Unapendekeza mabadiliko gani kwenye mfumo wa elimu

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Ninahisi ili tusonge mbele sekta nyingi tanzania zinahaitaji mabadiliko na mabadiliko hayo ni kwa watu walio katika nafasi za kufanya maamuzi kuwa wabunifu. Kwa leo naoba nishirikiane na great thikers wenzangu ni mabadilko gani ungefanya kwenye sekta ya ELIMU kama ungepewa postion na post ya kufanya Decision making

Binafis ningefanya mabadiliko ya kufanya shule hasa za primary na sekondary kuwa na nguvu ya kuchagua baadhi ya masomo yanayoendana na mazigira na mahitaji ya shule husika

Binafsi kuwa na mtaala standard kwa shule zote sio haki kwa sababu shule za mjini zina rasimali tofauti na shule za vijijini. Vile vile kuna wanafunzi wa maeneo fulani wana vipaji fulani zaidi kulinko wa maeneno mengine.

Tuchukulie mfano ingekuwaje mtaala wa elimu ungekuwa flexible wanafunzi wa arusha( Wambulu,Wamasai) wakaruhusiwa kuwa na somo la PE(Physical education) la kukimbia badla ya kulazimisha wanafuzi wote wa sekondary wafanya mtihani wa biology

Wenzetu kenya wanaexport wanariadha nje wankimbia kwa jina la Quatar, USA , etc

So kifupi mabadiliko ya elimu abayo ningeyafanya kama ningekuwa katika nafasi ya aauzi ni kuwa na mtaala unaoendana na maeneo husika. Kwa style hii naamini elimu ya michezo au utamaduni inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi. Kwangu hilo ni Moja ya mabadilo mengi yanayohitakika kwenye elimu yetu.

Je wewe ungefanya mabadiliko gani ?
 
Ninahisi ili tusonge mbele sekta nyingi tanzania zinahaitaji mabadiliko na mabadiliko hayo ni kwa watu walio katika nafasi za kufanya maamuzi kuwa wabunifu. Kwa leo naoba nishirikiane na great thikers wenzangu ni mabadilko gani ungefanya kwenye sekta ya ELIMU kama ungepewa postion na post ya kufanya Decision making
Asante "Mtazamaji" kwa kuanzisha mada hii. Nakubaliana nawe kabisa kuwa sekta nyingi hapa Tz zinahitaji mabadiliko, tatizo kubwa ni kwamba hao hao wenye maamuzi SIYO WABUNIFU na sababu kubwa ya wao kukosa ubunifu ni huo huo mfumo wa elimu. Mfumo wa elimu ulioko, sambamba na fikra au mtezamo wa viongozi na watendaji wa serikali ambao wamelelewa na mfumo huo, uliandaliwa na Nyerere miaka ya 1960s na 1970s wakati wa siasa ya Ujamaa. Ili kunyoosha fikra za nchi zilenge upande mmoja, watu kama Dokta Chagula waliondolewa kutoka uongozi wa Chuo Kikuu na badala yake wakawekwa makada wa chama, Pius Msekwa na Ibrahim Kaduma kuhakikisha kuwa fikra na mtezamo wa wasomi vimethibitiwa (rendered harmless to the rulers) kwa muda mrefu ujao. Ili kufanikisha azma hiyo UDSM ilizunguka dunia kutafuta maprofesa wakomunisti na wasomi wengine wenye sympathy na ukomunisti kuja Tanzania kusia mbegu za fikra hasi na hao ndiyo wamelea na kuwakuza maprofesa wetu wa leo. Kwa kuwa kwa muda mrefu Chuo Kikuu kilikuwa kimoja tu (kwa kuzingatia principle ya Nyerere ya Unity, yaani mtawala mmoja, chama kimoja, gazeti limoja, radio station moja, Chuo Kikuu kimoja, etc.) asilimia kubwa ya viongozi na watendaji wa serikali pamoja na wasomi wengi, ikiwa ni pamoja na maprofesa wa vyuo vikuu vya serikali na visivyo vya serikali, pia waalimu wa vyuo vingine na shule za sekondari hadi msingi, sehemu kubwa yao au wamepitia moja kwa moja kwenye tanuru la UDSM (or better dimbwi la barafu iliyoganda la UDSM) au wamelelewa kiakili na kimawazo na watu waliopitia kwenye tanuru au dimbwi hilo.

Kama wewe ni mbunifu, mtendaji mzuri, una akili, hutakiwi; utakuwa tishio kwa wakubwa wako. Bosi antaka ang'are kuliko wakuu wa idara kwa hiyo anateua wasaidizi wake wasiomfikia kwa ubunifu, utendaji wala akili. Wakuu wa idara nao wanateua wakuu wa vitengo kwa misingi hiyo hiyo, na hawa pia kwa walio chini yao. Matokeo yake ni successive incompetence yaani utendaji mbovu unaozidi kuongezeka kutoka uongozi wa juu kwenda chini na kutoka uongozi wa leo kwenda kwa uongozi wa kesho. Watu wengi wenye ubunifu, utendaji mzuri na akili hawathaminiwi na badala yake wanathaminiwa wasiokuwa na wazo jipya, wasio na akili na wasio watendaji wazuri. Matokeo yake ni kuwa wale ambao wangeboresha mambo wanakuwa frustrated na kuondoka au wajifanye wajingajinga kama wenzao ili wabaki kazini.

Katika miaka ya 1983/84 Nyerere aligundua kuwa mfumo aliokuwa anajitahidi kujenga ulikuwa siyo mfumo wa kuleta maendeleo bali wa kuyakwamisha. Kwa hiyo alianza kurudisha zile system alizobomoa lakini kwa kuwa alitoka madarakani baada ya muda si mrefu hakukamilisha wala sehemu ya kumi ya marekebisho hayo, hasa kwenye mfumo wa utawala serikali kuu na serikali za mitaa. Rais Mwinyi naye pia alijaribu kuendeleza marekebisho hasa kwenye uchumi na kupanua kwa kiasi uwanja wa siasa lakini naye hakuweza kukamilisha mambo. Baada ya hapo hakuna aliyeweza kukamilisha au kuboresha marekebisho aliyoanzisha au Nyerere mwenyewe au Mzee Mwinyi ya kurudisha nchi kwenye mkondo wa maendeleo ya kweli badala ya ndoto za Alinacha.

Mfumo wa elimu unachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha marekebisho hayo kwani, kama nilivyosema hapo juu, fikra na mtezamo wa wasomi wetu umeganda kwenye miaka ya 60 na 70 na viongozi wetu pamoja na watendaji wengi wamelelewa na mfumo huo. Hili ni janga la taifa, kubwa kuliko El Nino, Tsunami hata tetemeko la ardhi na lina madhara makubwa kwa taifa kuliko hata vita, nadhani kwa sababu zilizo dhahiri.
 
NguchiroTheElde

Kweli kabisa inauma kuona hakuna customised education japo ya somo moja linaoendana na mazingira.

Mfano kuna shule ziko karibu na fukwe. lakini hazina somo la uvuvi au kupiga kasia maji au somo la kuogelea. kuna watu ulaya wanaishi na kuendesha maisha yao kwa mchezo ya kupiga kasia. Hivi tungekuwa na masomo kama haya sitashanga kuna mpiga kasia/ muogeleaji kutoka visiwa vya ukerewe anapata medali japo ya shaba in near future.

Kuna maeneo yana misitu lakini wanafunzi wanamaliza hawana si tu ujuzi hata taaluma ya kufuga nyuki na kuvuna asali taaluma hizi wanazo watu wacahche na zitapotea muda si mrefu.

Na hakina wizara ya elimu inaweza kujaribu kufanya elimu iwe burudani japo kwa somo moja nakuvutia jamii au watu wasio na mwelekeo sana wa elimu.Nina hakika shule za primary/sekondary arusha vijini zingeruhusiwa kuwa na somo la ufugaji wazazi wengi waneshawishika kirahisi kupeleka watoto wao shule. Mtoto anakwenda shule sabbu ya somo la ufugaji kama chambo lakini pia atafundishwaelimu nyinine na pande zote serikali na jamii inafaidika.

Tunahitaji kuona vitu katika diffrent angle

Inauma nikisikia shule fulani imekuwa ya mwisho hasa za nje ya mji kwa sababu ya mfumo mbovu uliopo wa kutotambua uwezo taofauti, mazingira tofauti na changamoto tofauti na matatizo tofauti walizonazo wanafunzi wa shule moja na nyingine.
 
Lets hope that the MMES,WILL BE A SUCCESS , Jinsi edu ya tz inavyoendeshwa haiitaji uwe msomi sana utoe plans,mission and objectives sasa waliopo kwenye system wanamka asubuhi na matongongo yao wanatoa maamuzi yanayokuja kutuhaunt baadaye.watu wanaiba mitihani,elimu imekuwa mtaji,watu wanaumia

SUGGESTION

WIZARA YA ELIMU ISAFISHWE NDANI NJE BARAZA LA MITIHANI.,TAASISI YA ELIMU , BARAZA LA MITAALA ZIPEWE FRESH MIND TUTAONA CHANGES
 
Sidhani kama tunatakiwa kuanza kutafuta mchawi!
we should focus on what need to be done.

Starting point siyo kukimbia kubadili mitaala. Inatakiwa tuanze kwa kuwasomesha waalimu wetu, tena wapelekwe kusoma nje ya nchi ili wafunguke zaidi. Wakisharudi, wawafundishe waalimu wenzao, mpaka hatua ya kuwa na uhakika zaidi ya robo tatu ya waalimu wote Tanzania wako conversant na hiyo mitaala wanayotarajia kuibadilisha. Kuanzia hapo ndo tunaweza kubadili mitaala kwa awamu.

Isifanyike kama inavyofanyika sasa. ambapo walimu wale wale, hawajapata mafunzo yoyote, wanapewa mitaala mipya wafundishe. Tukiendelea kufanya hivi, hii nchi tutaiangamiza.
 
Sidhani kama tunatakiwa kuanza kutafuta mchawi!
we should focus on what need to be done.

Starting point siyo kukimbia kubadili mitaala. Inatakiwa tuanze kwa kuwasomesha waalimu wetu, tena wapelekwe kusoma nje ya nchi ili wafunguke zaidi. Wakisharudi, wawafundishe waalimu wenzao, mpaka hatua ya kuwa na uhakika zaidi ya robo tatu ya waalimu wote Tanzania wako conversant na hiyo mitaala wanayotarajia kuibadilisha. Kuanzia hapo ndo tunaweza kubadili mitaala kwa awamu.

Isifanyike kama inavyofanyika sasa. ambapo walimu wale wale, hawajapata mafunzo yoyote, wanapewa mitaala mipya wafundishe. Tukiendelea kufanya hivi, hii nchi tutaiangamiza.

Kabengwe nakubalina na wewe lakini unasikia wanasiasa maneno nyao vijana wakimaliza shule wasisubiri kuajiriwa wajiajiri.
Kama serikali iliweza kuazisha initiativa za upe na tukafuta ujinga kwanini tusitumie style hii kuwapa vijana wetu ujuzi wa kuyamudu mazigira.

Iweje shule iko msituni kusiwe na mwanakijiji wa kufundisha jinsi ya kurina asali. kuwafundisha kwa vitendo jinsi ya kuotesha miche.Iweje shule ziko karibu na ziwa then hakuna hata somo la kuogelea.

Sidhani kama tunahitaji kuwapelekawalimu wa primary nje kwenda kusoma. KUna ujuzui wa kawaida kumanage mazingira watu wanao ata kijijini wakiwezeshwa tu wanafuzi wanaweza kuwa na elimu bora.

Sidhani kama kwa shule za umasaini kuwa na somo la ufugaji unahitaji vitu vingi ukimchukua mfugaji mmoja mwenye ujuzu unampiga msasa then mambo yanakuwa safi.


Binafisi naona kwa masomo machcahe tunayoweza wanafunzi wanaweza kufundishwa practically. Shule umasaiani haina labaratory wala falsh disk wanafunzi wanajifunza distillation kwa nadharia. Je hata kujifunza ufugaji au kurina asali itushinde kwa vitendo wakati rasilimali tunazo.

It could am crazy thinking lakini if it was me primary school walu zingepewa flexibility ya kuchagua japo somo moja linaloendana na mazingira yao.
 
Mimi nadhani kuwe na mabadiliko kabisa kwa namna mitiani inavyotengenezwa, kumbukumbu yangu ya mwisho ilikuwa ni namna mitihani inavyokuja before A'levels. Wanafunzi wana soma kwa kubahatisha na inabidi akariri tarehe nyingi na matokeo mengi for no reason. Namna hii mi naamini aipanui mawazo ya wanafunzi.

Kinacho itajika sasa ni kuwafundisha wanafunzi wa reason badala ya kumwambia mwanafunzi ajibu vita vya majimaji vilikuwa lini na awataje wahusika wakuu na vyanzo chungu mtele ambazo umfanya akariri. Inabidi wanafunzi waelezee athari za vita na mwisho watoe opinion zao wao kama vilisaidia au avikusaidia kutokana sababu zao ambazo zina justifiable argunment. Hii itasaidia wanafunzi kupekua historia yetu au somo lolote wanalochukua kufungua vitabu vingi na kuweza kufanya ma-research yao badala ya kurely on class notes or one book.

Na vile vile mara nyingi watu wamalizapo shule huwa na desturi ya kusoma baada ya hapo. Kwa maoni yangu namna elimu Tanzania inavyotolewa kwa wanafunzi wa secondary imeshapitwa na wakati na aifundishi wanafunzi ku-reason na kutoa strong arguments. Inachofundisha ni kukariri kwa average students na kuwaacha magenius ndio wapete kwa kuwa wanavipaji vya kujiuliza binafsi. Ni maoni yangu tu anyway.
 
Mtazamaji nakubaliana na wewe asilimia mia moja!

Huo mfano wa practical trainings ulioutoa ni sahihi kabisa. My focus was in theory, na kuwaandaa vijana kuweza kupambana na changamoto za utandawazi. Sidhani kama kuwafundisha ufugaji, uvuvi, kuogelea, n.k pekee kunatosha bila kuwaandaa kuweza kukabiliana na changamoto wanazoweza kukutana nazo hasa kiuongozi na kupambanua mambo kinaga ubaga!

Otherwise I support your idea! It's a brilliant idea.
 
Mtazamaji nakubaliana na wewe asilimia mia moja!

Huo mfano wa practical trainings ulioutoa ni sahihi kabisa. My focus was in theory, na kuwaandaa vijana kuweza kupambana na changamoto za utandawazi. Sidhani kama kuwafundisha ufugaji, uvuvi, kuogelea, n.k pekee kunatosha bila kuwaandaa kuweza kukabiliana na changamoto wanazoweza kukutana nazo hasa kiuongozi na kupambanua mambo kinaga ubaga!

Otherwise I support your idea! It's a brilliant idea.



Kabengwe kweli kuwafundisha wanafuzi uvuvi, kuogeleoaa, kilmo cha nyuki au ufugaji sio solution pekee. Nilikuwa najaribu kuonyesha udhaifu wa elimu zetu. Binafsi nimesoma shule kando ya ziwa lakini sikujua kuogelea mpaka nikafundiswa kwa mbinde kuna siku kiodogo nizame. Hi unaona kwa kiasi fulani inaonyesha udhaifu wa carriculum za elimu yetu sababu haikunifunidisha kumudu mazingira nayoishi. Nilijifunza informally kwa kujiiba iba

Ndiyo maana nasema kama watoto wa kimasai umasaini anamaliza la saba hajafundishwa somo moja la ufugaji bora kama si vipindi vichache pia ni failure ya elimu. kama wambulu wanajua kukimbia shule za kwao ziwe na kipindi japo somo la michezo na riadha may be kwa wanafuzni wa darasa la tano na la sita.

Imani yangu elimu bora ni ile inamuwezesha mwanafunzi kuyamudu mazingira yake vizuri na kwa ufanisi.

Mfano wakati niko darasa la sita jiografia ramani ya dunia ilikuwa kichwani. Lakini cha ajabu nilishanga kusikia wamekani wengi hata walisoma wanadhani afrika ni nchi. yule mgombea urais USA Sarah Palin alithibitisha hilo.

Sasa kama mwanafunzi anamaliza darasa la saba arumeru, simajrio hajafundihwa kama si somo japo topi ya ufugaji bora tunategemea nini? Wakati huyo uyo mwanafunzi anajua mji mkuu wa USA.kwangu naona elimu ya aina hii inalenga zaidi kwenye white colar jobs. Elimu yetu ina lenga zaidi kazi za kalamu.


  • watoto wangapi wanaishia darasa la saba au form 4 na kushindwa kuendelea?
  • Je watoto/vijanan hawa wanakula na skills gani za kuwawezesha kumudu mazingira yao?
  • zaidi ya kujua kusoma na kuandika wanakuwa na mbinu gani zitazofanya jamii zao zione matunda ya elimu yao.

Sikatai watoto lazima wajifunze hesabu, english lugha but we must have customised education . Atleast to have one or two subject katila level fulani inayoendana na mazingira ya eno la shule.

Nadhani umefika wakati serikali itambue hata wanaoishia la saba na form 4 wanatakiwa kuwa na mchango wa maendeleo kwenye jamii zao. Serikali irekeibishe mitaala kiasi kwamba mtu anayemaliza darasa la saba/ form4 anakuwa ametayarsihwa at minimu level ya kujiajiri/kutoa mchango kwenye jamii yake na sio kusmsoea babu na bibi barua .

