Unamkumbuka nani katika maisha yako ya shule ambae ungependa uonane naye?

Itezi

JF-Expert Member
Feb 8, 2014
389
95
Wana Jamiiforums je unamkumbuka nani katika maisha yako ya shule iwe ni primary, O- level, A- level au chuo ambaye ungependa uonane naye, lakini hujui yuko wapi?

Binafsi namkumbuka dada mmoja alikuwa anaitwa Beatrice Magwira niliachana nae mwaka 1990 pale Morogoro shule ya Ifakara Wilaya ya Kilombero yeye akiwa kidato cha pili, kwao ilikuwa ni Mzinga kambi ya Jeshi, kama yuko humu au kuna mtu ana taarifa zake naomba anijulishe hata kwa PM tafadhali nina deni nae huyu dada (nawiwa).

Kwa mara ya mwisho nilipata habari zisizo rasmi kuwa ni mwalimu huko Dodoma.
 
Benjamin mwinyindege Nyasho Primary school Musoma mwaka 1988 mkuu upo wapi au kwa yoyote mwenye taarifa nae
 
Duhhhhhh Hilo ni deni la fedha au kuna kingine ?? Tangu mwaka wa 1990. Duhhh madeni mengine ni kusamehe tu .

Mimi nawiwa kwenye nafsi maana aliyonitendea ni makuu,,,,,, tulipotezana, si unajua tena kulikuwa na S.L.P tu wakati huo,,,,
 
Anaitwa Anneth Sempombwe tulisoma wote Kanyenye primary school Tabora hiyo, nilikuwa nampenda kinoma na nimekuja kuonana nae juzi juzi tu hapa ana fanya kazi mahakama kuu ya mkoa Mwanza halafu eti keshaolewa!!
 
mm namkumbuka mschana mmoja hivi aliniacha moshi technical 2013 alipomaliza form4 mm nikiwa form six..anaitwa joana metoja..nilikua nampenda kwa dhati ila ndoivo tena nilimpenda kipindi anakaribia kuhitimu xo hatukuzoeana kiivo
 
Salama Mohammedi ALGHAITHANY GOOD SAMARITAN SCHOOLS
POPOTE ULIPO NAKUPENDA SANA SANA SANA
Nimesahau ghorofa yenu mnyoishi pale mnazi mmoja natumai tutakutana tena
 
shamila ibrahimu,stela david,na atuganile tulikuwa wote kenton high school naomba mnitafute
janeth nyamuhanga and jackline nyamuhanga(twins) na fadhila shedewa tulikuwa wote st hellen's academy kama mpo humu naomba mnitafute nawamiss sana
 
Namtafuta dada flani hivi anaitwa ROSEJANET MRUMA, nlimwacha pale muheza highschool, nna deni nae....2010,nataka nimlipe
 
Kuna mudada alikuja geto sijajua kufinya hadi akalala bonge la usingizi nami natoa vimacho toka siku hiyo hakuja tena
 
Kuna rafiki yangu tulisoma nae nursery school. Alikuwa anaitwa Ania Rashid, binti wa bwana McBel aliekuwa na hotel korogwe.

Huwa namuwaza kweli
 
Back
Top Bottom