Unaongea lugha ngapi? (Binafsi Ninaongea Lugha saba(7)

Habari zenu wakuu, natumai mu wazima wa afya.
Embu tufahamu ni lugha ngapi tunazozungumza.
Binafsi ninaongea jumla ya Lugha saba (7).

1.Kiswahili (swahili)
Ni lugha ambayo ninaongea na kuandika kwa ufasaha zaidi ya asilimia 90% ukizingatia pia ni lugha mama.

2.Kireno (Portuguese)
Hii pia ni Lugha ambayo ninaizungumza na kuandika pia kwa ufasaha sana kama ilivyo kwa lugha mama hapo juu.

3.Kingereza ( English)
Kutokana na kuwa lugha ya kufundishia (language of instruction) katika ngazi ya sekondari na pia ni second official language. Hapa kuna utofauti kidogo maana ninaweza kuelewa, kuandika na kusoma vizuri sana lakini linanitatiza kidogo suala la kuzungumza kwa ufasaha zaidi na ndio maana nimeiweka katika nafasi ya tatu. 70% fluency.

4. Kimwani (mwani)
Hii ni Lugha inayozungumzwa kaskazini mwa nchi ya msumbiji na pia ni lugha inayoshabihiana misamiati kwa zaidi ya asimilia 80% na kiswahili ndio maana imekuwa rahisi sana kuielewa na kuzungumza lakini katika uandishi wanatumia mfumo wa kireno.

5. Kimakuwa (makhuwa, macua, eMakhuwa)
Hii ni lugha inayozungumzwa na jamii kubwa takribani watu ml.3 katika mkoa wa Nampula nchini msumbiji (wazee wa mtupweshi watakuwa wananielewa vizuri hapa). Ninaongea na kuelewa kwa ufasaha lakini kuandika sifahamu maana ni lugha inayotumia sana "tone" katika matamshi.

6. Tsonga (Changana)
Hapa nazungumzia lugha inazungumzwa kusini mwa nchi ya msumbiji (katika mikoa ya Gaza, nyambani na Maputo) , kaskazini mwa nchi ya Afrika ya kusini (south africa) na zimbabwe. pia ni lugha inayoendana kiasi fulani na lugha ya kizulu. Ninaongea na kuielewa vizuri japo kuandika sio sana.

7.Kihispania (Spanish)
Ni lugha iliyopo katika kundi la Romance languages pamoja kireno, kiitaliano, kiCatalan, kifaransa n.k
Kihispania ni lugha ambayo imeshabihiana sana na lugha ya kireno na hapa ni tofauti kabisa na lugha nyingine maana hii Sikujifunza nimejikuta tu naielewa vizuri ingawa kuandika sifaham sababu sijawahi kufanya hivyo kutokana na utofauti katika Lahaja zake.
kileno nakumbuk kma bonitee.bondyaa.nintee perblemar sjui ndy ina andikwa hivyo ila najua kutamka maana nshawai.kufka lichinga congres nakaguruwe nlipitaga
 
Mkuu;
Acheni kuharibu lugha za watu. Huyu anaitwa mahmoud, maana yake huyu atakuwa me utamwulizaje hivyo?? Ati; Takweenya!! Bull shit kabisa. Kwani hiyo imekuwa mwanamke?
Kama hujui vizuri usikariri uliza wenye lugha yao. si kama mnavyodanganyana kwamba Takwenya ni exclusive kwa wanawake na subhai ni wanaume tu!!! kuna wakati inatumika kotekote acha kukariri.
 
kileno nakumbuk kma bonitee.bondyaa.nintee perblemar sjui ndy ina andikwa hivyo ila najua kutamka maana nshawai.kufka lichinga congres nakaguruwe nlipitaga
Huandikwa hivi mkuu
Boa noite /boanoit/- habari za usiku
Bom dia /bon'dia/ - habari za asubuhi
Não tem problema /naunte problema/ - hakuna tatizo.
 
voce nao fala nem lingua portuguesa e estas a mentir mas porque metes assim ??? uxingondo xakuine wena ???
 
