Unamkumbuka marehemu Jerry Nashon Dudumizi?

Hizo ndo zilikuwa lyrics za ukweli, sio siku hizi wimbo kuanzia mwanzo hadi mwisho umejaa yoyoyoyo.

By the way pole kwa kisago cha jana.
Yeah. ..naona mistari ilikua ya ukweli kweli.

Halafu nilisahau sijui hata nimekuquote ya nini! Asante nimeshapoa.
 
Pendo mimi mumeo kazi yangu ni kibarua wa kuponda kokoto hapa mjini pendo oooh
duh nimekikumbuka kibao hicho jamaa aliingia na gia kuwa nI mkurugenzi wa Shirika kumbe wapi ila baada ya kukiri mke alimuelewa na kumwambia ajiendeleze kwani elimu haina mwisho.
 
Jerry Nashon alikulia katika kijiji kiitwacho Kigera kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma jirani na shule ya Sekondari Mara. Jerry alianza kujifunza gitaa akiwa Musoma Catholic Mission club ambayo leo ni Mwembeni secondary School. Alikuwa ana mazoea ya kwenda kwenye hiyo social club ya kanisa iliyofanya kazi nzuri sana ya kuwaunganisha vijana wenye vipaji mbalimbali. Alijiunga katika bendi ya Special Baruti Band iliyokuwa na Rashid Ruyembe mwaka 1980. Jerry alianza kuendelezwa na Charles Koya ambaye wakati huo alikuwa mpiga rhythm wa bendi hiyo. Alikuwa mwanafunzi mzuri na baada ya muda mfupi alikuwa mpigaji mahiri na akaweza kurekodi na bendi yake hiyo katika studio za Tanzania Film Company, RTD na hatimaye katika studio mbalimbali nchini Kenya. Jerry na Special Baruti Band walifanya maonyesho mengi katika jiji la Nairobi , katika kumbi na club mbalimbali kama vile Bombax Hotel, Kaka Night Club, Rwadhia Night Club na nje ya Jiji katika mikoa takribani yote ya Kenya kasoro Mombasa na Kisumu. Katika kumwona kiongozi wa bendi hiyo, ambaye ndiye alikuwa mtunzi na mwimbaji akipata umaarufu mkubwa nae akaona heri ahame kutoka upigaji wa rhythm na kuwa mwimbaji mtunzi. Taratibu alianza kujifunza na juhudi zake zikaonekana na Jeshi la Magereza Musoma nalo likamchukua akajiunge na Magereza Jazz Band. Baada ya miaka miwili na nusu hivi akiwa na Special Baruti Band Jerry alihamia Dar es Salaam. Wakati huo mji wa Musoma ulikuwa na bendi nyingine, kulikuweko na Musoma Jazz Band waliopiga kwa mtindo wao wa Segese, Mara Jazz Band maarufu kwa mtindo wao wa Sensera, pia ilikuwepo bendi iliyomilikiwa na Seminary ya Kikatoliki ya Makoko, hii iliitwa Juja Jazz band , haikuwa na mtizamo wa kibiashara hivyo haikuwa na umaarufu kama zilizotajwa hapo juu. Jerry alidumu kwa muda Magereza Jazz band kasha akahamia Bima Orchestra nahatimae Vijana Jazz Band mpaka mauti yake.
 
immaculata mama,napiga tarumbeta sikuoni bibi....
ni umbali gani uko uliko,nipigie simu nambari 29691.....
Sio hivyo ni 26561
Haki ya ***** nakupenda makurata ( hapo mbele akaimba lugha ya kwao namanyele)
 
Hapana, visa vya mesenja umeimbwa na Max Bushoke akiwa na Bima lee Orchestra.Dudumizi ameimba VIP, Top queen na nyinginezo. Jamaa ana sauti tamu sana, RIP.
Kuna wimbo unaitwa Ibrahim, ni kisa kinachofikirisha sana.
Ibrahim alipata Telegram(mfumo wa zamani wa mawasiliano, siyo hii ya kisasa ya kwenye android),kuwa mkewe kafariki, mke ambaye alikimkimbia Ibrahim baada ya kupata ajali na kuvunjika miguu, mke akasepa na watoto.
Kabla ya telegram ya kifo cha mke wa Ibrahim, ilitangulia telegram ya kifo cha mama wa Ibrahim. Swali likaja, je akamzike yupi?
Jerry Nashon anasimulia kisa hicho kwa hisia na kumshauri "akamzike mama kwanza, mama ni mama na mke ni mke, nenda kamzike mamaaaa"
Mke utapata mwingine na mama hutampata tena"
Wimbo huo upo youtube na Eddie Nassoro, kwa anaehitaji kuusikiliza andika:
Ibrahim Jerry Nashon zilipendwa, utaupata youtube.
 
kama sikosei jamaa alifariki 1994 wakati huo niko 6 Mapambano shule ya msingi! Miaka inakwenda kweli!
Hivi Jerry Nashon(R.I.P), Eddie Sheggy(R.I.P) nani alianza kufariki?
Aisee 1994 hadi leo ni 26yrs, umri wa mtu mzima.
 
Hivi Jerry Nashon(R.I.P), Eddie Sheggy(R.I.P) nani alianza kufariki?
Aisee 1994 hadi leo ni 26yrs, umri wa mtu mzima.
Eddy Sheggy alifariki baadae sana. Miaka ya 2000's hivi.
 
Katika nyimbo zote alizoimba Jerry Nashon, hii ya Pesa Zanisumbua ameimba kwa hisia kali sana. Ni nyimbo ambayo naisikiliza mpaka leo hii ikiwa imejaa huzuni, huruma, na tumaini huku akinguruma na sauti yake ya Dudumizi. Mwenyezi Mungu Amlaze Mahala Pema.
 
Back
Top Bottom