Unamfahamu dereva bodaboda yeyote aliyefariki kwa korona hata ya kusingiziwa?

Je, unamfahamu dereva bodaboda yoyote aliyekufa kwa korona hata ya kusingiziwa?


  • Total voters
    105
  • Poll closed .

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
1. Hakuna "social distancing", wanakaa na abiria wa kila sampuli bila kuzingatia umbali. Wengine wanapakia 'mishikaki'. Wa bajaji kadhalika, wengine hadi kwa dereva wanapakia abiria.

2. Wanashika helementi zinazovaliwa na abiria kadhaa kwa siku.

3. Wanabeba abiria wazima kwa wagonjwa.

4. Wengi hawavai barakoa au wanavaa zile za almradi.

5. Pikipiki ndio ambulensi za kufikia wagonjwa nyumba zisizo na barabara.

LAKINI

Ukilinganisha na makundi mengine katika jamii, madereva wa bodaboda au bajaji huwa salama zaidi unapozungumziwa ugonjwa wa virusi vya korona. Kweli si kweli?

EDIT 1: Matokeo - Wengi hawajasikia mwendesha bodaboda kafa kwa korona hata ya kusingiziwa


Unamfahamu dereva bodaboda yeyote aliyefariki kwa korona hata ya kusingiziwa?
* Ndio (kura 5, 6.2%)
* Hapana (kura 61, 75.3%)
* Sijui (kura 15, 18.5%)

(matokeo ya mpaka tarehe 10 Mei 2020 saa 11 asubuhi EAT).

Wengi wa waliojibu swali hawajaweza kusikia kifo cha bodaboda kinachohisiwa kusababishwa na korona. Hii inaashiria kwamba wanaoendesha bodaboda hawaathiriwi na korona sawa na makundi mengine, licha ya kwamba wao wako kwenye hatari kubwa zaidi ya maambukizi.


Edit 2: Tafsiri ya Matokeo

Waendesha bodaboda hukaa sana juani kusubiri abiria au waendeshapo abiria. Hii inawafanya wapigwe na jua muda mwingi. Hii inawawezesha kupata Vitamin D za kutosha kwenye miili yao. Matokeo yake, wapatapo maambukizi hata hawajitambui kwamba wameambukizwa, au wakijitambua hupata dalili ndogo na hawahitaji kwenda ICU au kudondoka ghafla na kufariki. Hii ni hata kwa bodaboda watu wenye umri mkubwa, wenye magonjwa menginewe, na vihatarishi vingine. Waendesha bajaji hali kadhalika.



Edit 3: Maelezo ya Kisayansi


















SOURCE: Viral video


Edit 4: Yatokanayo

1. Kwa wale wakaao ofisini au kwenye magari kwa muda mrefu wakae juani walau kwa dakika ishirini hasa asubuhi ili kuweza kupata sehemu kubwa ya mahitaji yao ya Vitamin D.

2. Kupata viongeza Vitamin D vya lishe au vya moja kwa moja.

3. Swali hili limeuliza kuhusu dereva bodaboda. Lingeweza pia kuuliza makundi mengine kama wavuvi wakaao juani na walao samaki; maaskari-trafiki washindao juani barabarani; na makundi mengine ya watu walio na uwezekano kuwa na viwango vikubwa sahihi vya Vitamin D.

4. Makundi yafungiwayo ndani kama vile wafungwa, mahabusu na watu wengine wasiopigwa na jua mara kwa mara, wanatakiwa kufunguliwa kwa muda wa kutosha kila siku ili kuwaongezea kinga.

5. Maamuzi ya kimkakati na ya kisera.
 
Tetesi ikiwa kweli, ina maana licha ya wa bodaboda ndio walio katika hatari kubwa, lakini ndio kundi salama zaidi mpaka sasa.
 
Watu wanakufa sana, hakuna mahali ugonjwa ambako haujafika.

Hao wanaotangazwa ni kwa sababu wana watu wa kuwatangaza.
 
You have a point..

Corona inaua kuanzia miaka 45 au awe na magonjwa
Na watu ambao sio active ..
Sio bodaboda Tu hata mafundi ujenzi umri below 40 si rahisi kusikia..

Boda Boda wengi Wana Corona na hawajijui
Ni carriers..wanasambaza..sio rahisi kuugua wao
 
Ongeongezea hapo na kipengele cha sijui, maana kuna wengine hawako hapana wala hawako ndio
 
You have a point..

Corona inaua kuanzia miaka 45 au awe na magonjwa
Na watu ambao sio active ..

Sio bodaboda Tu hata mafundi ujenzi umri below 40 si rahisi kusikia..

Boda Boda wengi Wana Corona na hawajijui
Ni carriers..wanasambaza..sio rahisi kuugua wao
 
You have a point..

Corona inaua kuanzia miaka 45 au awe na magonjwa
Na watu ambao sio active ..
Sio bodaboda Tu hata mafundi ujenzi umri below 40 si rahisi kusikia..

Boda Boda wengi Wana Corona na hawajijui
Ni carriers..wanasambaza..sio rahisi kuugua wao

Asante. Nataka tu kufahamu kama mtu ameshawahi kusikia dereva fulani wa bodaboda kafa kwa korona.
 
Back
Top Bottom