Unamiliki gari nchini TZ?

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
481
145
Salaam wakuu,
Magari yamekuwa gharama sana kuwa nayo,lakini ni jambo la kusikitisha, mtu bora akuibie kwa njia nyingine na si kukuibia na kuliharibu gari lako.
Janga hili nimeona niwaeleze,kila mtu afuatilie kivyake.Kumbe ukiwekewa mafuta yaliyochanganya na maji au kitu kingine,gari ikapata tatizo lolote au ika sense na kuzima,uwe na receipt,usiwe nayo-mtu wa kituo cha mafuta kuja kuchukuliwa hatua na mamlaka husika inaweza kuchukua zaidi ya mwezi 1.
Na hapo ni kama una uwezo wa kufuatilia kwa karibu.
Kama una gari lako,bora ukajazia sehemu(kituo) moja na kama ni boss wa huku uswahilini,bora ukanunua mafuta kwa kidumu.
Gari ya huyu ndg -si ya zamani sana ,Landcruiser haina hata miezi 6,imezima na hakuwa na njia, baada ya kuyasikia hayo na aliweka mafuta full tank na maji yanaonekana na ana safari,imebidi ajihudumie ili asafirigharama kama 1.2M
Kama uko mikoani ndio kivumbi.Mpaka uje kupata hizo forms za hizo mamlaka sijui gharama za taxi,muda etc utaupata wapi.
Kuna haja ya kupata watu wa kulitafutia ufumbuzi hili.
 
Hilo nalo neno.
Huu mchezo upo sana tena nchi nzima.
Sijui hata hawa matajiri hizi pesa za dhulma na wizi inakuwaje.
Maana kwanza unamuharibia mtu gari lake,pili unamuibia na kumtia hasara kubwa.
Na kuna Gari nyingine Engine zake zikiingia maji mara mbili ni bora uiuze,maana kuna siku litazingua moja kwa moja.
Hili linajulikana na wafanyakazi wa Vituo vya mafuta wanalijua hili wao na Managers wao.Na ndio maana wafanyakazi wa vituo vingi vya mafuta huwa hawafukuzwi kazi hovyohovyo,maana wanajua siri ya utajiri wa bosi wao.
Hii si kwa vitu vote,vipo vituo ambavyo mafuta yao ni salam na hawachanganyi na maji wala mafuta ya taa
 
Back
Top Bottom