Unapogundua mwenza wako si muaminifu na amekumbukiza ugonjwa hatua gani utachukua?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Wanawake kutokana na maswala ya uzazi tunapata bahati ya kupitia vipimo vingi sana. Mara nyingi hapa ndipo unagundua una magonjwa. Hapa tayari una ujauzito na unafahamu ulikua muaminfu kwa mwenza wako.

Kwa wanaume hali kadhalika, hujawahi kumfumania mke wako lakini unajikuta unapata maumivu wakati wa haja ndogo. Unaamua kwenda hospitali unafahamishwa kuwa una gonorrhoea.

Kuna aliyeniambia mchukulie mwenza wako kama kito cha thamani, huwezi kuitupa pete yako ya dhahabu na tanzanite kisa imeanguka kwenye kinyesi. Niliyatafakari maneno yake lakini nemeona niwaletee wananzengo hii mada tuijadili.
 
Inaumiza sana hali hiyo, unaepuka vishawishi unakuwa mwaminifu ukidhani mwenzio nae yupo hivyo(kwa mienendo yake) lakini mwsho wa siku inakuwa hivyo. Binafsi nasisitiza tu kujikinga na kuwa na tabia ya kupima mara kwa mara japo itaweza tafsirika ya kuwa humuamini mwenza wako. Afya njema ni muhimu sana.
 
Amini nafsi yako tu, ya mwingine mwachie mwenyewe, Kama ugonjwa unatibika jitibu, na angalia namna ya kujilinda, inawezekana kuachana,kutengana, au kuambiana ukweli, ondoeni sababu iliyosababisha hilo litokee, Elimishaneni juu athari zake, Mjichunge. kama hautibiki ambianane ukweli, suluhisha, elimisha, Mkae kwa kujitunza ili kuongeza muda wa kuishi.
 
Kwakweli inaumiza sana, unajitunza vizuri kumbe mwenzako anahangaika ovyo nje anakuletea magonjwa.
Mtu unaweza kuchukua maamuzi magumu kwa hasira na uchungu wa kuumizwa

Na kuna watu wengi hupata magonjwa kwa style hiyo, kuna wengine wakishagungua wamebeba maradhi nje huko hawawi wawazi kwa wenza wao wanaona ni bora waishi wote katika hali hiyo. Kwa kukusudia na kujua kabisa hali sio shwari kwake anaamua amfiche mwenza wake na mwsho wa siku anamuambukiza (huu ni ujinga uliokithiri).
 
kuna rafiki yangu alijiua ajili ya hii kitu, bt kwa upande wangu ikinipata nitachukua tahadhari za kiafya then mengine nitamuachia mungu maana dunia inachallenge nyingi sana hata usipougua utakutana na zingine ngumu zaidi.
 
Kuna wakati fulani wa zamani sana..
rafiki yangu alikuwa na demu wake mzuri kupita kiasi na alipanga hadi kumuoa!!
kuna siku huyu rafiki yangu alisafiri katika mishe zake na huyu mchumba wake alimfungulia saluni..
siku moja alikuja rafiki yangu mwingine alikuwa ametoka sudan huko alikuwa katika kaz za udereva...
hawa jamaa wawili wote ni my best friends lakini wao kwa wao si friends.
basi katika pita pita zetu huyu jamaa wa sudan akamuona yule dem wa msela wangu akaanza kudondosha mate na nikamweleza kwamba ishu ni msela wangu na anajenga nae future!alikubali usoni ila akili yake haikumpa akapambana hadi akapita nae na akamvuruga pande zote..
jamaa wakati ananipa stori amemchakata hivyo nilichukia sana ila sasa nikakosa namna...
mara paap yule mchumba wa yule dada amerudi.
baada ya siku 2 jamaa kaniita ananiambia maswaibu yalompata kapata GONO si la nchi hii na huko alikuwa na mishe zake hakuchepuka!!
anasema amempiga sana dem wake aseme alitafunwa na nani lakini hakusema!!
daahh nili feel guilt sana ila sikuwa na jinsi.
alimtema yule dada na saluni akaichkua.
 
Maamuz gani utachukua wakati una kibendi? We ni kuvaa barakoa na.kujifukiza tu huku ukinywa antibiotics.

Tuvumiliane jamani,.kipindi cha kubeba mimba ndio.kipindi ambacho watu wengi huonja kazi za nje sababu ya ugwadu 😂😂😂
Kwakweli inaumiza sana, unajitunza vizuri kumbe mwenzako anahangaika ovyo nje anakuletea magonjwa.
Mtu unaweza kuchukua maamuzi magumu kwa hasira na uchungu wa kuumizwa
 
Kuna kipindi nilienda lll mkoani huko ,

Sasa Jiran nahome kuna kituo cha Afya..

Alikuwepo Nurse wakike, kaolewa

Yeye kila siku akawa anamuambia mumewe ,wamempangia zamu ya usiku

Siku zikaenda wee, Watu wakamtonya Mume wa Nurse kua mkeo anabanduliwa na Jamaa .

Anavyokuaga yupo kazin huwa hayupo.


Siku za mwizi 40 alisema JPM, jamaa siku hiyo akatonywa, akaamua kuja na mwanawe kuzuga km mwanawe anaumwa, kufika hapo, Mkewe hayupooo.

Jamaa akarudi home, baadae tena saba usiku akarudi , mkewe hayupoooo


Akaamua kurudi kulala, anakakuta kadem et ndio kamefika na vinguo vya kazin.


KUNA WATU WANAPIGA

DEMU ALIPIGWA KIPIGO,SIJAWWH ONA, ALIPIGWAAA

NYIE WATU, DEMU ALIPIGWA MPAKA AKAWA ANAUNGURUMA KAMA MBWA ANAYETAKA KUFAA,.PIGWA SANAAAAAAAAAAAAA .


Alivyopona, Jamaa likamuacha kabisa.
 
Na kuna watu wengi hupata magonjwa kwa style hiyo, kuna wengine wakishagungua wamebeba maradhi nje huko hawawi wawazi kwa wenza wao wanaona ni bora waishi wote katika hali hiyo. Kwa kukusudia na kujua kabisa hali sio shwari kwake anaamua amfiche mwenza wake na mwsho wa siku anamuambukiza (huu ni ujinga uliokithiri).
Ujinga na ukatili, imagine mtu anamuambukiza mke wake mwisho wa siku wote wanaumwa wanabaki watoto wakiteseka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom