Unaombwa kutoa Ushauri kwa huyu ndugu yetu. Je, amuoe huyu binti?

Kuchakuro Ps

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
438
507
Wakuu Salam,
Kijana mmoja alikuwa anataka kuoa binti mmoja kutoka kabila...lakini Wazazi wakakataa.
Baada ya Wazazi kuona speed ya kijana wao kutaka kumuoa huyo binti wasiemtaka inashika Kasi, wakatafuta binti wanae mtaka Kwaajili ya kijana wao, wakatuma barua ya posa na Sasa maandalizi ya harusi yanaendelea.
Sasa huyu bwana akalazimika kumuunganisha huyo dada aliyemuacha na rafiki yake, amefanya hivo kutokana na hitaji kubwa la huyo binti.
Binti anataka ndoa.
Sasa changamoto ipo kwa huyu aliyeungwa na huyu binti.
Ni kwamba yeye Kama uchumi wake ungekuwa uko Vizuri kidogo angekuwa amefanya maamuzi ya kuoa siku nyingi tu, Sasa kutokana na changamoto hiyo akawa anavuta subira.
Lakini Sasa limekuja hili aamue vipi?
Kwani kuna msukumo mkubwa kutoka kwa huyu binti, Binti anataka ndoa kwa kasi.
Huyu Binti yeye ni mwajiliwa lakini kijana hana kazi.
Tumshauri Vizuri kijana mwenzetu.
 
Huyo binti amekuwa bidhaa anauzwa kokote?

Anataka kuolewa Mkuu.
Yeye sio bidhaa, lakini mpenzi wake ameamua kumtafutia mpenzi mwingine ambae ni rafiki yake na ana Imani nae kuwa hatamfanya huyo binti ajute kumkosa yeye.
 
Usiwe na haraka, tulia uandike, stori ni yako, Hakuna anayeweza kukuwahi.
 
Back
Top Bottom