Unamiliki iPhone ya macho matatu wakati hata kiwanja huna, wewe ni bure tu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure
 
Daaah, umenikumbusha kuna mzungu mmoja aliwahi tembelea Afrika nafikiri West africa. Basi alivyorudi huku siku moja tukawa tunapiga nae stories vitu alivyoviona huko West Africa. Alinambia waafrica sio maskini kama tunavyojitangaza ila ni akili zetu kidogo zina mushkeli, aliongea kama wewe ulivyosema hapo, huko alikutana na watu wanamiliki simu mbili mbili zote za bei mbaya lakini ukienda makwao maisha wanayoishi ni duni sana kitu ambacho wao wazungu hawafanyi. Na hizo simu mbili unakuta watu wanamiliki kwa show off hamna lolote la maana wanafanya nazo.
 
Daaah, umenikumbusha kuna mzungu mmoja aliwahi tembelea africa nafikiri West africa. basi alivyorudi huku siku moja tukawa tunapiga nae stories vitu alivyoviona huko west africa.Alinambia waafrica sio maskini kama tunavyojitangaza ila ni akili zetu kidogo zina mushkeli, aliongea kama wewe ulivyosema hapo, huko alikutana na watu wanamiliki simu mbili mbili zote za bei mbaya lakini ukienda makwao maisha wanayoishi ni duni sana kitu ambacho wao wazungu hawafanyi. na hizo simu mbili unakuta watu wanamiliki kwa show off hamna lolote la maana wanafanya nazo.

Kila mtu anaishi maisha yake.
 
Unatusagia kuguni ety weeh
Situmewajengea nyumba za kupanga au utazilipia wewe et eeeh
 
Ni vema ukamweleza huyo ndugu yako taratibu.. sio vema kumzodoa kupitia huku jf anaweza asielewe, lakini ukimweleza yeye mwenyewe uso kwa uso atakusikia na atajirekebisha.
 
20210914_163315.jpg

Wewe njoo huku dukani, ukiona mwenye aifoni ya macho matatu ndiyo mimi huyo.
 
Hivi mimi niwaze kununua kiwanja cha nini sasa mkuu wakati dingi yangu ashajenga mijumba kibao hapa town. Hayo si ni matumizi mabaya ya pesa?

Mkuu usipende kupangia watu. Wakati wewe kipaumbele chako ni kununua kiwanja Kisemvule kuna wenzako walishavuka hizo stage zamani sana.

Wakati mwingine anawaza anunue gari ya kifahari Elon Musk anawaza Mars Colonization.

Mkuu hebu google hili somo "hierarchy of needs". Huko utapata kujifunza kitu
 
Back
Top Bottom