Unamkumbuka marehemu Jerry Nashon Dudumizi?

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,346
4,605
Kwa wale watu wa miaka hiyo bila shaka mtakumbuka umahili wa bwana huyu katika medani za muziki wa dansi....R.I.p Jerry Nashon Dudumizi
 

Attachments

  • 1437843596840.jpg
    1437843596840.jpg
    42.4 KB · Views: 1,052
Duh!jana tu nimepata kuisikiliza top queen of morroco road ikimzungumzia Regina.Pana vyuma vimemezwa na ardhi.
 
Dah nilikuwa mdogo lkn nimesikiliza pia na jamaa wengine wakali wa miaka hiyo ya nyuma Mabeno Villa Issaya Mwinamo and the like
 
Kabla ya kuwa Vijana Jazz alikuwa Bima Lee ambako pia aliwika sana... RIP DUDUMIZI
 
ameimba nyimbo nyingi sana akiwa Bima lee Orchestra ikiwemo hiyo uliyoitaja.
Ndiye aliyekuwa mhimili wa bendi ya Bima. Katika mitindo kama 'bima ndele, 'tingisha' nk. Alianzia kuimba akiwa vijana jazz kama mpiga gitaa na jina la dudumizi linaelezwa alipewa na hemed maneti wakati wakiwa mazoezini alipomsikia akiimba na kusema anaimba kama dudumizi, jina likashamiri mpaka kuwa maarufu.
kumbuka dudumizi alianza Vijana Jazz baadae akaenda bima lee. Ametunga na kuimba nyimbo nyingi akiwa Bima lee akishirikiana na Shaabani dede, Eddy Sheggy, Jafari homange, Athumani Momba,na wengine wengi tu waliopita Bima lee. Dudumizi ni moja ya aina ya waimbaji ngumu sana kuwapata kwa sasa.
Namkumbuka kwa wimbo wake wa Pesa Zinanisumbua (Mwamvua)
Ametiririka mpaka akaweka vionjo vya Kijaruo!
 
kama sikosei jamaa alifariki 1994 wakati huo niko 6 Mapambano shule ya msingi! Miaka inakwenda kweli!
 
....baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa, na kisirani cha kufokewa na boss, nahitaji vip, wakunibembeleza, so kwa maneno ila kunitomasa tomasaaah na mikono yako lakini yenye bangiliii...hiyo ni sehemu ya wimbo wa VIP aliyoimba marehemu Dudumizi. R.I.P
 
VIP, Thereza, zile nyimbo acha kabisa
Nasema kwa heri kwa uchungu moyo wangu unawaka aa Therezaaa.

Najiuliza kila mara nakujuta moyoni ni penzi gani analokupa huyoo, ni dawa gani aliyokunywesha ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi.
 
Nasema kwa heri kwa uchungu moyo wangu unawaka aa Therezaaa.

Najiuliza kila mara nakujuta moyoni ni penzi gani analokupa huyoo, ni dawa gani aliyokunywesha ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi.
Hahahaaaaa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom