Unamfahamu huyu mpemba mwenye tabia hii?

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Hapo zamani za kale...
Mpemba alirithishwa duka na mzazi wake. Hili duka ni mojawapo ya maduka maarufu kijijini. Kila baada ya muda fulani, familia hii huchagua mmoja wao kusimamia biashara. Utamaduni huu umekuwa ukiendelezwa kwa vizazi vitano sasa. Ni utamaduni wa kistaarabu...

Wakati anakabidhiwa kulikuwa na sukari kg 12, maandazi 50, mchele kg 6, pakiti nane za sigara, maziwa mtindi lita tatu. Viberiti, chumvi, mikate, na vitu vingine vidogo vidogo vikikuwepo. Pamoja na hayo, alielezwa kuwa kuna deni la shilingi elfu 7 wanalodaiwa katika maduka mawili ya jumla.

Pia, alifahamishwa juu ya njia mbalimbali za kuboresha mauzo kama vile kukopesha wateja kwa riba. Zaidi ya hayo, alikabidhiwa wafanyakazi wanne. Mmoja muuza duka, mwingine mbeba bidhaa na kutumwa hapa na pale, mwingine mfanya usafi na ulinzi na wa mwisho mwandalizi wa chakula, na msaidizi ikitokea mmoja wao ni mgojwa. Watumishi hawa walikuwa na sare ambazo walizivaa, lakini kutokana na kuwa na maslahi kidogo, sare zilichakaa na kukosekana kwa ufuatiliaji, kulioelekea wawe wakivaa siku moja moja.

Alipoanza rasmi usimamizi, Mpemba akatazama safu ya watumishi, akaona imezidi, akanuia kuwapunguza. Kwa kuwa hawa watumishi waliajiriwa enzi na enzi tangu anakua, akaona kuwafukuza ghafla itakuwa ngumu. Akawatafutia sababu. Akawasubiri siku moja asubuhi, akawatembelea kwa kushtukiza. Akawaita wote akawaambia mtumishi asiye na sare, kazi imeishia hapo.

Kama vile haitoshi, akasema pamoja na kuwa ni katikati ya mwezi hata mshahara hakuna. Akaendelea kueleza kuwa, walipaswa kuvaa sare siku zote, hivyo kutokuwa na sare kazini inamaanisha wamekiuka masharti. Hakujali uzoefu, wala hakujali utetezi wao. Hapangiwi... Duka amekabidhiwa. Akaendelea kuonesha kuwa waliomtangulia waliharibu tu, na yeye ataleta mabadiliko chanya biasharani. Alikuwa akienda biasharani kila siku kudhihirisha kuwa ni mchapa kazi

Ikaenda, ikaenda....
Hakuna aliyeajiriwa...
Watumishi waliokuwa wameponea chupuchupu ni wawili, mlinzi na muuza duka. Akawaongezea majukumu ya wale wawili walioondolewa. Nao wakidhani kwamba watapata mshahara mnono, kwa kuwa wenzao wameondolea, wakaishia kuisikia nyongeza ndotoni. Hata walipojaribu kuuliza ni lini watafikiriwa, Mpemba aliwajibu waziwazi kwamba kuliko awaongezee mshahara, ni bora atumie hiyo hela kuongeza mtaji. Watumishi wakatishwa, kwamba wakileta ujuaji wataondolewa, kuna watu kibao wanatamani kazi zao.... Wakanywea....

Mpemba aliamua kujiimarisha. Akaajiri watumishi nane wapya, wanne wa kumlinda toka kijiji cha jirani, watatu wa kufuatilia nyendo za wale wasioridhika na maamuzi yake, na mmoja mwandani wake, anayemshauri hili na lile. Kimsingi wazazi na ndugu wa mpemba hawakufurahishwa na mabadiliko yaliyowanyima pumzi watumishi wa dukani. Pili, Mpemba alitaka manunuzi yote afanye yeye, pamoja na kuwepo kwa wenye uwezo wa kufanya hayo.

Siku zilikatika...
Mpemba akanunua baiskeli mbili na mkokoteni mmoja. Hizi zilikuwa baiskeli za kukodishwa kwa wateja wenye uwezo. Fedha aliyoitumia alisema ilitokana na mauzo, ila ukweli ni kwamba alikopa. Alikopa marafiki, akakopa watumishi wake, deni limefika elfu 60. Baadhi ya vitu dukani vimepungua. Ameviongeza: Sukari kg 12 na nusu, mchele kg 8.

Hata hivyo maandazi hayaizwi tena kwa kuwa hana uhusiano mzuri na mpika maandazi. Pakiti za sigara zimebaki 2, maziwa mtindi nayo hayauzwi, badala yake watu washauriwe kunywa maji. Viberiti, chumvi, mikate, na vitu vingine vidogo vidogo vipo kama alivyovikuta.

Ukafika msimu wa mvua. Mvua za mwaka huo zilikuwa zimezidi kiwango cha kawaida. Baadhi ya maeneo yamefunikwa na maji mengi. Duka la mpemba lipo kilimani. Mpemba ana furaha kwamba mafuriko hayamhusu, ila akasahau kuwa dirisha aliloagiza likae wazi lilisababisha maji kuingia dukani.

Madhara ya mvua yalizua hofu. Wanafamilia walitamani kujua mwenendo wa biashara na hasara ya mvua ili wafanye maamuzi iwezekanavyo. Ukawepo utaratibu wa kuandika taarifa na kuiwasilisha jioni kwa wanafamilia. Pia taarifa hii ilihitajika ofisi ya kata. Nako waliunganisha taarifa nyingi ili kuweza kujua namna gani jamii itasaidika. Maeneo yaliyozidiwa, yalipelekewa msaada wa chakula.

Baadhi ya maduka yakafungwa, Mpemba akaona huu ndio wakati wa 'kupiga hela'. Akahimiza watumishi wake kuendelea na kazi. Hakujali hali ya mvua, akidai kuwa mvua zipo miaka yote na kuna wahitaji wa bidhaa hivyo duka lake liwe wazi. Watumishi wakaendelea na kazi. Si amri, kwani kuna mjadala?! Wakavaa makoti ya mvua na mabuti ambayo maji yaliingia ndani...

Miamvuli ilihitajika. Mpemba alikuwa anauza miamvuli, alipoona inakaribia kuisha na hakuna mawasiliano na mtaa wa pili ikakopatikana, akasema miamvuli haina ubora, hivyo wateja na watumishi watumie majani ya mgomba badala ya miamvuli. Wateja watafanyaje? Wapo waliodhani kuwa mpemba atatumia mkokoteni kusambaza huduma kwa wateja. Wakati huo, wateja wa kukodi baiskeli hawakuwepo, hivyo baiskeli zilipigwa na kutu stoo.

Mvua zikaendelea. Watumishi wakajitahidi kumwambia tatizo la dirisha, Mpemba akaweka msimamo kuwa hakuna kufunga dirisha. Anasema wateja wanahitaji kujua duka lipo wazi. Madhara yalipoongezeka, Mpemba akaona kwamba siri itafichuka, kwamba alionywa kuhusu dirisha hakusikia. Hivyo, akawaagiza watumishi wake waandae taarifa ila wasiiweke wazi.

Alitoa sababu, kuwa si lazima ofisi ya Kata ijue mwenendo wake, huenda atahujumiwa. Alisema kwamba wabaya wake wanataka kutumia taarifa vibaya. Haikujulikana kama wanafamilia nao ni sehemu ya wabaya wake au la, kwa kuwa nao hawakupewa taarifa. Kilichishangaza ni Mpemba kualika 'wabaya' wake kuja kujinunulia matumizi kwa kuwa duka lake li wazi. Tena walipewa makaribisho ya hali ya juu kuliko wateja wa kawaida...haikueleweka hawa ni wabaya au walipakwa ubaya kwa sababu fulani...

Kimsingi msimamo wa kuendelea kufungua duka ulimpatia sifa kubwa Mpemba, walimwona kama mtu shupavu sana. Zipo bidhaa zilizoharibika kama madaftari. Baadhi yake yalitupwa nyakati za usiku ili kutokuzua tafrani kwa wanafamilia. Kalamu nazo zilikuwa zinagoma, mbao za shelfu ziliendelea kuoza taratibu. Madhara haya hayakuonekana kwa haraka. Taarifa zilitoka kuwa kila kitu kipo sawa... Wakati haya yote yakiendelea, Mpemba yupo 'hanemuni'....

Bidhaa zilipungua dukani. Baadhi ya wateja waliokuwa wakitegemea kazi mtaa wa pili ili kujikimu walikwama. Madaraja yaliyowaunganisha yalikuwa yamevunjika hivyo hali ikawa mbaya. Vijiji vilitegeana, kila kijiji kilipambana kurejesha hali lakini ilichukua muda. Waliokufa kwa mafuriko waliongezeka.... Wapo waliopona chupuchupu, wapo ambao hawakudhurika kabisa.

