Unampa heshima gani au nafasi gani katika maisha yako anayekusaidia kulea watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unampa heshima gani au nafasi gani katika maisha yako anayekusaidia kulea watoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by telitaibi, Jul 20, 2012.

 1. telitaibi

  telitaibi JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Waacheni watoto waje kwangu wala msiwazuie kwani ufalme wa MUNGU ni wao.

  awe mke au dada au msichana wa kazi, anyone ambaye anaishi na wewe wakati wa kulea malaika hawa unampa nafasi gani na wewe unachangia vipi katika ukuaji wa watoto wako kwani wanakuwa na kufata wale walio wazunguka.

  JIILIZE COME NA JIBU TUFUNDISHANE HAPA MAMBO YA KUJISAHAU NI HASARA KUBWA

  Matendo na maneno yenu?

  ukaribu wenu na ukarimu wenu vipi?

  mahusiano yenu vipi?

  je mnapendana na kusaidiana

  Kumbuka mchicha hauzai pera itabaki kuwa mboga ya majani.
   
 2. telitaibi

  telitaibi JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hapo inakuaje nasi tumepitia tukiwa watoto
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Ngoja nije kwanza . . . . . . .
   
 4. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa vizuri..Una maana ya ma house girl wetu au sisi wenyewe?

  Sina cha kumpa ila nampenda sana house girl wangu...mpaka watu wananishangaa kuwa labda na over do. Nilikuwa nje ya nchi niakenda kununua viatu vya kila mwana familia..nilikuwa nimeongozana na mtanzania mwenzangu. Nilipomwambia hivi viatu namnunulia house girl alinishangaa sana afu nilipomuhoji kwa nini ...akaona soo akaanza kusema...mimi house girl wangu hawezi vaa flat shoes..nkamuuliza why?..akasema ni mshamba anaona virefu ndio bomba...nikamwambia wakwangu si mshamba...amekaa mjini zaidi ya miaka 5 hivyo anajua kila fashion inayoingia. Lakini nilijua alichokuwa anashangaa ni kwa nini nanunua viatu vya bei kwa ajiri ya house girl

  Kwa kuwa nampenda sana house girl wangu na yeye namuona wazi anawapenda sana wanangu...kiasi kuwa kuna kipindi anawatetea hata wanapotaka kuadhibiwa wakifanya makosa.

  House girl si msomi hivyo sitegemei awe role model wa wanangu ila what I need from her ni kuwapenda wanangu that's all. Akiwanyanyasa nikiwa sipo basi wanangu watakuwa wahoga na watakuwa wajinga hata wakifika mashuleni. Malezi mengine ni jukumu langu na baba yao.
   
 5. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi house girl kwanza ndugu baadae. yani niko radhi nsimnunulie ndugu yangu zawadi nimnunulie house girl kwani ana msaada mkubwa sana kwangu ambao siwezi kuulipa kwa mshahara wowote ule zaidi ya kumpenda.
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Sijakufahamu
   
Loading...