We need CREATIVE leaders with VISION . .. yaanai ngoja niishie hapa inauma sana
 
Elimu ya kati, polytechnics and colleges zipewe nafasi ku-assimilate wanafunzi ambao hawatoweza kuingia vyuo vikuu. Kutokuwa na middle ground ya elimu (btw, pia wanafunzi wengi waendao vyuo vikuu, labda wange-benefit zaidi katika sekta hii, sio kukimbilia chuoni tu) inamaanisha, wahitimu wengi kidato cha nne wanabaki bila option ya kujiendeleza zaidi kielimu.
Katika arrangement kama hii, mafunzo yanayolenga zaidi kwa wajasiria-mali zinaweza kutolewa. job specific trainings, kama carpentry, ukulima, mechanics etc zinahitajika. nafahamu VETA wanatoa elimu kama hii, lakini lengo ni kuwa na sehemu (formal) nyingi zaidi kote nchini.

katika mashule, elimu ya ziada pia ipewe nafasi. Specific interest groups/Societies(sp), clubs pia ni mjia moja ya elimu jamii inayoweza kuchangia kuelimisha na kuongeza interest katika fani mbali mbali. Hizi sio lazima ziwe examined, lakini kuwepo kwake kunamuongezea mwanafunzi general interests.

KK
Elimu | Tanzania
kotinkarwak@googlemail.com
 
Mimi nadhani tuanze na jinsi gani ya kupata walimu, tena bora. Ninakumbuka miaka ya 70 na 80 Vyuo vya elimu vikuwa na hadhi tofauti. Mfano Mwl aliyesoma Marangu,Mpwapwa au Ifunda alikuwa super. Hata chuo cha Mpwapwa kipo katika list ya vyuo vilivyopewa exemption na University kubwa duniani [I can testify], yaani Diploma ilikuwa nganzi ya kwenda Master. Hii ilito changamoto sana kwa vyuo vingine na tulikuwa na walimu bora. Tujilulize UDSM, chang'ombe,Mkwawa, Dodoma vina hadhi na ubora upi.
Pili, tuwe na vyuo vya elimu [speciality], mfano chang'ombe kitoe walimu wa science tu, Mkwawa Art, Dodoma Sociology etc, hii itawezesha kuwe na focus, kama walimu ni wabovu tutajua wanatoka wapi na kuweza kurekebisha matatizo hayo haraka.
Tatu, Wanafunzi waandaliwe kuwa watalaam wa fani zao mapema, mfano kama yupo mpiga ala aende kwenye shule za ala, kama yupo Mwalimu aandaliwe kuwa mwalimu, hakuna sababu ya mimi kuwa Daktari na nimetumia miaka mingi kukariri Mirambo, maji maji etc. Nina suggest mfumo wa zamani wa shule kama Shycom, Moshi tech, Tanga tech, Mkwawa Teach, urudishwe. Wanafunzi wachague hatima zao wakiwa form three.
Wanafunzi wafundishwe critical thinking kama alivyo suggest mwenzangu, hii habari ya mkwawa alizaliwa lini is outdated. Kwanini muda huo mwanafunzi asifundishwe Buisness planing [hata kama ni form 1 iwe buisness planing ya level yake], au project management [hata kama ni ya mradi wa bata 3 pale shuleni kwao]. Dunia ya sasa haiangalii una A ngapi, wanaangali utakuwa na impact gani katika buisness.
Pia watu wafundishwe kujiuza, A na B are nothing kama hujui kuiuza,ndio maana jirani wanasema hatujui kitu, in fact nimefanya kazi mahali kama kenya. Ni weupe kabisa interms of content, lakini ni wazuri kujiuza. Hivi kwani mambo yanayotupambaninisha na hii globalization tusiyaangalie kwa makini, leo ukiangalia CV za vijana wetu unaweza dhani hawajui, but give them opportunity! sasa si kila mtu atakuwa na fursa ya benefit of doubt, dunia iko katika fast pace.
Vyuo vikuu au sekondari zikidhi haja, sio kila mtu anabanda la kuku hii ni sekondari, ana garage ya gari chuo kikuu kishiriki. Je ana facility za kutosha!!
Na mwisho Elimu iwe elimu mbali na siasa, elimu ishughulikiwe na wataalaam wa elimu si akina Mungai au Maghembe, Wanasiasa wakae mbali kabisa ili tusije kupata akina EL wanaojenga madarasa bila walimu kwa kuchangisha wananchi huku wakishiriki ubadhirifu na wizi kwa gharama za umaskini wa watanzania, na kuwaacha fukara wa mali na elimu
 
Back
Top Bottom