Mvua zinaendelea kunyesha....

Muda ukafika wa kupatikana kwa msimamizi wa duka. Mpemba akawa anatamani kuendelea kusimamia duka. Ila hawezi kusema. Ridhaa inatoka kwa wanafamilia, na wale watumishi wake. Wapo wanane walio nyuma yake, aliowapa ugali. Hawa walijipambanua hadharani kuwa Mpemba anastahili kuwa msimamizi wa kudumu. Yeye ndiye msimamizi wa mchakato. Hana wasiwasi... Anajua la kufanya.

Wapenzi wake walitaja mafanikio 'makubwa' ikiwemo ununuzi wa baiskeli na mkokoteni, kuongeka kwa sukari na Mchele. Walipozungumzia hizi bidhaa mbili hawataji 'ongezeko' wanataja bidhaa hizi kama bidhaa mpya. Pia Mpemba mwanzoni alipokabidhiwa kijiti, alianza kugawa pipi bure. Pipi hizo alizikopa kwenye duka la jumla la Mwarabu. Ili upate pipi ya bure lazima upaze sauti mtaani kuwa Mpemba ni msimamizi bora wa duka.

Siku chache zilizopita, Mpemba kampigia mwarabu simu, kwamba anaomba kuunguziwa deni kwa kuwa mvua imeleta maafa. Amefanikiwa katika hilo japokuwa itambidi akope tena ili pipi za bure ziendelee kutolewa dukani kwake. Haya ni mafanikio makubwa ukizingatia watakaodaiwa ni wanafamilia wote.

Wapo wale watumishi wawili wasioridhidhishwa na utendaji wake, hawa ni wale waliobebeshwa mzigo wa kazi. Kwa kuwa walitishwa kuachishwa kazi, baadhi ya watu wachache katika ukoo wao walianza kulalamika. Hawa walinyamazishwa na timu ya Mpemba, timu iliyoamini Mpemba ni MTEULE toka mbinguni, ikizingatiwa kuwa alishajitanabai kuwa anatamani kuwa kiongozi wa timu ya malaika.

Hata mambo yaliyofanywa na timu ya walioajiriwa na Mpemba hayakuhesabiwa kama mambo ya timu, bali ni ya Mpemba. Hakuna aliyepata nafasi ya kuwika.... Wapo waliowika, lakini wiki haikuisha, wakazimishwa kama jenereta lililoisha mafuta.... Sifa zikaelekezwa kwa Mpemba. Kuna wakati walitamani kusema harufu ya kitunguu swaumu imesababishwa na Mpemba...

Nafasi yake kama mwanadamu haikuwepo tena, hakuna aliyedhani Mpemba anakosea, hata ukidhani anakosea huwezi kusema, waliosema 'walinyakuliwa' na pepo mbaya, pepo asiye na jina. Wengine walijikuta pembeni mwa kaburi wakiwa na majeraha na isijulikane wamefikaje hapo...

Kutokana na hali hiyo, wengi hata ndani ya familia walimwogopa Mpemba... Wanafamilia nao wapo mdomo wazi, Mpemba huyu si yule waliyemlea, Kimsingi wanafamilia wanamwogopa, hata wanaotaka kumwonya anawanyamazisha kabla hawajatamka neno la pili. Nguvu yake, ukaidi wake, ukiziwi wake haukuwa na mfano.

Pengine Mpemba si mwanadamu, pengine hakuzaliwa, alitokea tu, akatwaa enzi na utukufu toka kwa wanadamu. Pengine Mpemba ni malaika, pengine ni mteule, ambaye ameshushwa kuwakomesha wale wasiojua neno 'kusifia' au wale wasio na uwezo wa kunyamaza waonapo kosa....

Pengine Mpemba ni kitabu cha kujifunzia... Kila akisomaye anapata funzo fulani... Nani ajua mambo haya?

Pengine, hata mawazo haya ni juhudi kubwa za Mpemba....

Pengine.... Mema na mabaya, yote ni maendeleo.
✍🏼️ Bibi Happy J
 
Sijasoma nikamaliza ila asilimia kubwa kunaukweli, ila kuna mengi ni ya uzushi na sio kweli

ni mtazamo wangu tu lakini kuhusu mpemba huyo
 
We ntoto weye! Kweli familia ilinipa duka lakini nshaliendeleza. Au hujatosheka na maendeleo? Sukari mpaka nlangoni, watoto wenu nshawaajiri. Wataka nini tena?
 
️ Bibi Happy J
Njoo mkuu umalizie hii hadith...
 
Back
Top Bottom