Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Nikiwa mdogo miaka ya 90 kuna jirani alikua na volkswagen bettle siku moja amefika anaingia apaki nikakidandia kwa uku kwenye mlango huwa kuna ile sehem ya kanyaga ghala nikateleza nikaanguka miguu ikaingia chin ya gari likanipanda nikasikia makelele watu huko nashukuru Mungu hata haikuvunjika.
Miaka ya 2008 au 09 nikiwa shule A level shule moja Dar niliumwa malaria week 2 nakunywa panadol tu sijui nilikua na mawazo gani siendi hospital ilifika hatua sasa hali ikawa mbaya zaidi nilikua najikaza niende kula ghafla nikaona nguvu zote zimeisha nikaona giza macho yakafumba yenyewe kulikua na mwanafunz mwenzangu ndo alinidaka nikakumbuka kumwomba Mungu nikataja tu Yesu nisaidie alivyonitua chini kunilaza ghafla nilipata nguvu ambazo kubwa nikajikuta nataka nipelekwe hospital bahat nzuri wakaniwahisha
 
Well;
Nakumbuka ilikua 2008 imebaki wiki moja tu mtihani Wa kumaliza darasa la saba (7) ufanyike (nami nilikua miongoni mwa darasa la saba), basi bhana so unajua wiki hip ya mwisho wanafunzi masomo yanakua hakuna ni kujiandaa tu na mitihani.

Tukajikusanya washkaji kama 7 hivii tukapanga twende tukaogeree; nadhan mnaelewa Barabara ya Lami ikiwa inatengenezwa hua kuna mahala pembezoni wanachimba mchanga au kokoto( hua wanaita KARASHA); sasa mvua ikapiga hivyo maji yakajaaaa balaaa.

Tuendelee sasaaa;
Tukafika hapo mzee crew yetu tukaanza mashambulizi ya kuogelea hhaa Mimi hapo sifahamu kuogelea basi nacheza n pembezoni tu mwa vifusi sijui nini kikaniambia nenda nenda katikati hahahaa kufika kati nikazidiwa aisee nikaanza kupiga Lita zangu napnda juu nashuka chini huku napiga kelelee (hapo wenzangu wako mbali ma wanajua naelewa kuogelea) nikaaanza kuona mwisho w maisha ushafika hapo haha nikaanza kupiga kelele kila nikiibuka juu ya maji, kumbuka maji yanatabia yanakupeleka sehemu yenye kina kirefuu, sijui nilipata wapi ujasiri na mawazo, basi nikasema nikipanda juu navuta pumzi nikishuka chinii nizame mpaka chini then nianze kama kutembea kuelekea kule kwenye kifusi yaani mwisho Wa maji nikafanya hivo nikawezaaa hahaaa nilipotoka hapo nikakaa pembeni;
Kuanzia hapo Mimi na kuogelea ni panya na paka (hua nakumbuka sana mistari ya Mh. Temba; usiguse maji kama hujui kuogelea),

Hua nawaza sana ningekata moto pale ndo mitihani ningeukosaa hahahahaha, nafurahi nilifanya mitihani na nikafaulu vemaa hahaa...
 
Asubuhi saa 12 naamka na wenge nikimbie shule.. naenda kushika kitasa ili nifungue nakuta black mamba kajizinga pale kwenye kitasa ananikodolea macho..
Yaani umbali wa nyoka na mkono wangu kama inch 5 tu.
Nilishtuka sana..hua siui mdudu yoyote baada ya mbu so niliamsha wengine waje wamtoe nikawaambia wamfukuze nje. Bahati mbaya wale binaadamu walimuua yule nyoka
LOL pole sana,hakuna urafiki kati ya nyoka na mwanadamu,hasa blackmamba,waliomuua walifanya sahihi,pole leo hii tusingekua tunapata nondo zako walahi
 
Mmmh.. .

Nilikaa I.c.u..mda sana tu..

Lakini ajabu..nilikuwa pembeni ya mwili wangu ulipolala...natoka na kuingia wodini...naona ndugu na madoctor...tatizo nilikuwa siwezi kushika mtu au kitu wala kuongea na nikitembea nilikuwa sikanyagi ardhi!

Nikajiuliza sana sana...kwa nini iwe hivi? jibu sikupata!

Kwa ufupi...nilirudi .. katika hali ya kushangaza mno.
Lakini ndugu zangu ... huu ulimwengu
una mapana!



Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana ndugu.
 
Mwaka 98 maeneo ya mazizini unguja kituo cha polisi ilikua kuna gari 2.8 inatoka airpot imekolea kama spidi 80 mimi nina vespa nilimpakia kaka yangu niliingia katikati ya gari ikatupiga mzinga mkubwa sana ikatuburuza kama mita20 sikujua dereva alisimama kwa kutumia nini.ulikua ni uokovu wa Mungu tu kutoka wazima tulichunika na mimi nikapasua sped meter kwa kichwa.

Nikiwa na miaka 13 nilianguka kwenye mti mrefu kuanzia juu mpaka chini nikagongana na matawi mpaka nikafika chini kabisa. Nilijifuta mavumbi tu.
 
Mwaka 98 maeneo ya mazizini unguja kituo cha polisi ilikua kuna gari 2.8 inatoka airpot imekolea kama spidi 80 mimi nina vespa nilimpakia kaka yangu niliingia katikati ya gari ikatupiga mzinga mkubwa sana ikatuburuza kama mita20 sikujua dereva alisimama kwa kutumia nini.ulikua ni uokovu wa Mungu tu kutoka wazima tulichunika na mimi nikapasua sped meter kwa kichwa.

Nikiwa na miaka 13 nilianguka kwenye mti mrefu kuanzia juu mpaka chini nikagongana na matawi mpaka nikafika chini kabisa. Nilijifuta mavumbi tu.
Lol pole Sana Mkuu,Mwache Mungu aitwe Mungu.
 
Miaka ile ndo niko likizo ya mwezi wa sita nikiwa F.1, nilikuwa nimelala chumbani kwangu nyumbani kijijini na najisomea huku nimelala chali na kibatali karibu na kichwa. Sikuwa na usingizi kabisa lakini sijui kilichonikuta!

Nilikuja kupata fahamu niko gizani. Nilipowasha kiberiti nilikuta kitabu kiko chini, kibatari kiko chali sakafuni na mafuta yote yamemwagika.

Nadhani nilipoteza fahamu baada ya kuvuta moshi wa kibatari kwa muda mrefu na kama kibatari kingebinukia kitandani na moto usizimike, na mimi wakati huo sina fahamu, leo nisingekuwepo hapa kusimulia kilichotokea.

Kwa hilo, niliuona mkono wa MUNGU akiniepusha na janga la kuteketea kwa moto ukizingatia nilikuwa peke yangu kwenye nyumba siku hiyo!

Mungu ni mwema daima!!!
 
lee van cliff, Huyo hakuwa Koboko.... (Black Mamba). Manake huyu hana simile .. haujamchokoza lakini anakutoa nduki.

Mimi siamini kwenye "God intervention" kila jambo linafuata misingi na kanuni za asili... hapo ilikuwa nyoka akugonge au akuache, au wewe umuue. Hakuna cha ajabu hapo (hakuna kanuni iliyovunjwa).

Nyoka kuingia ndani kwako inawezekana, nyoka kukudhuru au kutokukudhuru inawezekana pia.

Jiulize hivi angekugonga je, ungesema nini kuhusu Mungu (virse versa ??)

Sent using Jamii Forums mobile app
Black mamba ni mpole sana tena sana, ila uisilmbe aliamshe!!!.
unaweza kaa karibu na black mamba, na asikufanye chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana usiku tarehe 13/01/2020, nilipata simu majira ya mchana ya kunitaka niwe Njombe asubuhi ya Leo!

SAA NNE na nusu usiku nikapata IT kitu cha Royal Crown! Tukaondoka tukiwa abiria watatu, tangu tunaondoka pale Rombo Kimara dereva nilimuona kama vile sio mtulivu! Akaniambia Boss wewe siti yako hii ya mbele, tukikutana na askari utanisaidia.

Hadi kufika Chalinze tukawa tumekoswa koswa mno! Tukamchukua Mwanajeshi dogo mmoja, tukawa wanne! Jamaa akaendesha lakini akawa anazidiwa na usingizi unamuona kabisa!

Kufika Mikese ikabidi tununue miwa na kisha tufungue madirisha! Safari ikaendelea kwa mbinde sana. Kufika kona za Iyovi, dah nashindwa kuandika maana nusura tuingie nyuma ya lorry! Kwa kweli tulipitaje hadi ninavyoandika sijui. I am alive that much I know!

