Unapokosa pa kushtakia shida yako inaumaje ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unapokosa pa kushtakia shida yako inaumaje !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Judgement, Dec 16, 2011.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Takriban karibu kila uchao binadamu tunakutana na changamoto tofautitofauti, Kadhia, Matatizo, Karaha, Shida, Taabu, Mashaka, Mikwazano, Kero, Maudhi,Hasara na mengi mengineyo ya kufanana na hayo.

  Ni vitu vilivyotuzunguka na si rahisi kuviepuka vyote kwa mara moja. Kikikukosa hichi utakua na kile, ndiyo maisha yalivyo.

  Pamoja na yote hizo sintofahamu zote zinapotukabili hatukosi sehemu ama maeneo ya kushtakia kwa mfano ukipata hasara utatafuta uwezekano wa kutoipata tena.

  Ukiudhiwa utaombwa radhi nawe ukiudhi utaomba radhi yakaisha. Tatizo umeibiwa utampeleka polisi mwizi wako. Shida sijui umeme/maji kwako hakuna kwa jirani wanavyo utashtaki Tanesco/Idara ya maji. Kero voucher inagoma kuingia sijui M-pesa uliotuma haijafiki fasta customer care.

  Kadhia tumbo, kifua vinauma utanyooka Muhimbili, Bugando, Kcmc, Mountmeru n.k. Ofcoz changamoto chungu mbovu zina maeneo yake ya kushtakia. Sasa yote 9 !

  10 ni hili tatizo linaloitwa NETWORK hili mimi nimekosa pa kulishtakia ! Umeandika thread yako umeifikia unataka kui'shut NETWORK haifungui ina search tu!

  Simu yako ina crdt enough unapiga unapohitaji simu haiendi sababu NETWORK ! Haishii hapo imeshaenea kwenye Ma'benki unakwenda upate huduma unaambiwa System iko down!

  Kwenye Maofisi ya Serikali, Taasisi zitoazo huduma kwa wananchi/jamii hadithi ni hizohizo ndiyo nimeshusha huu uzi membars mnisaidie Roadmap huyu ADUI NETWORK NIKAMSHITAKI WAPI ?
   
Loading...