Unamiliki iPhone ya macho matatu wakati hata kiwanja huna, wewe ni bure tu

Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure
Wapo wengi hao,vijana wa kizazi hiki tabu sana,nilikutana na kijana graduate kabisa,yupo na ajira,28yrs Bado anakaa nyumbani,salary laki 4,Kuna siku nikamuona ana simu ya apple,kuuliza akasema amedunduliza mishahara ya miezi mitatu Ili apate milioni akanunua cm,Tena haoni hatari kabisa.
Anataka aonekane kwamba ana cm,
Ikabidi nimpe makavu,
Nikamuambia hiyo salary yake mi nilikuwa nalipwa 12 yrs ago!!aache ujinga,atafute gheto,awekeze pesa yake,unachokiona Cha maana sana leo,ndani ya 10 yrs kitakuwa hakina maana,sasa Cha nini?wekeza kwenye vitu vya kujenga uchumi wako,kama nyumba,viwanja,
 
Acha kuwapangia watu vipaumbele vya maisha, tumetofautiana preference vipaumbele na vionjo.. Wewe unawaza kiwanja kama ndiyo top notch ya mafanikio katika maisha, Mwingine hawazi unavyo waza wewe. Mwingine mafanikio katika maisha yake ni kukaa Kidimbwi na kunywa moet chamdor na hennesy za laki na nusu.. mwingine mafanikio yake ni kushika amri kumi za mungu...
Unatumia simu gani wewe..?
...kweli mkuu... Mwingine kilele cha mafanikio yake hapa jijini ni kuwa ka IST kake...mwinginge ni kumiliki boda boda Tano...mwingine ni kumiliki VX kama ya Wabunge!..basi ili mradi kila mmoja wetu ana ndoto zake. Tunatofautina. Na ndio maana dunia yetu ina raha sana. Tunatofautiana....
 
Mkuu una Fikra Fupi sana.. Kila mtu anainjoi maisha kwa namna apendavyo.. na hatufanani katika mizani za mafanikio.

Wewe mafanikio yako unayapima kwa kujenga etc. Wengine hupima yao kwa kumililiki macho matatu.

Ndio maana huwa napenda kusema "Mafanikio Makubwa katika Maisha ya Mwanadamu ni kuishi maisha yake kwa namna apendavyo"

NB: sina macho matatu wala kiwanja.
...Umemaliza Mkuu!
 
Kiwanja alichonunua mtu miaka ya 80s pale ubungo au magomeni asaiv anaweza kuuza shilingi ngapi??
Na mtu alienunua iPhone mwaka Jana na akitaka kuuza mwaka huu au mwaka ujao anaweza uza hio Simu bei hiohio??
Just think, kiwanja ni asset nzuri sana kuliko Simu, but kila mtu ana malengo ake na matamanio yake
...Neno
 
Hivi mimi niwaze kununua kiwanja cha nini sasa mkuu wakati dingi yangu ashajenga mijumba kibao hapa town. Hayo si ni matumizi mabaya ya pesa?

Mkuu usipende kupangia watu. Wakati wewe kipaumbele chako ni kununua kiwanja Kisemvule kuna wenzako walishavuka hizo stage zamani sana.

Wakati mwingine anawaza anunue gari ya kifahari Elon Musk anawaza Mars Colonization.

Mkuu hebu google hili somo "hierarchy of needs". Huko utapata kujifunza kitu
Mwambie bana,wote tukijenga nani atapanga?

Aendelee kununua viwanja,sisi tunatembea na viwanja vyetu mfukoni,komaa kununua dunia kama unaishi milele.
 
Tofautisha need na necessity.Kuna aina za watu neno kiwanja kwao walishavuka zamani hawahitaji kununua kiwanja hata kama hana lakini familia yao ina uwezo wana viwanja vingi sana hawezi kuwaza ushombo wa kitu kiwanja.Tembea uone mengi mtoa mada hujatembea.

Hivi unajua Marekani,Ulaya kwa kwetu Africa nenda tu hapo Kenya na Ushelisheli unakuta viwanja hakuna na hata sehemu ya kuzikwa hana unafikiri mtu kama huyo atajitesa asiwe na simu nzuri kisa hana kiwanja.Umasikini wako wa kimawazo usimtie mtoto wa mwenzio.Ulaya kuna watu hata hatua moja ya kujenga hawezi pata lakini ana usafiri hii sio need ni necessity.

Simu zimefikia mahali sasa sio luxury ni necessity.Wakati simu za mkononi zinaingia miaka ya mwanzo ya 90 ukiwa na simu ya mkononi tu mtu anakuzodoa utamilikije simu huna kiwanja.Simu sasa hivi ni kila kitu ni computer na ni ofisi unayotembea nayo.Sasa hivi unaweza omba chuo au hata kukata ticket ya ndege au kulipia maji au umeme kwa kutumia tu simu.

Hivi hawa Watanzania wenzetu wenye asili ya Asia unaweza niambia wanashobokea viwanja vya kazi gani wakati wanaishi mjini nyumba za msajili cha muhimu kwake ni usafiri na mawasiliano.

NARUDIA TENA UNALOWAZA WEWE MWINGINE ATAKUONA BADO UKO KWENYE UJIMA DUNIA YA OLD STONE AGE.ULAYA NA MAREKANI WATU HAWAWAZI KUJENGA VIWANJA HAKUNA VIMEHODHIWA NA MATAJIRI WANACHOWAZA NI KUWEKA LEASE LABDA YA MIAKA 99 AU KUNUNUA APARTMENT.
Umeongea mengi lakini ni PUMBA TUPU; mtoa mada hajawaongelea hao unaosema kwao wana viwanja. kawaongelea makapuku ambao hata hela ya kula ni shida na anaishi nyumba mbovu ya kupanga badala ya kununua kiwanja ananunua simu ya bei mbaya cha muhimu anachofanya na hio simu ni kuangalia umbea instagram,facebook na kutuma messages whatsapp; hana lingine lolote na hio simu ilio mcost pesa nyingi sasa huo si ujuha!!! Kingine ulaya watu hawajengi nyumba wewe, nyumba wanazikuta zishajengwa tena na serikali hata wenye pesa zao ni kununua tu. Hata hao matajiri wenye eneo kubwa la ardhi pia, hawaruhusiwi kujijengea tu kwa vile wana pesa lazima wakubaliwe kujenga na serikali hizo ndio taratibu zao. Simu nunua ya bei mbaya lakini iwe at least iwe inakuingizia pesa pia sio show off za samaki samaki huku pa kulala dhofli hal.
 
sijaandika Pumba bro najua nilichoandika hata kama mtu ni kapuku kila mtu ana plan za maisha yake huwezi lazimisha unachofikiria wewe mwingine afikirie.
 
Umeongea mengi lakini ni PUMBA TUPU; mtoa mada hajawaongelea hao unaosema kwao wana viwanja. kawaongelea makapuku ambao hata hela ya kula ni shida na anaishi nyumba mbovu ya kupanga badala ya kununua kiwanja ananunua simu ya bei mbaya cha muhimu anachofanya na hio simu ni kuangalia umbea instagram,facebook na kutuma messages whatsapp; hana lingine lolote na hio simu ilio mcost pesa nyingi sasa huo si ujuha!!! Kingine ulaya watu hawajengi nyumba wewe, nyumba wanazikuta zishajengwa tena na serikali hata wenye pesa zao ni kununua tu. Hata hao matajiri wenye eneo kubwa la ardhi pia, hawaruhusiwi kujijengea tu kwa vile wana pesa lazima wakubaliwe kujenga na serikali hizo ndio taratibu zao. Simu nunua ya bei mbaya lakini iwe at least iwe inakuingizia pesa pia sio show off za samaki samaki huku pa kulala dhofli hal.
hata wewe unaonyesha hujatembea je unamuonaje mtu ana nyumba ya majani kwao na kwake lakini nje amepaki shangingi la milioni60 hali hii iko Tabora na Zambia huyo na wewe nani mjinga.Kama ni nyumba anayo lakini ya majani na ana simu ya bei mbaya the life is choice kilicho akili mwako sio kilicho akilini kwa mwenzio ndio maana mungu akaumba mrefu mfupi mweupe mweusi.
 
Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure
Kiwanja cha nini mimi kwani nataka kuanzisha timu ya mpira?
 
Kwan inauzwa bei gan hyo iPhone mkuu
 
Ni sawa lakini unakuta jitu lipo lipo tu sasa utasema hio ni aki

Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure
Siyo kila mtu anatakiwa amiliki kiwanja, wengine hatuna hata mpango wa kujenga tunatafuta hela kinatumia
 
Back
Top Bottom