Unapoishangaa Iringa kutomchagua Dr Mahiga,wengine tunashangaa CCM kumuacha Mahiga kwenye Urais

Ndiyo tatizo la watu wasiojua umuhimu wa demokrasi. Yeye nani hasa hadi ashangae utashi wa wapiga kura kumchagua mwakilishi wamtakaye Bungeni?

Madikteta ndivyo walivyo!!!

Wajuzi wa "Political Economy" wanasema maendeleoo ya kiuchumi huenda sambamba na demokrasia,tunapokimbizana kuleta maendeleo tusiiache nyuma demokrasia na heshima ya "Political Pluralism"...nchi zote zilizoendelea,maendeleo na demokrasia vilienda pamoja!Viongozi wanapoonyesha kuheshimu maamuzi,uhai na maisha ya watu ndio watu wanapozidi kuonyesha imani kwa serikali.

Tusifurahie kasi ya "maendeleo" isiyoendana na demokrasia ya kweli,binadamu ana hulka ya kupenda na kukitafuta kile anachokikosa zaidi ya kile anachokipata,ndio maana kuna wanawake wanapewa kila kitu,lakini kama wananyimwa "uhuru" hata wa kuchangamana na jamii ya wanawake wenzao wanageuka "micharuko".

Uongozi bora ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya watu,mitazamo kinzani,kukosolewa na hata kukataliwa na wachache.Ivory Coast iliwahi kuwa tulivu,pengine tulivu zaidi hata ya Tanzania.


Leo tunawashangaa Wanairinga kwa kuacha kumchagua Dr Mahiga Augustine,jasusi na mwanadiplomasia mbobezi kuwaongoza katika jimbo lao la Iringa Mjini.

Na sisi tulio wengi,wenye kuijua historia ya Dr Mahiga,tuliishangaa CCM ngazi ya Taifa katika kinyang'anyiro cha Urais kumuacha Dr Mahiga na kuwachangua wengine ambao walikuwa wanabeep tu nafasi ya urais na wakashangaa wameipata.

Lazima tuishangae CCM,maana ilishindwa kuona umuhimu wa Dr Mahiga,hata kwa kumuingiza tu katika nafasi tatu za mwisho katika kuelekea nafasi moja ya kugombea urais.

Tukiwa na majibu ya kwanini hata huko ngazi ya Taifa walimuweka kando Dr Mahiga,kwanini tuwashangae hawa wananchi wa Iringa?Kama fulani alikuwa Rais baada ya kuwazidi kina Mahiga,kwanini aone ajabu Iringa kumchagua mwingine badala ya Mahiga?

Wakati mwingine tunapaswa kuziishi kauli zetu,tunapopaza sauti kuwa maendeleo hayana chama,kwamba sisi iwe Chadema,CCM au CUF tunafanya nao tu kazi,kwanini tuanze kusema kauli za mgawanyiko wa itikadi katika hadhara zenye sura ya kitaifa?

Huwezi kuifanya nchi nzima kuwa na mtazamo mmoja,wala huwezi kuamua mambo ya Taifa kama mambo ya familia yako binafsi.Wapiga kura na raia walio na umri wa miaka 18,umri unaowawezesha kuchagua lile lililo jema kwao.

Kwanini uwapangie watu mtu wa kumchagua wakati wewe huwa hupangiwi?Ndio maana wenye vyeti feki wengine umefukuza na wengine umewaacha sababu ni wachapa kazi.Kama usivyopenda wewe kupangiwa na wengine,na wewe usiwapangie wenzako.
 
Ulifanya kosa Kubwa sana la kiufundi Ndg salary slip tr h 26042018 ,vp kuna nyingine tena tarehe 01/08,VP utakuwepo au utaogopa tena?
Ina maana Salary slip naye hakuandamana? Basi hawa jamaa wanadanganya watu yaani wanataka kuwatumia wengine kama karai, kujinufausha.
 
Siasa za nchi hii zinafurahisha sana...

Ule uchaguzi wa ndani ya CCM kumpata mgombea uraisi nadhani kuna kitu hakikuenda sawa hadi akapatikana huyu aliyepo.
Mambo mengine utokezea kama fundisho kwa wahusika! Aliye chaguliwa siyo tu anaelekea kuipeleka CCM nje ya madaraka lakini kiburi na ulevi wa madaraka yasiyo tarajiwa kumepelekea Watanzania wengi kwa sauti moja kuitaka Katiba mpya!
 
Back
Top Bottom