Unaoga mara ngapi kwa siku?

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,433
12,282
Kuoga ni tabia au mazoea hujengwa tangu utoto, waliokua wavivu wa kuoga utotoni hata wakiwa wakubwa hali huwa hivyo hivyo na kinyume chake husadifu ukubwani.

Je, wewe unaoga mara ngapi kwa siku? Au waoga kila ukichafuka?

1621416982927.png

 
Hapa mnatutafuta sisi maACHIKOGI..

Mimi kutegema na chiku somo, ba! Kuna chiku kukoga mara 1,2 mpaka 3 somo, ila kuna chiku chikogi kabisa
(kwa lafudhi ya lugha ya kina harmonize)

Kuoga costant, ni nikiwa na mechi.. Hapo hapakwepeki..
 
Kuoga ni tabia au mazoea hujengwa tangu utoto,waliokua wavivu wa kuoga utotoni hata wakiwa wakubwa hali huwa hivyo hivyo na kinyume chake husadifu ukubwani.

Je wewe unaoga mara ngapi kwa siku? au waoga kila ukichafuka?
Kuoga zaidi au kutooga inategemea mazingira sehemu ulipo, unaweza upo Dar kazini, nyumbani unafika saa 10 kwa siku utaoga mara ngapi? au upo Makambako baridi kali, hapo kwa wiki utaoga mara ngapi?
 
Kuoga ni tabia au mazoea hujengwa tangu utoto,waliokua wavivu wa kuoga utotoni hata wakiwa wakubwa hali huwa hivyo hivyo na kinyume chake husadifu ukubwani.

Je wewe unaoga mara ngapi kwa siku? au waoga kila ukichafuka?
Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtata sana kuoga aisee, hii biashara ya kuoga oga ilikuwa ngumu sana kwangu, na popote nilipopata nafasi nilipiga ndefu na maza akijipindua naingia bafuni nafungulia maji weeeeeeeee nikiwa pembeni kisha najipaka maji natoka au pakitokea ugomvi au kasheshe yoyote na maza siogi! akinichapa namweleza wazi siogiii unajifanya kunichapa?

Ila mbona tangu nimekuwa mkubwa aisee naoga vibaya sana, sina tatizo kabisa na kuoga hata mara 3 kwa siku sioni shida

Nakupinga mkuu kuwa ukiwa mvivu wa kuoga utotoni itaendelea hadi ukubwani
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom