Unapojifuangua Ndama.....

Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
8,412
2,252
VITENDO vya kishirikina vimekigubika Kijiji cha Kasala, wilayani Kyela, baada ya mwanamke mmoja, Maria Asukenie (20) aliyekuwa mjamzito kujifungua ndama mweusi.

Ndama huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa na hali ya mwanamke huyo si nzuri.

Akisimulia mkasa huo, mmoja wa watu walishuhudia tukio hilo, Rajabu Rajabu, alisema Maria alijifungua juzi, saa 4 asubuhi, baada ya kujisikia uchungu.

Alisema kitendo hicho kinahusishwa na imani za kishirikina, kwani kitu kama hicho hakijawahi kutokea kijijini hapo.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ilembula, Aliko Mwakalukwa, aliwataka watu kuachana na imani hizo, kwani jambo hilo ni tukio la kawaida.

Pia aliwataka wakazi wa eneo hilo kutozungumzia suala hilo, kwani linaleta utata miongoni mwa watu.

Alisema kuendelea kulizungumzia suala hili ni kunaweza kuleta uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii hiyo.

Source
 
Basi hata picha hakuna...?! huyo mwandishi yaani hata kamera ya bei rahisi hakuwa nayo basi... hii kweli nyepesi nyepesi tena ya bei rahisi...!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom