Unapofikiria mtu ambaye ni mzuri, nani anakuja kwenye akili yako?

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Nianze mada hii kwa kukuuliza swali.
Unapofikilia mtu ambaye ni mzuri, nani anakuja kwenye akili yako?
Nini kimefanya ukamuwaza yeye?

Je ni umbo lake, mavazi yake, nywele zake, sauti yake, ukarimu wake, au ni makeup zake n.k ?

Kamsi nyingi zinaeleza uzuri kwa maneno mbalimbali ila kwa ujumla Uzuri ni hali ya mtu / kitu kuvutia na kupendeza.

swali mhimu linalojitokeza katika tafsiri hii ni je watu wote tunavutiwa na kupendezwa na mtu/vitu au mambo sawa?

Bila shaka jibu la swali hili ni Hapana. Ikiwa ndivyo, uzuri ni nini basi?

Kwa ugumu wa swali hili kuna dhana mbalimbali ujitokeza katika kutafsiri uzuri kulingana na mkutadha na mtazamo wa mtu au jamii.

Kuna msemo maarufu wa kiingereza usemao “Beauty is in the eye of the beholder’ kuwa “uzuri wa kitu uko kwenye macho ya mtazamaji” ikimaanisha kila mmoja ana vigezo vyake vya uzuri, au kwa maneno mengine ni kuwa hakuna kitu ni kizuri kwa asili yake bali mtazamaji yeye ndo uhamua hiki ni kizuri au vinginevyo.

Kwa mfano tafsiri ya uzuri kwa waandaaji wa mashindano ya miss world haiwezi kuwa sawa na tafsiri ya uzuri kwa watetezi wa haki za binadamu. Mashindano ya miss world wanatamani kuona mshindi akiwa kigori wa umri wa miaka 17-26, mrefu wa anagalau feet 5’1, mwonekano mzuri na Ngozi yenye afya, intelligent etc., ila mshindi wa tuzo za nobel za haki za binadamu kwa mwanamke, msisitizo wao mkubwa uko kwenye ujasiri, kujiamini, uvumilivu, moyo wa kujitolea, huruma n.k.

Kwa mfano niliotoa hapo juu kuna mtazamo wa sifa mbili kuu. Moja ni sifa za nje na zinazoonekana (outside-beauty au attractiveness) na zingine ni sifa za ndani ambazo ujidhihirisha kwa mwenendo na tabia (inner-beauty au characters).

Uzuri wa mwonekano (outside beauty-attractiveness) huu ndio unaoleweka kama uzuri kwenye dunia ya leo (comercial world). Aina hii inapewa promo na vyombo vya matangazo kama TV na Magazeti, film industry, music industry, na marketing industry.

Dhana hii imekua chanzo cha mitindo na tabia mbalimbali tunazoziona katika jamii zetu ikiwemo, kujichubua, kutumia vipodozi vingi, kubadilisha maumbo ya mwili na hata fasheni za mavazi.

Mfano, wanawake wengi wana aamini uzuri ni kuvaa mavazi yanayoleta mvuto kama skin jeans, min skirt, na matumizi ya vifaa kama Brazilian hair, eyeshadow, mascara, na lipstick. Pamoja na kuwa fasheni hizi ni gharama kubwa bado hazina matokeo endelevu ya kulinda uzuri wa mtu na mbaya Zaidi kuna hatari za kiafya zitokanazo na product hizi za urembo.

Aina nyingine ni uzuri wa ndani (inner-beauty). Uzuri huu unajikita zaidi kumulika haiba na tabia ya mtu. Ina focus kwenye mambo yasionekana kwa macho bali ujidhihirisha kwa mwenendo na tabia ya mtu. Tabia hizo ni Pamoja na tabasamu, jinsi anavyoongea, ukarimu, upole, uvumilivu n.k. sifa za uzuri huu mtu uweza kuzeeka navyo na havihitaji gharama kuvipata bali ni maamzu na makuzi.

Ushahidi wa uzuri huu unakwenda mbali katika historia, Pamoja na kutokuwepo kwa fasheni na urembo wa gharama bado wanawake wengi walikua wanasifiwa kuwa walikua wazuri. Fanya rejea ya story ya mke wa Ibrahimu Sarah, mke wa Yakobo Rebeka, na hata story ya mpwa wa Moldekai Ester.

Naomba ieleweke kuwa Pamoja na tofauti hizi za kimtazamo, hakuna dhana ya uzuri inayoonekana bora zaidi ya nyingine.

Inaweza kukushangaza ila tafiti ndivyo zinavyoonyesha-uzuri wa mwonekano unalipa kama ulivyo uzuri wa tabia.

Jamii za kimagharibi zinathamini sana tafiti. Katika tafiti ambazo zimewahi kufanyika juu ya uzuri wa mwonekano ulibaini yafuatayo:

Watu wanaovutia kimuonekano

· Huonekana wana afya njema
· Huonekana wana akili (intelligent)
· Uaminika kwa upesi na hivyo ni vyepesi kupata kazi na kupewa huduma kama mikopo
· Wana ushawishi mkubwa hivyo wana chance ya kufanya vizuri katika biashara na siasa
· Ni wepesi kupata wapenzi wanaovutia pia
· Hupendwa sana na watu,(are more likable) inashangaza tafiti zinaonyesha watu wazuri hupendwa zaidi hata na Watoto wadogo
· Wakianzisha makampuni wana chance kubwa ya kufanikiwa

Hata hivyo, tofauti na mtazamo wa nje unakuwepo kwa wengi kuzani kuwa watu wenye muonekano mzuri wanabahati na kufaidika Zaidi-tafiti paia see zilizofanyika kwa watu waliozaniwa wana muonekanao mzuri yafuatayo kati ya mengi yalibainika:

Watu wenye mwonekano mzuri
· wengi licha kuonekana wachangamfu huisi hawana furaha ya kweli
· wengi licha ya kupendwa kwa wepesi huisi kuwa wanatumiwa na wao sio wazuri kiivyo (contrast effect)
· wengi licha ya kusifiwa huisi hawaheshimiki
· wengi ukutana na vita ya kupingwa, kuchukiwa na kuonewa wivu na watu wa jinsia sawa (Same-sex dunce effect)
· wengi uhisi hawatendewi sawa kwani jamii inakua na matarajio makubwa kwao-(punished by high expectations)
· wengi huisi wanapendelewa na sio uwezo wao-hivyo ushindwa kujiamini (contingent self-esteem)
· Wazuri licha kuwa maarufu-hujihisi wapweke

Wito wangu, unaweza kuwa na uwezo wa kukata, kusafisha, toboa, kujaza, na kuapndikiza mwilini mwako chochote ili kufaidika na kuitwa mzuri. Hata hivyo lazima ujue utalipa gharama saw ana ulivyo faidika.

Elimika , ila Usiache kutoa mtazamo wako kwenye mada
 
Sijasoma uzi wote, ila mwanamke mzuri kwangu ni

1: lazima awe mweusi
2: anivutie - (physical appearance yake, dressing)
 
Uzi mzuri. Watu wengi huenda mbali katika kuutafuta uzuri kwa kile kudhani ni suluhisho na njia ya msingi katika kupata raha na furaha ya maisha.
 
Kwangu mimi uzuri ni kile ambacho kinanifurahisha.
 
Back
Top Bottom