Basi, ikabidi asimame nikachukua gari mimi ukumbuke hatufahamiani labda zole story tu za kum-keep busy! Nikaamua kuendesha kuanzia kwenye zile kona hadi Makambako ambapo tulifika SAA mbili kasoro asubuhi.

Hizi za magari ninazo nyingi but acheni Mungu aitwe Mungu.

Karibuni Njombe, usije na fulana kama mimi! Utapata ngiri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2013 niliitwa na rafiki yangu kwenda kumtembelea katika kazi zake.
jamaa alikuwa amenunua boat yake mwenyewe, ana NUNUA samaki uko visiwa vya Ukerewe analeta mwanza kuuza.
nimekaa uko kisiwani kama siku 4 hivi, siku ya 5 jamaa akawaambia wafanyakazi wa ile boat wa jiandae kwa ajiri ya safari ya kupeleka mzigo mwanza.
basi safari ikawadia, jamaa akaniambia niende na boat, yeye atazunguka kwa gari kupitia Bunda na tutakutana Mwanza.
Tulianza safari majira ya jion kabisa, usiku kucha had asubuhi yake, mwanza tukawa tu naiona kwa mbali.
Safari ilikuwa na changamoto kubwa sana, mvua upepo mkubwa sana na mawimbi makubwa yalikuwa yakisukasuka boat yetu, ilifikia hatua tuliamua kutia nanga ili upepo upungue.

hayo yana fanyika mimi nimelala tu.
sasa kutokana na upepo na mawimbi kuwa makubwa, kiwango cha mafuta yalitumika mengi kuliko kawaida, hali iliyopekea mafuta kutuishia kabla safari haijakamilika.
Wakati mafuta yanatuishi ilikuwa ni majira ya saa moja unusu asubuhi.
yule bahari mkuu wa ile boat akamwambia moja ya vijana wanao fanya nae kazi arushe Nanga ili wa fanye masailiano na boss(rafiki yangu) wamtaarifu kwamba mafuta yamewaishia.
Sasa kwakua mimi nilikuwa nimekaa upande wa mbele na ndo uliki Nanga, nikamwambia acha tu, nitarusha mimi mwenyewe, ikumbukwe kwamba wakati ili linakwenda kufanyika hali ya hewa ilikuwa bado ni mbaya, mawimbi makubwa yalikuwa bado yanapiga.
basi nikaenda kunyenyua ile Nanga niitupe ndani ya maji..
nilikuwa nimevaa sweta, sasa wakati narusha Nanga, Nanga ikaenda na mimi..
nilizama zaida ya futa 23 Nanga imeng'ang'ania sweta langu..
SIJUI NINI KILITOKEA, NANGA IKANIACHIA NIKARUDI JUU.
kwa kiasi kidogo najua kuyakata maji, lakini sio kwa kiwango cha kumudu kujiokoa.
Wakati narudi juu, ni kashika kamba ya nanga na yule bahari akawa ameshavua, yuko ndani ya boxer kwa ajiri ya kuja kuniokoa.
wale wengine wemeshika vichwa tu kwa mshangaoo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikua 95 nikielekea shule,ilikus kawaida kuongozana na rafiki yangu kila siku isipokua anaumwa ama mimi nnaumwa ama kuna aina yoyote ya dharura bas mmoja wetu atakwenda peke yake,siku hiyo niko peke yangu nikikatiza naeneo yasiyo na idadi kubwa ya watu nikamuona yule rafikiangu mbele yangu,nikaita kwa jina lake nae akanisubiri,tulitembea kwa dakika kama mbili na akadai niende taratibu afunge kamba ya kiatu nikakubali,sekunde kadhaa nageuka nyuma hakuna mtu kabisa ,nilipiga kelele na mama mmoja akatoka na nikamweleza kila kitu,yule mama alinisindikiza mpaka kwetu na ikawa mwisho wa kusoma ile shule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa naendesha gari,ghafla nikaona mdudu anatembea kwenye kidole changu,nikawa nafungua dirisha ili nimrushe kwa nje,ile niko katika harakati za kunyanyua mkono nimrushe,mwenzangu akaniambia kuna gari tunaligonga,lilikuwa linakuja opposite direction,wakati naangalia mbele ni kweli nimehama njia ila liko mbali kidogo na ile gari,na dereva wa lile gari alikuwa tayari ameshasogea pembeni kwani alishaona nimeyumba,niko katika harakati za kurudisha gari upande wangu yule mwenzangu akawa amenivuta mkono nilioshika sterling,kwakweli kilichotokea pale ni kwa neema ya Mungu tu tuko hai mpaka leo,gari iliyumba kama mara tatu huku tairi za upande mmoja zikiwa tayari juu,nikatumia ufundi wangu wote mpaka gari ikatulia,thanks God am still alive...
Baada ya kunusurika huyo mwenzako ulimzaba au hukumzaba makofi? Ahsante
 
Nikiwa dogo, kama darasa la nne hiv, home palikuwa karibu na shule sasa breki ya saa nne lazima nichomoke shule fasta hadi home napiga chai fasta then nageuka shule kabla break haijaisha.

Siku hiyo nimetimua mbio hatari kufika home chai hakuna kuna uji wa mtoto (mdogo wangu alikuwa anatambaa), kama mnavyojua uji wa watoto una mixer za hatari, karanga,soya, mchele mahindo nk nk basi utamu balaa nikafungua chupa (chupa za chai) nikapiga kapu mbili fasta nikarudisha chupa ili maza asijue kama nimeiba uji, afu nikazuga kumuuliza maza " mama mbona chai hamna" jibu la maza sasa "sijapika bado si huyo mdogo wako amevunja chupa nikiwa nimesha weka uji sasa nenda ukaumwage uji wote jalalani afu ulete hilo ganda la chupa nilioshe vzr tuanze kutunzia chumvi humo"

Aisee kufika jalalani kumwaga uji vinadondoka vipande vya chupa Tu (flask zile) nilichoka aisee nikawaza nimwambie maza au nikaushe.

Nikakausha, sasa usiku kimbembe nikishtuka toka usingizini najisemea mwenyewe "kumbe bado sijafa" Mungu ushukuriwe

NYINGINE
Tunacheza kombolela ile tumetimua mbio kwenda kujificha nikakanyaga mfuniko wa shimo la Choo lilikuwa lefu balaa ile naenda kutumbukia nikanasa kwa mikono nondo moja hiv i nikawa na ning'inia nikiangalia kinyesi kwa chini naona hadi wale funza wananisubili niachie nondo tu nikawavae huko, mara akatokea mdada mmoja lakini alikuwa na Upungufu wa akili nikajua anakuja kunikanyaga vidole ili niachie nakazame nikaanza kupiga kelele Yule dada aliponikaribia akafanya ile ishara ya kuweka kidole kwenye lips kuashiria nisipige kelele akanishika mabegani akanivuta kwa nguvu nikatoka.

Aisee nilimweshimu Yule chizi miaka yote niliyoishi mtaa ule hadi tunaama, huyo dada alikuwa anaitwa oliva majina ya oliva pia nayaheshimu pia

ASANTE MUNGU wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuamini kabisa kama ingetokea katika maisha yangu ,yani bila kutazamia ilitokea tu! Kwa kweli kuna mambo yanaweza kutokea bila kuzaniwa wala kufikiri ila nazani ni kwa ajiri ya maombi ya wengi hali yoyote inaweza kujiri.

Kwa kweli siamini hadi leo kama naweza kuwa hapa,yani ilikuwa mwaka 2015 miezi ya mwishoni ambapo mimi nilikuwa katika shughuri zangu mida ya saa 7 mchana maeneo fulani,alipita jamaa mmoja ambaye sikuzani kama angeweza ila ndo ikaja kuwa ,ndo huyu tunaye sasa ni JOHN POMBE MAGUFURI akiomba kura kwa wana nchi wa Tanzania na baada ya hapo akashika hatamu ya kuongoza nchi, dah siamini kabisa,jamaa anapiga kazi sijawahi ona,yani hata huyo nyoka wako angemuona huyo jamaa angetoka speed ya jet.viva POMBE

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani hiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,kwa sauti ya mkulu pombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kunusurika huyo mwenzako ulimzaba au hukumzaba makofi? Ahsante
Hapana mkuu,nilimsamehe kwakuwa inawezekana hakuwa yeye,kwani mpaka sasa siamini kama ni kwa akili zake angeweza kufanya tukio la hatari kama lile na hata yeye alijilaumu sana kwanini alichukua ule uamuzi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom