Unamkumbuka Lumola? Mgombea Ubunge (CHADEMA) Bukene

NAJYUZ

JF-Expert Member
May 10, 2021
480
1,000
Na Thadei Ole Mushi.

Mwaka 2020 kupitia hapa hapa Social Media nilimpata Mdogo wangu wa Hiyari anayeitwa LUMOLA Steven Kahumbi.

Ilikuwaje?

Huyu Dogo amezaliwa Tumbo Moja na Mbunge wa Nzega Dr. Hamisi A. Kigwangalla . Dogo yeye akiwa Chadema na Hamis yeye akiwa mwana CCM mwandamizi.

Kutokana na wawili Hawa kuwa vyama viwili tofauti undugu wao uliingia Dosari kipindi Cha Kampeni za 2020 pale ambapo LUMOLA aliamua kujitosa kwenda kugombea Ubunge Jimbo la Bukene.

Kwa njia anazozijua Hamis akawa anamhujumu Mdogo wake pamoja na uwezo mkubwa ambao Dogo alikuwa anao hasa kwenye Hoja zake zilizomfanya kutamani kuwa Mbunge.

Hujuma zile zilimpelekea LUMOLA kunitafuta inbox na tuliongea Sana. Nilimsikiliza nikavutiwa Naye Sana. Ni wiki hiyo hiyo alikuwa akielekea Dodoma kufuatilia Rufaa yake ya Ubunge baada ya Mkurugenzi kule Bukene kutupilia Fomu zake za kuomba Ridhaa hiyo mbali.

LUMOLA alikuwa na Budget Kidogo Sana na Kwa jinsi mambo yalivyokuwa kule Dodoma ilimlazimu Mtu hasa Mpinzani kukaa zaidi ya wiki mbili kufuatilia Rufaa yake.

Nilikuja na wazo hapa kuwa pamoja na kwamba mm ni Mwana-CCM nilitamani Sana kumuona LUMOLA akiwa Bungeni hivyo kupitia Ukurasa huu niliwaomba mumuunge mkono wa kumchangia chochote akiwa huko Dodoma na mlifanya hivyo.... Pitia link hii kuona post ya kuwaomba mumchangie.CCM wenzangu walinipinga Sana na kuniona kama Msaliti lakini niliendelea kuamini ninachokiamini.

LUMOLA HAKUWAHI KUNIAMBIA HII SIRI

Amesoma Degree Kwa Miaka nane. Hili Hakuwahi kuniambia Hadi Jana alipohitimu.

Jana tarehe 02 December 2021 amekamilisha safari aliyoianza miaka 8 iliyopita DIT.

November 2013 Lumola alichaguliwa kujiunga na masomo ya Shahada ya Uhandisi Umeme na Mawasiliano Angani (Bachelor of Electronics and Telecommunications Engineering). Shahada ambayo angeipata 2017 lakini mambo yakawa tofauti. Tabia yake ya Harakati na kupenda Haki na Usawa ikamgharimu miaka mingine minne zaidi na jana ndio imekuwa kilele cha masomo yake DIT.

Mwaka 2014 Lumola akiwa Waziri Mkuu DITSO. Utawala wa DIT walitoa Tamko kwamba Wanafunzi ambao hawajalipa Ada hawatoruhusiwa kufanya mitihani na badala yake waahirishe mwaka huo wa masomo. Inakadiriwa zaidi ya Wanafunzi 600 walikuwa hawajalipa Ada. Serikali ya Wanafunzi waliomba sana Wanafunzi husika wapewe mitihani lakini wasipewe matokeo mpaka watakapolipa Ada lakini msimamo wa Taasisi haukubadilika.

MAANDAMANO

Baada ya jitihada za mazungumzo kutozaa matunda Lumola aliongoza Maandamano kwenda ilipokuwa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia kipindi hicho Waziri alikuwa Mbarawa na Naibu wake alikuwa January Makamba na Katibu Mkuu alikuwa Profesa Patrick Makungu.

Pamoja na vizuizi vya Polisi kwenye Kona ya Bibititi na Akiba Lumola na wenzake walifanikiwa kufika nje ya Jengo la Wizara.

Bunge la Bajeti lilikuwa likiendelea hivyo Waziri na Naibu hawakuwepo. Wanafunzi walimkuta Katibu Mkuu Prof. Makungu ambaye alitoka nje ya Jengo akawauliza Wanafunzi mmekuja wengi sana naomba mnitajie mtu mmoja ambaye anaweza kunielezea vizuri nikaelewa kilichowaleta wizarani. Umma wote wa Wanafunzi ukasema Waziri Mkuu

Lumola akamuelezea Kisha Prof. Makungu akasema nakuja tuyazungumzie chuoni kwenu.

Yalijiri mengi lakini Profesa Makungu alivutiwa sana na Hoja za Kina Lumola na wenzao kwamba Wanafunzi wote wapewe mitihani lakini ambao hawajalipa Ada wasipewe matokeo mpaka watakapolipa Ada. Hivyo kwa niaba ya Wizara KM Makungu akaagiza Wanafunzi wote wapewe mitihani.

TAMKO LA WAZIRI MKUU

Kutokana na impact ya mgomo wa Lumola na wenzake aliyekuwa Waziri Mkuu JMT Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda alitoa Tamko kwamba Taasisi yoyote ya Serikali isizuie Wanafunzi kufanya mitihani kwasababu hawajalipa ada.

FUNZO KWA VIJANA.

Kwa nafasi (Fursa) aliyokuwa nayo Lumola kupitia kaka yake ambaye alikuwa Waziri angelikuwa kijana Mwingine angelibadilika na kuwa Chawa Pro- Max. Kupitia kaka yake Lumola angelimaliza Chuo Tena Kwa GPA kubwa kabisa na angelipata Kazi kupitia Connection ya kaka yake. Leo Lumola angelikuwa katakata haswa na Usafiri anao na hata nyumba Nzuri tu. Yote hayo aliyaacha akaamini katika fikra na ndoto zake. Hili ndilo lililonisukuma kuwa Naye karibu sana.

Huyo ndio Lumola Hongera sana kaka kwa kukamilisha masomo yako DIT. Na Lumola anabaki kwangu kama Moja ya Vijana walioiweka Imani yangu ya CCM hatarini.

Credit:Thadei Ole Mushi
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,446
2,000
Kwa kweli hata mimi huwa nakaelewa sana hako ka dogo! Ni moja ya vijana wanajielewa hapa nchini! Na ipo siku Lumola atakuwa mbunge wa Bukene!
 

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
5,556
2,000
Huu mgomo me mwenyewe nilikuwepo , hapo chuoni, Ilikuwa asubuhi na mapema tunatoka ghetto kuelekea chuoni kufanya mtihani, tunafika tu tunakuta watu wako nje , yoyote aliye jaribu kuingia kwenye chumba Cha mtihani alitolewa nje, Tukauliza Kuna Nini hapa tukaambiwa kunamgomo.

Baada ya mda kidogo wakatukusanya kipindi hicho raisi wa serikali ya wanafunzi ditso akiwa Elihuruma Himida, tukaandamana mpaka wizarani. Tukakutane na huyo katibu wa wizara ya elimu .Ambaye baadae alikuja chuoni kuzungumza na wanafunzi.

Tukiwa DH profesa mkuu wa chuo walimdisi Hadi basi.

Baada ya wiki mbili wanafunzi wote tulifamya mtihani, ila baada ya mtokea watu kibao walikamatwa na carry nyingi zilitokea. Stori ndefu sana niishie hapa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom