Unalipwa mshahara kwa wewe kuripoti kazini asubuhi na kurudi nuymbani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unalipwa mshahara kwa wewe kuripoti kazini asubuhi na kurudi nuymbani!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Esther Kimario, Jan 22, 2012.

 1. E

  Esther Kimario Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wengi tunatafuta kazi, lakini ni muhimu kujua kama kweli tunazihitaji kazi hizo, vinginevyo kazi hizo zitageuka KUWA LAANA kwetu! Nina ndugu yangu ambaye alikaa muda mrefu bila kazi, mwisho alichakachua cheti cha form four na kupata kazi ya jeshi. Cha kushangaza alipopata tuu akatafuta cheti kingine cha kufoji kinachoonesha ni mgonjwa! Kwa miaka zaidi ya mitano anakwenda kuripoti tuu kazini na kurudi nyumbani!! Na anajisifia sana kwa hili... Mimi nasema HII NI LAANA na mtu kama huyu hapaswi kuwa na kazi!!!!! KABISA!! Najisikia vibaya kuwa mimi nakatwa hela mwisho wa mwezi (PAYE na makato mengine kibao) kumlipa mshahara mzembe kama huyu!!!!!

  Serikali nayo iamke bana!! utamlipaje mtu kwa miaka mitano mshahara kwa yeye kufika na kuripoti kazini na kurudi??:argue:

  Jamani naombeni tukipata kazi tuwatendee haki wenzetu na tuitendee haki nchi yetu!!!!!
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mbona hao wawakilish wanalala bungeni na wanalipwa
  mkubwa akijinyea,mtoto akijamba asiadhbiwe,HUU NI MFUMO
   
 3. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ndo tulivyo shemeji yangu Esther, hii nchi hamna mwenye uchungu nayo. Huskii wengine wanasema ni shamba la bibi kila mtu anachuma? na wewe kama kuna uwezekano chuma tu
   
 4. E

  Esther Kimario Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shem tukifanya hivyo tutaishia wapi??? I dont think tutaitendea haki nchi hii tukiacha kupambana na tabia chafu kama hizi!...
   
 5. E

  Esther Kimario Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri tunakila sababu ya kuendeleza mapambano dhidi ya wakubwa wanaojinyea na watoto wenye kujamba hovyo makusudi (Sijui kama mf. ni sahihi sana) ... Maana kama hatutawadhibiti mapema kesho wakiwa wakubwa wote watavaa pampas! Wote taifa la wenye kujinyea?? Hapana... tuna kila sababu ya kukataa hili!
   
 6. M

  Mamatau Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unaeyajua haya kwa nini hutoi taarifa kwa wahusika wachukue hatua stahiki? Au alikuwa anakupa mgao na sasa mmeshindwana ndio unaleta umbea wako hapa?
   
 7. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  hao ndo wanaoharibu nchi.mtu umechakachua cheti ukapata kazi badala ya kuwa mwaminifu na mfanyakazi mwenye bidii wewe una kuwa mzembe.
   
 8. E

  Esther Kimario Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mamatau, unakifahamu chombo husika kupeleka taarifa hizi? (Nasikitika tone uliyotumia si nzuri) but mchango wako ni muhimu! Sitaki kudhani kuwa unahalalisha tabia kama hizi.
   
 9. E

  Esther Kimario Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usemayo ni kweli Dr. lkn bahati mbaya sana watu waliofoji mara nyingi hata uwezo wao wa ku-reason huwa ni mdogo! Hivi ni chombo gani hasa kinashughulikia issues kama hizi?
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Hufuti dhambi kwa kufanya dhambi.
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Hizi ni athari za siasa za "ujamaa na kujitegemea" zilizobaki kwenye jamii. Watu wamekuwa wanauona uozo wanauwachia kwa sababu tu anchokitumikia ni cha wote (umma). Mambo kama hayo kwenye mashirika ya binafsi ni kidogo sana.

  Nakumbuka mfanyakazi aliyeajiriwa kutoka wizarani kwenye kampni binafsi, alikuwa na tabia ya kuripoti kazini mapema lakini ikifika saa 3 humuoni, anarudi baada ya masaa mawili, akiulizwa anasema alikwenda kupata "breakfast"! khaa, unatoka nyumbani kwako hujanywa chai? unatumia muda wa kazi kwenda kupata "breakfast", akapewa verbal warning hakuijali, haikufika muda akatimuliwa kazi.

  Jee, tasisi za Serikali na mashirika ya umma wanayaweza hayo?
   
 12. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  uvivu uliopitiliza kiwango
   
 13. E

  Esther Kimario Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana na wewe kwa sehemu Faiza, Lkn pia ni muhimu kujua kuwa misingi ya ujamaa ilikuwa ni pamoja na kufanya kazi na kuondoa matabaka... ujamaa ulikuwa na lengo la wote tufanye kazi na pia kuyabana makupe yanayoishi kwa jasho la watu... mtu wa namna hii ni kupe! Hafanyi kazi yoyote na bado ana uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi!!!! Ujamaa ulipinga matabaka (Tabaka la wafanyaji kazi na tabaka linaloneemeka na jasho la wafanyaji kazi) .... Im sure jasho letu ndilo linalowabeba kndi la watu wa aina hii!
   
 14. E

  Esther Kimario Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As you are saying ni zaidi ya uvivu! Ni wizi na unyonyaji! Ni kukosa maadili na kutokuthamini wenzako... na ukingalia kwa undani ni kutokuthamini ulichonacho mwenyewe pia...
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Badala yake ukazaa si makupe tu, ma ndondocha, misukule na ma vampire. Hizo ndio athari zake. Theory inaweza kuwa nzuri sana kwenye makaratasi na kuielezea na kuitetea inategemea na uhodari wako wa kusema, lakini ikifikia kwenye vitendo hapo wasemaji huwa hawana cha kufanya na action speaks louder than words.
   
 16. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  EPA,RICHMOND,MEREMETA,DOWANS nk wamewakatisha tamaa raia jamani,dawa ya moto ni moto
   
 17. E

  Esther Kimario Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imefika wakati tuwachukulie hatua wote mnaotuibia kwa kisingizio ati "mbona epa na richmond" ...! Ni fikra duni kujustify uovu eti kwa sababu kuna waovu kwenye jamii yako!
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Esther Kimario,

  Kutokuchangiwa sana kwa hii mada inaonesha ni jinsi ilivyowagusa wengi.

  JF hushamiri wakati wa kazi na wachangiaji wengi humu hutumia muda wao wa kazi kujazana humu, hizo kazi wanafanya saa ngapi?

  Halafu wanalia mafao madogo.
   
 19. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Una changia mada au una ugomvi binafsi na mtoa mada? Mimi ningekuona una busara kama ungemwelekeza wapi kwa kwenda na kuliripoti hilo na sio kumshushia tuhuma ambazo ni sehemu ya hisia zako. Sidhani kama anafanya umbea, mimi kwa maoni yangu ni kwamba ametoa nasaha
   
 20. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono na mguu pia. Na ndio sisi sisi tunaohodhi nafasi za IT kwenye mabenki, tukipita kwa madaha kwenye makorido huku tunaning'iniza flash disks kwenye mifuko ya mashati ilhali websites za mabenki husika zipo under construction for 2yrs. Kazi zetu kubwa ni kucheza karata, kuvaa mashati mazuri kama waimba kwaya na kusubiri lunch time tuwahi steers kula sambusa moja na juice kama mademu.

  Vijitu vya namna hii havichelewi kujiita intellectuals mbele za watu
   
Loading...