaso
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
47,898
62,887
Alice alikua jirani yangu huku Kwamtogole, nilipomfahamu Alice alikua mwajiriwa katika Taasisi ya Serikali. Alifika Dar akitokea mkoani baada ya mjomba wake kumsaidia kupata ajira hii kabla hajastaafu. Elimu ya Alice ni kidato cha sita.
Hii story yako hujatuambia mtoto wa Alice ni wa jinsia gani?

Lakini kikubwa hii ni tabia binafsi ya mtu, nimeshuhudia mtu anamkula binti na mama yake kwa hiyari yao na mmoja anajuwa kwamba huyu jamaa ameshamla binti yangu na bado mama anakwenda kuvuliwa chupi.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
56,962
210,582
Hii story yako hujatuambia mtoto wa Alice ni wa jinsia gani?

Lakini kikubwa hii ni tabia binafsi ya mtu, nimeshuhudia mtu anamkula binti na mama yake kwa hiyari yao na mmoja anajuwa kwamba huyu jamaa ameshamla binti yangu na bado mama anakwenda kuvuliwa chupi.
Mtoto wa Alice ni wa kiume, Alice alikunywa pombe kila siku kwakua hakua na furaha ndani ya nyumba ya Robert. Akiwa amelewa na kulala fofo Robert alikwenda chumbani kwa mtoto.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
56,962
210,582
Yani chura zote hizi mjini uende kulawiti mtoto ni ushetani tu hakuna lugha nyingine.
Alice hakujua maisha yake katika chumba na sebule yalikua ya uhuru na amani kuliko kuishi kwa mwanaume.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Top Bottom