Hahahahhaha Nimefurahi sana mkuu kusoma hiyo meseji hapo ukiwa na maana "wewe wala hujui kuongea lugha ya kireno na kwanini unaongopa hivi?" Ingawa umekosea kidogo kuandika
 
Wenger nae anajua lugha 7. Na ana ukwasi wa kutosha. Naamini na wewe utakuwa na ukwasi kama Wenger.
 
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima wa afya.
Embu tufahamu ni lugha ngapi tunazozungumza.
Binafsi ninaongea jumla ya Lugha saba (7).

1.Kiswahili (swahili)
Ni lugha ambayo ninaongea na kuandika kwa ufasaha zaidi ya asilimia 90% ukizingatia pia ni lugha mama.

2.Kireno (Portuguese)
Hii pia ni Lugha ambayo ninaizungumza na kuandika pia kwa ufasaha sana kama ilivyo kwa lugha mama hapo juu.

3.Kingereza ( English)
Kutokana na kuwa lugha ya kufundishia (language of instruction) katika ngazi ya sekondari na pia ni second official language. Hapa kuna utofauti kidogo maana ninaweza kuelewa, kuandika na kusoma vizuri sana lakini linanitatiza kidogo suala la kuzungumza kwa ufasaha zaidi na ndio maana nimeiweka katika nafasi ya tatu. 70% fluency.

4. Kimwani (mwani)
Hii ni Lugha inayozungumzwa kaskazini mwa nchi ya msumbiji na pia ni lugha inayoshabihiana misamiati kwa zaidi ya asimilia 80% na kiswahili ndio maana imekuwa rahisi sana kuielewa na kuzungumza lakini katika uandishi wanatumia mfumo wa kireno.

5. Kimakuwa (makhuwa, macua, eMakhuwa)
Hii ni lugha inayozungumzwa na jamii kubwa takribani watu ml.3 katika mkoa wa Nampula nchini msumbiji (wazee wa mtupweshi watakuwa wananielewa vizuri hapa). Ninaongea na kuelewa kwa ufasaha lakini kuandika sifahamu maana ni lugha inayotumia sana "tone" katika matamshi.

6. Tsonga (Changana)
Hapa nazungumzia lugha inazungumzwa kusini mwa nchi ya msumbiji (katika mikoa ya Gaza, nyambani na Maputo) , kaskazini mwa nchi ya Afrika ya kusini (south africa) na zimbabwe. pia ni lugha inayoendana kiasi fulani na lugha ya kizulu. Ninaongea na kuielewa vizuri japo kuandika sio sana.

7.Kihispania (Spanish)
Ni lugha iliyopo katika kundi la Romance languages pamoja kireno, kiitaliano, kiCatalan, kifaransa n.k
Kihispania ni lugha ambayo imeshabihiana sana na lugha ya kireno na hapa ni tofauti kabisa na lugha nyingine maana hii Sikujifunza nimejikuta tu naielewa vizuri ingawa kuandika sifaham sababu sijawahi kufanya hivyo kutokana na utofauti katika Lahaja zake.
natamani sana kujua kifarasa na kispanish embu nipe nondo najifunzaje mdogo mdogo ila sina marafiki wanaaongea hii lugha cjui atanikosoa nani msaadaaa plz
 
mkuu mimi sijui kifaransa japo naelewa kidogo kwa kuwa nayo ni romance language ila naweza kupa msaada katika spanish
 
Hapana mkuu, Kifaransa sijui ila nikipata muda ningependa kujifunza lakini inauwia vigumu sababu sijawah pata exposure sehem wanazozungumza kifaransa maana huwa ni njia rahisi sana kujifunza lugha ngeni.
Hata mimi natamani ,japo niwahi kujfunza kama wiki mbili mwalimu akasafr,nikaishia hapo hapo
 
Kisandawe
Kiswahili
sina uhakika sana na kiingereza changu cha shule zetu za kata kama naweza uongea dk 5!!
 
Kama unajua Portuguesekwa ufasaha ni rahisi ku switch kwend kweny spanish same as ukijua French kwend kweny kiitaliano... ni lugha ambazo zinashare roots nyingi.
NB: Spanish=asilimia kubwa matamshi kama kiswahili uandishi rules kama Portugues,French...
 
Back
Top Bottom