Unaomba msaada wa kufukuza mwizi, akifukuzwa unalalamika!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaomba msaada wa kufukuza mwizi, akifukuzwa unalalamika!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Freetown, Apr 29, 2009.

 1. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Habari hii hapa chini haina tofauti na kuomba msaada wa kufukuza mwizi, na ukipewa msaada huo unalalamika kwanini unamfukuza huyo mwizi.
  Iwapo serikali iliomba wananchi kutoa ushirikiano kufichua ouvu/waovu iweje tena serikari/viongozi wanalalamika??? wadau mnasemaje kuhusu hili jambo?? au ndo mambo ya JEDWALI anayozungumzia Mwanakijiji????

  SOURCE: Nipashe

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) Sophia Simba, amejitokeza na kuwatetea wanaotuhumiwa kuwa mafisadi mapapa watano waliotajwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na kusititiza kwamba kwa kitendo cha kuwataja ni sawa na lugha ya kijiweni kwamba amechemsha.

  Badala yake, Simba alisema mapapa hao ni watu safi na waadilifu kwa kuwa Mahakama haijawahukumu.

  Sophia aliyasema hayo jana kwenye Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kufungua warsha ya siku moja ya Kituo cha Demokrasia nchini (TCD).

  ``Lakini kabla sijaendelea kuna mwandishi yoyote toka vyombo vya IPP hapa? Tafadhali kama yupo atupishe,`` alisema Sophia huku akiangaza macho yake huku na kule kwa sekunde kadhaa.

  Hata hivyo, baada ya kuona hakuna mwandishi aliyetoka Sophia aliendelea ``Mengi ni nani mpaka awataje watu wale kwamba ni mafisadi, tena anawataja watu ambao ni wafanyabiashara wenzake, huenda kuna jambo jingine si ufisadi.

  ``Hatua ya kuwataja watu ambao ni wafanyabiashara kama yeye inatia wasiwasi,`` alisema.

  Waziri huyo alisema kwake watu waliotajwa bado ni wema na waadilifu kwa vile hawajatiwa hatiani kwa kosa lolote na mahakama.

  ``Mahakama ndiyo pekee yenye uwezo wa kusema fulani ni fisadi au fulani ni fisadi papa, sio Mengi, Mengi ni nani?`` alisema.

  Sophia alisema Mengi ameingilia kazi za serikali na kumtaka aiache serikali ifanye kazi yake.

  ``Na nikifika hapa, naomba nitumie neno la kijiweni kwamba Mengi kachemsha. Najua mnakwenda kunilima (kumuandika vibaya) kanilimeni, lakini maoni yangu ndiyo hayo,`` alisema Mengi alipoulizwa juu ya madai ya Waziri Simba alisema: ``Namwombea Mwenyezi Mungu amsamehe na kwa masikini wa Tanzania wamsamehe kwa sababu hajui anenalo.``

  Katika hatua nyingine, Serikali imesema itatoa tamko baada ya kupitia malalamiko yaliyotolewa na watu mbalimbali kuhusu hatua ya Mengi kuwataja hadharani `mafisadi Papa`.

  Mwishoni wiki iliyopita, Mengi aliwataja watu hao wanaotuhumiwa kuwa ni `mafisadi papa`, kuwa ni pamoja na Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz.

  Aliwataja wengine kuwa ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi.

  Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchukia, alitoa ufafanuzi huo jijini Dar es Salaam jana baada ya kuulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuhusu tamko la serikali juu ya shutuma zilizotolewa na Mengi.

  Mkuchika alikutana na Waandishi wa Habari ofisini kwake Dar es Salaam jana kwa nia ya kutoa tamko la serikali juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu kero ya muziki katika makazi ya watu.

  Alisema: ``Government moves on paper, nakusudia kupata ile tape na text ili niweze kuiangalia nijiridhishe ndipo nijue hatua za kuchukua.``

  Alisema serikali imepokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu namna taarifa hiyo ilivyotangazwa na vyombo vya habari na kwamba inachambua malalamiko hayo na kuyalinganisha na yale aliyosema Mwenyekiti wa IPP ili iweze kuyatolea maamuzi.

  ``Nimepokea malalamiko kutoka kwa watu wengi kwamba siku ile ITV haikutumika vizuri kwa hiyo tunasubiri kanda tuisikilize na tuone nini cha kufanya,``alisema.

  Kuhusu tuhuma za kuijilimbikizia `vijisenti` zinazomkabili aliyekuwa waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, Waziri Simba alisema suala hilo lipo katika hatua ya upelelezi hivyo ni kosa la jinai kulizungumzia.

  Alipoulizwa ni vipi Chenge aliweza kujilimbikizia fedha hizo, wakati kuna sheria ya maadili ya viongozi nchini, Waziri Simba alisema sheria hiyo ni kwa ajili ya Tanzania tu na haina ubavu wa kuvuka mipaka.


  ``Sheria hii ni ya hapa hapa nchini, hatuna uwezo wa kufuatilia akaunti za watu ambazo ziko nje ya nchini,`` alisema.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  whatever happened to presumption of innocence? Isnt this supposed to be HOME OF GREAT THINKERS?
   
 3. C

  Chief JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  If we take the presumption of innocence to the extreme, then no one is going to be taken to the court of law.
   
Loading...