Uchaguzi 2020 Unamuonaje Dkt. John Magufuli, macho yako yanaona kama sisi?

tz yetufom

Member
Jun 18, 2020
10
21
JE, UNAMUONAJE JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, MACHO YAKO YANAONA KAMA SISI?

Mwendi R.D
+255739333332


Serikali ya awamu ya tano kupitia kiongozi mahili Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli imefanya mambo mengi na makubwa ya kimaendeleo yanayopelekea wananchi wengi ikiwemo wanyonge na wenye hali ya chini kuendelea kuwa na imani kubwa na Chama cha Mapinduzi na serikali yake kupitia maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya katika kila tarafa, usambazaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya na dawa, ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, vyoo mabweni na mabwalo ya kulia chakula, Ukarabati mkubwa wa miundombinu ya shule zilizochakaa katika sekta ya elimu. Kuboreshwa kwa Miundombinu ya maji sambamba na ujenzi mpya wa miundombinu hiyo katika kila wilaya.

Miradi mingine ni pamoja na Ujenzi wa Mradi wa kufua Umeme kwa Maji wa Julius Nyerere, Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania, Mradi wa Reli ya Kati ya Standard Gauge, Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani -Tanga, Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi, Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia – Lindi:, Makaa ya Mawe Mchuchuma na Vanadium, Titanium na Chuma Liganga,Miradi ya maji mijini na vijijini, Miradi ya Viwanda, Barabara na Madaraja, Meli katika Maziwa Makuu:, Hii yote ikiwa ni kuhakikisha kunakuwa na matokeo makubwa ya kukuza uchumi wa Tanzania.

Sisi kama jukwaa la marafiki wa Magufuli (Tanzania Yetu “Friends of Magufuli”), tunatambua kwamba, kitakwimu na kifedha miradi iliyotekelezwa ni mingi sana, na fedha zilizotumika ni nyingi sana ambazo sisi tulio wengi ambao ni watoto wa masikini na wakulima wa kawaida tusiojua hesabu na mambo ya takwimu tumemuelewa mheshimiwa Rais na tumemuona kwa njia tofauti katika mioyo yetu.

Tunamuona Mh. John Pombe Joseph Magufuli katika mioyo yetu kwa amani, umoja, furaha mshikamano na upendo ambao ameutengeneza katika mioyo yetu na kwa watanzania waliyowengi. Kila tunapoona maendeleo yaliyofanyika katika sekta mbalimbali tunamuona Magufuli katika Tanzania yenye muonekano wa amani, umoja, furaha mshikamano na upendo.

Tunapoangalia ujenzi wa vituo vya afya katika tarafa zote nchini na uboreshaji wa miundombinu ya afya, mioyo yetu inamuona Mh. John Pombe Joseph Magufuli na Serikali yeke katika hali ya kutuletea amani, umoja, furaha mshikamano na upendo kwa Wakinamama waliyokuwa wanajifungulia sakafuni, na wengine kwenda umbali mrefu kuifikia hospitali ambao kwa sasa hawana hiyo adha tena. Vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga vimepungua. Misongo ya mawazo na ugumu wa mazingira ya kufanyia kazi kwa wahudumu wa afya haupo tena maana hawahitaji kuchuchumaa tena kumuhudumia mama mjamzito katika sakafu maana vitanda vipo tele na vya kutosha katika vituo vya afya.

Tunaendelea kuiona amani, umoja, furaha mshikamano na upendo katika familia zetu kulikoletwa na Serikali ya Mh. John Pombe Joseph Magufuli kupitia sekta ya maji. Utekelezaji wa miradi mingi ya maji katika Majiji, Mikoa, na Wilaya umepelekea kinamama kupata maji katika umbali mfupi na kutumia muda mfupi ambapo huko nyuma magonvi na mafarakano yalitokea kwa wanandoa pale mama anapochelewa kurudi kutokana na umbali mrefu wa kufuata maji na waume kudhani kwamba labda kinamama huchepuka katika mahusino nje ya ndoa. Tumeyaona maji ya kutosha hata kipindi cha ugonjwa wa COVID 19 hakuna aliyekosa maji ya kunawa na hivyo watanzania wengi kuendelea kumuona Mh. Magufuli katika mioyo yao iliyojaa amani, umoja, furaha mshikamano na upendo.

Tunapoangalia miundombinu katika sekta ya elimu, ujenzi wa madarasa, vyoo, mabweni, utengenezaji wa madawati n.k tunawaona walimu wakifurahia mazingira mazuri ya kufundishia na kuongeza molari ya kufundisha kwa furaha na upendo kati yao na wanafunzi. Nawaona watoto wakijifunza katika mazingira mazuri, taaluma na ufaulu ukiongezeka kila kukicha. Ninawaona wazazi katika miyo yao wakimuona Magufuli kama mkombozi wao katika ugumu wa maisha. Elimu bure imewapunguzia mzigo maskini wengi na sasa wamekuwa mstari wa mbele kuwahimiza watoto kwenda shule badala ya kuwaficha au kuwaambia wakachunge mifugo. Tunaona shule za serikali zikifanya vizuri na kuongoza katika mitihani ya Taifa kinyume na huko nyuma tulizoea kuona shule za watu binafsi tu zingiongoza.

Tunapoangalia utelezaji wa miradi mbalimbali kama Ujenzi wa Mradi wa kufua Umeme kwa Maji wa Julius Nyerere, Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania, Mradi wa Reli ya Kati ya Standard Gauge, Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani -Tanga, Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi, Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia – Lindi:, Makaa ya Mawe Mchuchuma na Vanadium, Titanium na Chuma Liganga,Miradi ya maji mijini na vijijini, Miradi ya Viwanda, Barabara na Madaraja, Meli katika Maziwa Makuu:, mioyo yetu inajawa na furaha na amani kwa njia anayotupitisha Mheshimiwa Magufuli. Tunaiona Tanzania mpya, tunaona uchumi unaokuwa kwa kasi, tunaona ongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato na uboreshaji wa huduma za kisekta kwa maendeleo ya kiuchumi, na kijamii miongoni mwa sisi watanzana wa kawaida.

Tunaona Mishahara ikienda kuboreshwa baada ya kukamilika kwa miradi hii kwa wafanyakazi wa serikali, tunaona ajira nyingi zikienda kuzalishwa kwa ajili ya wasomi wengi walio wazawa, tunaona umeme ukishuka bei na wananchi wengi wakivuta umeme na kutumia umeme katika nyumba zao, tunaona uharibifu wa mazingira ukipungua kutokana na miradi ya gesi majumbani, tunaona watanzania wakitumia muda mfupi kusafiri kwa treni za mwendo kasi kwenda na kurudi maeneo yao ndani ya siku moja, Tunaona ongezeko la viwanda na uwekezaji mwingi baada ya uwepo wa umeme wa uhakika na usafiri wa uhakika wa treni kwa ajili ya uzalishaji na usafilishaji wa bidhaa, tunaona wananchi wakitumia usafiri wa ndege maeneo mengi ya Tanzania huku watalii wakiongezeka katika nchi yetu kupitia shirika la ndege la Tanzania.

Tunaona watanzania wengi wakiajiriwa katika mradi wa bomba la mafuta, mapato ya serikali yakiongezeka kupitia mradi hii na msululu wa magari ya mafuta ukipungua barabarani. Tunaona ongezeko la uzalishaji wa sukari nchini huku sukari ikishuka bei na wananchi wengi kuajiriwa katika sekta ya kilimo cha miwa. Tunaendelea kuona ongezeko la viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali huku wananchi wengi wakiajiriwa katika viwanda hivi na wengine katika sekta za kilimo na mifugo kwa ajili ya kuwezesha malighafi za viwandani. Tunanaona pato la taifa na pato la mwananchi mmojammoja likikuwa kwa kasi na maisha bora kwa kila mtanzania yanapatikana kupia Mh. John Pombe Joseph Magufuli na farsafa yake ya hapa kazi tu.

Haya yote yanatufanya tuwe na amani, umoja, furaha mshikamano na upendo katika familia zetu hasa sisi watanzania wengi tuliyo katika hali ya chini kimaisha na kuamua kusimama na Mh Rais Magufuli, Rais wa wanyonge, Rais mzalendo, mchapakazi, anayechukia Rushwa kwa vitendo. Sisi kama jukwaa tunakila sababu ya kuyaeleza haya kwa kutumia lugha yetu rahisi inayoweza kufikika na kueleweka kwa watanzania wengi ya kwamba tunamuonaje na tunamuelewaje Mh. Rais Magufuli.

Sisi watanzania walio wengi tunamuona na kumuelewa Mh. John Pombe Joseph Magufuli kama Rais aliyeleta amani, umoja, furaha mshikamano na upendo katika maisha yetu maana kuna muda tulipata msongo wa mawazo kwa huduma duni za hospitali, maji, mazingira ya shule, miundombinu ya umeme n.k Ni msongo huu wa mawazo uliopelekea tufanye kazi kwa mazoea, kukosekana kwa amani mahali pa kazi, furaha mahali pa kazi, mshikamano mahali pa kazi na kukosekana kwa upendo baada ya matokeo ya kazi. Lakini sasa kila sehemu watu wanaimba ni nani kama magufuli?? Na wanauliza ni nani wa kutupaisha tena zaidi ya John Pombe Joseph Magufuli??

Sisi jukwaa la Marafiki wa Magufuli tumekuelewa, na tunawawakilisha wananchi wa hali ya chini kusimama pamoja na wewe katika safari yako ya kuwaletea watanzania maendeleo ya kweli. Tunasimama na wewe Rais unayemtanguliza Mungu katika kila jambo, hata kipindi cha Covid 19 tumeona, tunasimama na wewe kwa sababu hupendi rushwa, hupendi uvivu, hupendi mazoea kazini bali kazi tu. Tunasimama na wewe kwa sababu unapenda ukweli, tunasimama na wewe kwa sababu unajali shida za masikini na watu wa hali ya chini. Tunasimama na wewe kwa sababu ni shupavu na mchapa kazi.

Hakika mwenye macho haambiwi ona, kazi zake na sifa za uongozi wake zinajisemea zenyewe. Sisi jukwaa la marafiki wa Magufuli Tanzania nzima tunakuombea kwa Mungu afya njema, hekima ya Mungu iwe pamoja nawe katika kuwatumikia watanzania kwa awamu nyingine tena kwa viwango vya juu na mwendo wa uhakika chini ya kauli mbiu yetu KAZI ZAIDI KWA MAENDELEO MAKUBWA 2020-2025
 
Umedadavua ukweli mtupu na linaenda kujidhihirisha tarehe 28/10/2020.

Naomba utunze hili andiko tunaenda kulitumia kama rejea tutakavyokuwa tunashangiliq ushindi wa kimbungq.
 
Kwa jicho la uongozi, jiwe amefeli sana, hafai kuitwa kiongozi hata wa nyumba kumi
 
Hiyo miradi na matumizi Fulani ilimuondoa CAG mcha Mungu Prof Assad, ofisini kabla ya wakati wake kikatiba.!
 
Back
Top Bottom