Unamshauri nini rais Jakaya Kikwete kuhusu mihadarati

Nchi ya lawama itakwenda kilawama lawama mpaka lawama ziwatokee puani
yeye kamsadia ray c wewe umesadia nani?
Sidhani hata kidogo kama rais anatafuta umarufu kwa kumsadia ray c.vp wale walemavu anawapa bajaji
ama kweli tenda wema wende zako usingoje shukurani
 
kwanza unatakiwa ufahamu kuwa inapotokea mtu akasaidia mtu mmoja au akasaidia jambo moja,na wewe unatakiwa usaidie jengine.sio mtu anamkirimu mtu "a"wewe unalaumu kwanini hakumkirimu na mtu "b".unachotakiwa ni kumuunga mkono.kuhusu kupambana na madawa ya kulevya kwa ujumla;mara kadhaa kikwete anakemea kweli kweli kwenye hutuba zake.labda kama huwa humsikilizi maana kuna watu hawasikilizi halafu baadae wanaanza kulalamika.utasikia 'hamna cha maana alichoongea" ukimuuliza ulimsikiliza? Anakuambia "hapana ila namjua".kuhusu kukamata;kuna kutengo maalum cha kupambana na madawa ya kulevya na kinafanya kazi.kama kuna uzembe,ni kwa watumishi hao ambao kimsingi ni wasomi na si wanasiasa.si sahihi kudhani kama rais atakuwa anakamata mwenyewe mannualy.

Ni jambo jema kumpa support msanii wa aina ya Ray C kwenye suala kama hili kwani impact yake katika kutoa ujumbe kwa jamii kuhusu athari za madawa ya kulevya na uwezekano wa kuachana nazo ni kubwa kutokana na ukweli kwamba Ray C ana mashabiki wengi sana wa kizazi kipya katika taifa letu na nje ya nchi ambao ndio victim wakuu wa matatizo haya.

Lakini ingekuwa jambo jema zaidi kama angeshughulikia kiini cha tatizo hili. Kama alivyosema wakati wa kuingia ikulu kwamba anayo list ya hawa majambazi wa madawa ya kulevya. Na kwa kweli aliposema maneno haya ulikuwa unaweza kuhisi kabisa dhamira yake ya kuwashughulikia hawa wahalifu. Sasa kipindi chake cha uongozi kinaenda ukingoni na hakuna hata papa moja la majambazi hawa lililokamatwa na kuwekwa ndani.

Hii inadhihirisha kwamba CCM ni mfumo hatari sana. Wakati alipokuwa hajakaa kwenye usukani wa mfumo huu wa kiharamia, aliona kupambana na wahalifu hawa inawezekana kwa sababu yeye ndio mwenye sauti ya mwisho sasa kama Rais. Lakini kadri alivyokuwa pale ikulu, akakuta kuna mifumo ndani ya CCM ambayo haigusiki kwa sababu ndio inayoubeba mfumo mzima wa chama. Ukiigusa tu basi chama chote kinaporomoka na maisha yako unayaweka rehani.

Sasa suluhu kwetu watanzania ni kuung'oa mfumo mzima wa CCM madarakani. Bila hivyo basi kila atakayekuja kupitia CCM atakuwa na hadithi tamu ambazo hazitekelezeki. Juu ya uharamia wote wanaotufanyia kwenye kila nyanja inabidi tuwe na huruma nao. Tuwape mda wa kukaa benchi ili wapate mda wa kutubu dhambi zao mbele ya mungu wao kila mmoja kwa dini yake wakati bado wako hai. Tuhakikishe 2015 tuna Tanzania bila CCM kwenye ngazi zote za uongozi kuanzia ngazi ya mtaa.
 
Back
Top Bottom