Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
(Sometimes in our future)
Ni siku ya Jumamosi usiku. Watu wakiwa wamelala, watu ambao wako bado kwenye kufurahia mwisho wa juma bado wanamalizia chimpumu cha mwisho mwisho na wenye kufurahia muziki wako wanajimwaga kwenye kumbi mbalimbali. Kunasikika tetemeko kidogo ambalo limezoelewa maeneo ya Rukwa na Mbeya; Watu wakiwa wanajua ni "yale yale" ya kawaida, sekunde thelathini baadaye tetemeko kubwa linapiga na kutikisa kwa karibu sekunde kumi hivi. Mtikisiko wake unawaamsha watu waliolala huko Dar, Morogoro, hadi Tanga. Watu wanajiuliza ni nini kimetokea. Wengine wanasema ni "mlipuko wa mabomu kama kule Mbagala, wengine wanasema ni kulipuka kwa kituo cha mafuta".
Mara sms zinaanza kutembea na kuwataka watu waangalie TV na kwenye kituo cha kimataifa cha CNN kinaonesha kuwa kumetokea Tetemeko kubwa la ardhi kusini mwa Tanzania na linaonekana kufikia kiasi cha 7.6 kwenye kipimo cha Richter. Watu wanajaribu kupiga simu Mbeya haziingii, mawasiliano na Rukwa yamekatika. Kunapopambazuka siku ya Jumapili ndio tunaanza kupata picha ya kile kilichotokea: Kwa ufupi hali halisi ya Jumapili ya Tetemeko la Rukwa iko hivi:
NB: Makala ifuatayo ni ya hadhara. Chombo chochote cha habari chaweza kuitumia kwa kuichapa bila kubadilisha jina la mtunzi na lifuatalo:
Mwandishi ni Mtanzania anayeishi Marekani, na ni mwandishi wa makala mbalimbali za kisiasa na kijamii zinazohusu Tanzania na ni mwanachama mwandamizi wa mtandao maarufu wa JamiiForums.com.

- Nyumba zaidi ya 100,000 kati ya mikoa ya Rukwa, Mbeya na Iringa zimebomoka kabisa
- Makisio ya awali yanaonesha watu wapatao 25000 wamekufa na zaidi ya milioni 1.5 hawana makazi. Idadi inaweza kubadilika.
- Majengo kadhaa yameshika moto
- Barabara kuu ya kwenda Zambia imeharibika kabisa na haipitiki
- Reli ya Tazara imevunjika vunjika hasa maeneo kati ya Iringa na Mbeya
- Hospitali ya Rufaa Mbeya imebomoka, Hospitali ya Wazazi Meta imebomoka; hospitali pekee iliyo karibu ni zile za Songea au Malawi
- Kambi za Jeshi Uyole, JKT Nzovwe zote zimeharibika
- Rais yuko nje ya nchi safarini
- Bunge liko katika kuahirishwa
- n.k