Unam-treat FAIRLY house girl wako?

I just don't believe in house maids.

Wewe wakati unakuwa hukutunzwa na housemaids? Njoo bongo, ambapo hata kama una most of the home appliances umeme still ni issue, tuone kama utachota mkaa na vidole na kuanza kuwasha ili uchemshe tu left overs; tuone kama utafua nguo na malinen au mablanket.

Watu wengi walioko huko mamtoni, si kwamba hawapendi ni kuwa majority can not afford Househelps. I understand you guys, so try to also to understand people who have the househelps, the important thing is fair treatment as the thread suggests.
 
Nampenda h/g wangu kwani ndio anabaki na mwanangu nikienda kazini, aliomba kuongezewa mshahara mwanzoni mwa mwaka huu, nikampa kiasi anachotaka. Mshahara huwa nampa pale anapohitaji manake anaogopa kukaa nao mwenyewe kwa hofu ya kumissuse, itabidi nikopi hapo pa kumfungulia account hata km ni ya mpesa. Nakula naye meza moja,likizo, yeye mwenyewe hataki kwenda kwao. Nafikiria mtoto akikuwa nimpeleke shule, nimemuuliza amesema anapenda kuwa fundi nguo. Kuna kipindi anafanya kazi vizuri sana mpaka nafikiria kumfanyia mema zaidi ila kuna muda ananiboaaaa, ataamka saa mbili mpk nimuamshe, nikirudi jioni saa moja kila kitu ovyo, nyumba chafu, vyombo chafu, mtoto hajala, chakula hakijapikwa. Anapenda sana tv kila saa anafuatilia vipindi vyote na marudio yake, afu nje kwa majirani ndio usiseme alhamis wamempa mtoto kachori huko kwa majarani mtoto anaharisha mpk leo. Nishaurini jinsi ya kumuelewesha huyu binti kwani nampenda na mtoto kamzoea sana, natamani aelewe namuwazia nini ili tukae vizuri zaidi.
 
Hebu tujadili hili wana MMU,
House girl ni mtu muhimu sana katika nyumba.

Umuhimu wake ni pamoja na:
-Kukusaidia/kukufanyia kazi za nyumbani.

-Kukulindia nyumba pindi unapokuwa kazini.

-Kuhudumia watoto/familia yako hata/hasa pale ambapo haupo nyumbani........na mengine mengi mengi yasiyo idadi.

Kwa hiyo tunakubaliana kuwa huyu ni mtu muhimu sana kwako na kwa familia yako.

Sasa swali linakuja:
Hivi housegirl wako unampa treatment zinazostahili kweli?

-Unakula naye meza moja na chakula kimoja kama unachokula wewe, au ndo vile tena wewe na familia yako mnakula mapochopocho hapo dining room wakati yeye mnamfutika huko stoo akila makombo?

-Analala mahali panapostahili, au ndo kumweka sebuleni mbu wakimmaliza.

Umempa mkataba wa uhakika kwa mujibu wa sheria za kazi?
-Unamlipa mshahara unaostahili na kumwekea akiba ya uzeeni?
-Unampa bima ya afya na matibabu ya kiutu?
-Unampa likizo ya siku 28 kila mwaka?

-Unampatia elimu stahiki? Kumbuka wengi wameingia kwenye kazi hiyo kwa sababu hawakupata fursa ya kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali nyingi zikiwa za kiuchumi, lakini si kwamba hawana uwezo kiakili. Au unamtumia tu kama toiletipepa?

-Humpi manyanyaso ya kumfokeafokea bila sababu maalum?

-Unampa mapumziko yanayostahili au ndo vile akiamka saa kumi analala saa saba.

-Unaporudi kazini anakufurahia kama baba/mama au ndo anakereka kwa kujua muda wa kukaa kwa hofu umefika sasa.

-Unamsaidia kazi pale panapostahili?

-Mara moja moja unamnunulia japo mavazi na kumfanya kama mmoja wa familia yako? Au ndo vile tena gauni refu hadi linaburuza chini, kila siku hilo hilo....

Hebu tujadili haya kwanza.

Mh!
Liuzi lirefu alafu linacho sha?
Siku nyingine jitahidi kufupisha!!
LOOH!
ubongo wa mwananchi ni silaha hatari sana!
 
jana asubuhi nilipoamka tu nilimwambia hse gal abandike makande jikoni. Napenda hiki chakula sana. vile kinachelewa kuiva ni vyema kubandika mapema. nimefanya shughuli zangu za usafi, nimetoka kwenda kwenye mihangaiko yangu ya jumamosi, nikijua hsegal atashunghulikia makande. huko nilikoenda sikutia chochote mdomoni, maana nina hamu ya makande nisije nikaharibu appetite. nimerudi kwenye saa tisa mchana. Hamuwezi kuamini there was no makande. namuuliza huyo hse gal mnayesema tu treat vzuri, kwanini hajapika, jibu lake ni kwamba hakupika maana YEYE hapendi makande!!!!! naomba msiniulize nilichukua hatua gani, ila ingekua wewe ungefanyaje? huu ni mwezi wa 6 niko na huyu binti asopenda makande.

mimi hg wangu ana muda miezi miwili sasa juzi kanitolea kali, nimemuuliza mbona hujafagia nje kaniambia sio yeye aliyechafua! na kali zaidi nikamwambia afue foronya za mito ya kwenye sofa pia akasema sio yeye aliyechafua. I magine hayo majibu and she is taking care of my 2 year old daughter na wanashinda pekeyao nyumbani. niliondoka nikajiendea kazini nikamuacha , jioni nimerudi nikaloweka foronya zangu ili niziamkie saa 12 asubui.
 
mm kuna scenario moja iliniumiza sana,mama kaja naye kwenye gari ilikuwa usiku saa moja na nusu hv,akamtoa nje ya gari akamuacha nje ya mlango,akaingia supermarket kwa masaa mawili yule binti yupo nje anang'atwa na mbu mpk huruma jaman i felt so embarassed,sasa nikawa nawaza ameona garama gani kumuacha kwenye gari akasubir?na kama pale ni hvyo huko nyumbani huyo binti ana maisha gani?too bad,wanawake tuwe na utu na upendo plz
 
mimi hg wangu ana muda miezi miwili sasa juzi kanitolea kali, nimemuuliza mbona hujafagia nje kaniambia sio yeye aliyechafua! na kali zaidi nikamwambia afue foronya za mito ya kwenye sofa pia akasema sio yeye aliyechafua. I magine hayo majibu and she is taking care of my 2 year old daughter na wanashinda pekeyao nyumbani. niliondoka nikajiendea kazini nikamuacha , jioni nimerudi nikaloweka foronya zangu ili niziamkie saa 12 asubui.

pole sana...tafuta mwingine kimya kimya, ukimpata mtimue...la sivyo anaweza fikia stage ya muacha mtoto na njaa ukimuuliza atakwambia sio yeye aliyemzaa:(
 
mimi sina house girl na nawaonea gere saaaana mlionao...asikudanganye mtu, maisha ya bila house girl si rahisi...hasa kwa wanaofanya kazi na wenye watoto kama mimi...

ila nimeona house girl wa ndugu yangu ambaye nadhani ana pata tretment nzuri sana...anapewa laki na nusu/mwezi, amepanga chumba chake mwenyewe, anafanya kazi saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni then anarudi kwake...ni muislam so, Ijumaa anafanya kazi nusu siku japo mwajiri wake si muislam, Jumapili anapumzika kabisa, likizo mara moja kwa mwaka, malipo ya uzeeni...sidhani.
 
Mimi nilkuwa naye nikawa namlipa 50,000 kwa mwezi kula kulala na mengine yote kasoro sex kwangu, lakini wapi bwana. Ndege wengine hawafugiki kwa kweli.

Ni kweli wengine hawafugiki! uta-mtreat fair kabisa lakini visa haviishi, na kwa wale tunaoishi nyumba za kupanga... majirani nao ndo huwatolea macho, akiona mdada unaishi naye vizuri anamrubuni na kumchukua.

Halafu cha kushangaza utakuta wale wanaopata manyanyaso katika familia wanazofanyakazi ndio wanadumu muda mrefu, tofauti na pale wanapokuwa treated kama sehemu ya familia. Nimeshuhudia case kadhaa za aina hii.
Ifike mahali sasa waajiri wawathamini hawa watu lakini na wao wajitambue na kuidhamini kazi yao kama ilivyo kwa kazi nyingine yoyote, kwani wao ni muhimu sana!
 
hawa watu(mahg) wanakutana na changamoto au matatizo mengi,kuna case moja niliishuhudia miezi kadhaa iliyopita..nilikuwa kwenye hotel moja ivi maeneo flani,nilikuwa napata lunch,pembeni yangu kulikuwa na familia moja yenye asili ya kiasia walikuwa wanapata lunch na wenyewe,walikuwa na mdada ambaye ana asili ya kibantu,alikuwa kampakata mtoto wa kama miaka 2-4 ivi mtoto mwenyewe naye alikuwa na asili ya kiasia,kilicho nikera ni wale member wa ile familia kuconcentrate na kula,kunywa na stori huku waki muignore yule binti kabisa kama hawakuwa naye vile na mbaya zaidi alikuwa anasumbuliwa mno na yule mtoto aliyekuwa amemshika na hakupata msaada wowote kutoka kwa member wa ile familia kumbembeleza na yale mamisosi yote walikuwa wamejirundikia wao tu yule binti akawa na bite2 tu anatafuna na ukiangalia nguo zake alizovaa mmh ilikuwa ni aibu kwa mazingira yale,ilinikera mno nikareflect enzi zile za utumwa ndo nikachoka kabisa kuendelea kuwepo maeneo yale iliniuma sana kiukweli walichokuwa wanamfanyia yule mdada.

Tatizo la wadada wa aina hii, kufanya kazi kwa mbantu hawataki, na hata hapo walipo hawaondoki ng'ooo. Anaweza kukaa nao hata zaidi ya miaka 10!
 
Nampenda h/g wangu kwani ndio anabaki na mwanangu nikienda kazini, aliomba kuongezewa mshahara mwanzoni mwa mwaka huu, nikampa kiasi anachotaka. Mshahara huwa nampa pale anapohitaji manake anaogopa kukaa nao mwenyewe kwa hofu ya kumissuse, itabidi nikopi hapo pa kumfungulia account hata km ni ya mpesa. Nakula naye meza moja,likizo, yeye mwenyewe hataki kwenda kwao. Nafikiria mtoto akikuwa nimpeleke shule, nimemuuliza amesema anapenda kuwa fundi nguo. Kuna kipindi anafanya kazi vizuri sana mpaka nafikiria kumfanyia mema zaidi ila kuna muda ananiboaaaa, ataamka saa mbili mpk nimuamshe, nikirudi jioni saa moja kila kitu ovyo, nyumba chafu, vyombo chafu, mtoto hajala, chakula hakijapikwa. Anapenda sana tv kila saa anafuatilia vipindi vyote na marudio yake, afu nje kwa majirani ndio usiseme alhamis wamempa mtoto kachori huko kwa majarani mtoto anaharisha mpk leo. Nishaurini jinsi ya kumuelewesha huyu binti kwani nampenda na mtoto kamzoea sana, natamani aelewe namuwazia nini ili tukae vizuri zaidi.

Labda uwe unamuachia list ya vitu vya kufanya, ila kama ni mbovu sana wa TV hapo shughuli ipo. Mie mwenyewe wa kwangu ndio ambao huwa wananitumia ujumbe kuwa DSTv imekata!
 
asante kwa kulileta hili hapa,nina ndugu yangu mmoja ivi ana tabia ya kumnyanyasa msaidizi wake wa kazi kila saa anamgombeza na kumpiga makwenzi na vibao bila hata sababu ya msingi,mara ampimie chakula,asiingie sebuleni yaan vitu vya ajabu ajabu tu na ukimuuliza kwanini anamfanyia ivo mtoto wa watu ana msemo wake "fuata yaliyo kuleta".afu anamlipa mshahara elfu kumi wakati anafanya kazi nyingi kweli.Jamani hii sio tabia nzuri kabisa sijui wanawake wengine wakoje?
Huyu hana tofauti na ndungu yangu mie, anadai house girl wake anamkumbusha maisha aliyoishi kwao..lkn for hard working ameweza kuyaepuka .. kwa hiyo housegirl wake ni mzembe kuishi maisha hayo..na hawezi kumheshimu
 
Duh! mengine hatuyafanyi tuseme ukweli, kama ili la kumwekea akiba ya uzeeni......ila ni muhimu kumtendea haki house girl wako.
 
huwa siwaelewi wanataka nini siku hizi ni wa kubahatisha kama bahati nasibu akikaa miezi sita unashukuru.
 
Ni kweli hayo unayoyasema kuna baadhi ya watu huwanyanyasa sana wafanyakazi wao,lkn je umejaribu kuangalia upande mwengine wa shilingi?maana visa vyao vinaweza vikakutia pressure..
 
Ndo kwanza naanza maisha hata huyop house girl simjui samahani lakini!:disapointed:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom