Unakumbuka Ugomvi wa Tambaza na Azania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unakumbuka Ugomvi wa Tambaza na Azania?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by mtu chake, Aug 8, 2011.

 1. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kipindi niko Primary nilikua nasikia Ugomvi kati ya Azania na Tambaza..miaka ya 90"s....bahati nzuri au mbaya..nami nikachaguliwa..kusoma pale Azania..sasa..kulikuwa na ile michezo ya Don Bosco Pale Upanga...ukatokea Ugomvi Kati ya azania na Jitegemee..hakika sisahu..huu Ugomvi..maana ulikuwa mkubwa kiasi F.F.U wakaja kutawanya wanafunzi ugomvi ulikuwa mkubwa sana..na uliendelea kama Wiki hv mpaka serikali zote mbili za wanafunzi zilipokutana na kusuluhishwa

  Tena miaka hiyo hii tabia ya wanafunzi kupigana mashuleni ilikuwepo sana...
  Mfano:...Tambaza na Azania...kisa sikumbuki..ila Tambaza waliwahi kuja mpaka shuleni kwetu Azania..mapambo yalikuwa makali
  Azania na Jitegemee pale Don Bosco
  Azania na Pugu..ilikuwa mashindano ya Umiseta kule Pugu
  Kinondoni Muslim na Makongo sec..kule mwenge mashindano ya Umiseta
  Nakumbuka Ugomvi wa kwanza Azania na Tambaza kuna watu walikufa...na pia kuna jamaa aliua Kondakta kwa mwavuli ..naye alijiua..
  ikapelekea wanafunzi wengi wa Tambaza kuhamishwa mashule ya mikoani

  NAULIZA TU:mbona siku hizi hkuna mambo hayo?.....
  tatizo lilikuwa nini?
  Je wewe uliwahi kushiriki ugomvi wowote mashuleni wakati unasoma?
  Vipi mikoani nako wanafunzi walikuwa wanapigana shule kwa shule?
   
 2. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  rejea watemi wa miaka hiyo...tambaza marehemu puzzo pale kinondoni muslim a.k.a kibwelu kuna mshkaji alikuwa anajiita chaduma sighn cyborg!!!!!siku hizi hamna mambwiga watu wanaangalia kushine kimaisha utemi michongo ya kishamba!
   
 3. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Kaka yule sio Puzzo ni Puzza.
  Alijiua kwa kunywa Sumu.
  Baada ya yeye ikabidi nichaguliwe haraka kuwa kamanda mkuu wa kikosi cha kujihami cha wanafunzi wa Tambaza ambacho nilikiongoza kwa mafanikio makubwa.
  Hapo ndipo utumiaji wa mabomu ya mafuta taa ulipoanza.
   
 4. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Imenikumbusha mbali sana, kuna jamaa alihamishiwa shuleni kwetu Lugalo Iringa akitokea tambaza kwa ajili hiyo.
   
 5. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ugomvi huo nakumbuka nilikuwa na dogos o'level 93 au 94 nadhani ndio moto uliwaka na wakaamua wafute o'level ya Tambaza Second School iliyokuwa ya wavulana tu kwa kuwaamisha wote kwenda shule tofauti ilikuwa kuwagawanya wasiwe pamoja tena maana walishindikana

  Na hapo ndipo serikali ikaamua kuanzisha A'level ya girls and boys. Kabla yake kulikuwa na A'level ya boys PCM na PCB tu. Ila kulikuwa na wasichana wachache madarasa hayo yaani kati ya let's say 2-10 ilitegemea.

  Naikumbuka vizuri sababu dogo's ilibidi watinge safari ya mikoani hapo baada ya kutokuwa na walimu ambao waliamishiwa shule zingine pia.

  Oya nafurahi waliendelea salama na kufaulu then wakakitoa haoooooooo
   
 6. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Kaka yule sio Puzzo ni Puzza.
  Alijiua kwa kunywa Sumu.
  Baada ya yeye ikabidi nichaguliwe haraka kuwa kamanda mkuu wa kikosi cha kujihami cha wanafunzi wa Tambaza ambacho nilikiongoza kwa mafanikio makubwa.
  Hapo ndipo utumiaji wa mabomu ya mafuta taa ulipoanza.​

  • ..hahahahahahahaha...nakumbuka mkuu hapo kwenye red,mlikuja kupiga bomu shuleni kwetu Azania kwenye maabara ya kemia karibu na nguzo ya umeme..mkitokea Muhimbili hospital...dah..Enzi zile cjui ingekuwa sasa ingekuaje ?
   
 7. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  kweli mkuu ni puzza unajua jina limenichanganya na tozi mmoja wa forest hill miaka hiyo!aminia gang chomba kwa wadhifa huo kwa miaka ile kwani tambaza ilikuwa ni zaidi ya taliban!.....kabla hajajiua inasemakana alifanya sana usafi home!puzza kwakweli alikuwa kamanda tosha!kama kupinda yeye alikuwa amenyongorota kabisa!
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  kwanini alijiua
   
 9. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Je Unaikumba AZAJANGWA NA TAMBAZANA?Miaka ya 1989..1991?
   
 10. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  kifo chake kimebaki kitendawili kwani hakuacha barua yeyote alichowashangaza watu wa familia yake ni ule usafi na walivyomuuliza alisema kuna wageni watakuja!wanafamilia wakaondoka kurudi wakamkuta kamanda puzza keshajiua!inasikitisha sana kukumbuka tukio hili
   
 11. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 613
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  kamanda unamkumbuka sele muhdini aliyekuwa mpinzani mkubwa wa marehemu puzza pale tambaza?
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hebu anzisheni vurugu humu mjikumbushe kivitendo.
   
Loading...