Unamnunia mumeo/mpenzi wako: Kisa umemuona rafiki yake na mwanamke mwingine! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unamnunia mumeo/mpenzi wako: Kisa umemuona rafiki yake na mwanamke mwingine!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Feb 17, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nimeshakutana na kisa hiki kwa jamaa watano. Wapenzi wao wa kike kwa nyakati tofauti walishawahi kuwanunia tena kwa siku nyingi kisa eti waliwaona marafiki zao wakiwa na wanawake wengine tofauti na wanaowajua wao.

  Mwanzoni niliona ni jambo la kawaida nilipoambiwa na mtu wa kwanza. Hata hivyo, kutokana na matukio kuwa matano, inaonekana inawezekana hii maneno ikawa inawatokea wanaume wengi sema tu hawaongei. Lakini tujiulize jamani, hivi kama tukiendesha mapenzi yetu kwa kutumia tabia za wengine, si itakuwa kila siku mtu unalala 'mzungu wa nne' na mpenzio kwa tatizo ambalo hata halihusiani na mapenzi yenu?

  Ieleweke mapenzi ni taasisi binafsi, kamwe isihusishwe na matatizo ya uhusiano wa wengine. Kina dada ni kweli huwa mnaona uchngu shostito wako anaposalitiwa, lakini uchungu huo usiuhusishe na mapenzi yako na bf wako. Utajiharibia maana vidume vingi havipendi kuhusishwa na 'kesi' za watu wengine za mapenzi.

  Ni hayo tu kwa sasa!
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wana haki ya kutishia nyau manake wamekubaliana watengenezo security ring so mmoja wapo akinyolewa wanajua nini kitawakumba with time
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  hujanijibu ile maneno ya kusafisha meno bana!
   
 4. sister

  sister JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  sa jamani ukiona shost wako anafanyiwa hvyo nawe unahisi your boy anafanya hvyo mana kama yule ni rafiki wa bf wako anafanya hivyo mbele yako na ya bf wako basi dhahili wanafichiana siri na ukute wa kwako anafanya hvyo.
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  nafikiri message delivered, ila kwa kifupi sisi sote akina kaka na nyie wadada tuwe waaminifu, kwa kufanya hivi, haya yote hayawezi kutupata.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Na hapa ndo kale kausemi kuwa wanawake wote mwalimu wao mmoja kama sio kipofu unapotamalaki. Kwa hiyo mumeo naye akimfumania shostito wako na njemba nyingine akirudi hme akufanyeje wewe mkewe ambaye ni mwaminifu kwake! Ndo shida ya kuishi kwa hisia dada yangu.........yaani women basi tu!!!!!!!
   
 7. m

  miriamjoseph New Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi sioni haja ya kumnunia mtu!ila ni kutahadharishana tu?!ofcoz ata kama ni wewe uta kuwa unawasiwasi wenyewe wanasema leo kwake kesho kwako,alafu ndege wanao fanana huruka pamoja!....
   
Loading...