Jinsi ya kuondoa madoa na mabaka mwilini

Naona watu wanatumia hii kama fursa kutangaza biashara zao badala ya kutoa ushauri mnatuwekea namba za simu
 
Habari ndugu zangu
Mke wangu anasumbuliwa sana na tatzo la kutokwa na vipele wakati wa period toka alipo vunja unga na vimenwachia makovu mwili mzima
Tumezunguka hosptal zote bila mafanikio kama kuna mtu anajua dawa au daktari anipe contact
 
Aina ya hizo cosmetics alizotumia mkuu?

Kuna mafuta yanaitwa Bio-Oil husaidia sana kuondoa makovu

Japokuwa sio kila ngozi huwa inakubaligi kuondoa makovu 100%
 
Asali inauwezo wa kung'arisha ngozi yako kwa sifa yake kuu ya kuzuia na kupambana na uchochezi wa chembechembe za bakteria katika ngozi, hivyo inasaidia kupunguza muonekano wa makovu na kuchochea afya ya ngozi. Chembechembe za umajimaji za asali na mafuta ya nazi pia zinasaidia kuboresha seli ya ngozi, pia kufanyia masaji mchanganyiko huu inasaidia kuboresha mzunguko, ukuaji na pia ufufuaji wa seli za ngozi.

JINSI YA KUANDAA MCHANGANYIKO HUU.

1) Weka kijiko kimoja cha chai cha asali mbichi katika bakuli yako safi ya mchanganyiko.

2) Changanya na kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi katika bakuli yako yenye asali.

3) Changanya vizuri na paka mchanganyiko wako kwenye eneo lililo athirika kwa kusugua taratibu kutumia ncha ya kidole chako.

4) Endelea kusugua taratibu kwa dakika moja au mbili, kisha weka kitambaa kilichochemka na maji ya moto kwenye eneo ulilopaka mchanganyiko wako mpaka kipoe.

5) Rudia hivyo kila siku utayaona mabadiliko baada ya wiki mbili.

N.B Inashauriwa kutumia asali mbichi ambayo haija chakachuliwa.

Usisahau kuleta matokea baada ya wiki mbili.

Kwa maswali zaidi andika hapo chini ili watu wajifunze usinitumie PM maana sitakujibu.

Asanteni, by Mugisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna ngozi zingine zikiwekwa asali zinawasha na kuuma je unawasaidiaje hao watu au nini wafanye cha mbadala???

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Anaweza akatumia alo vera au mafuta ya ndege anaitwa Emu na hata kitunguu swaumu pia kinasaidia.

Nazidi kuandaa masomo zaidi hapo karibuni nitaweka mmbadala wa asali na mafuta ya nazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni makovu ya namna gani hata ya moto?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa makovu ya moto asali mbichi pia inaweza kutibu kwa kiasi chake lakini mara nyingi huwa inayafanya yafifie.

Ila vilevile wakati unapopata ajali hiyo ya moto unashauriwa usipake asali kwanza ila ni barafu kwanza au maji ya baridi baada ya hapo unapaka asali taratibu na kitambaa kisafi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom