Unakumbuka Tetemeko la Rukwa 1910?


Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,749
Likes
7,623
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,749 7,623 280
(Sometimes in our future)

Ni siku ya Jumamosi usiku. Watu wakiwa wamelala, watu ambao wako bado kwenye kufurahia mwisho wa juma bado wanamalizia chimpumu cha mwisho mwisho na wenye kufurahia muziki wako wanajimwaga kwenye kumbi mbalimbali. Kunasikika tetemeko kidogo ambalo limezoelewa maeneo ya Rukwa na Mbeya; Watu wakiwa wanajua ni "yale yale" ya kawaida, sekunde thelathini baadaye tetemeko kubwa linapiga na kutikisa kwa karibu sekunde kumi hivi. Mtikisiko wake unawaamsha watu waliolala huko Dar, Morogoro, hadi Tanga. Watu wanajiuliza ni nini kimetokea. Wengine wanasema ni "mlipuko wa mabomu kama kule Mbagala, wengine wanasema ni kulipuka kwa kituo cha mafuta".

Mara sms zinaanza kutembea na kuwataka watu waangalie TV na kwenye kituo cha kimataifa cha CNN kinaonesha kuwa kumetokea Tetemeko kubwa la ardhi kusini mwa Tanzania na linaonekana kufikia kiasi cha 7.6 kwenye kipimo cha Richter. Watu wanajaribu kupiga simu Mbeya haziingii, mawasiliano na Rukwa yamekatika. Kunapopambazuka siku ya Jumapili ndio tunaanza kupata picha ya kile kilichotokea: Kwa ufupi hali halisi ya Jumapili ya Tetemeko la Rukwa iko hivi:
  • Nyumba zaidi ya 100,000 kati ya mikoa ya Rukwa, Mbeya na Iringa zimebomoka kabisa
  • Makisio ya awali yanaonesha watu wapatao 25000 wamekufa na zaidi ya milioni 1.5 hawana makazi. Idadi inaweza kubadilika.
  • Majengo kadhaa yameshika moto
  • Barabara kuu ya kwenda Zambia imeharibika kabisa na haipitiki
  • Reli ya Tazara imevunjika vunjika hasa maeneo kati ya Iringa na Mbeya
  • Hospitali ya Rufaa Mbeya imebomoka, Hospitali ya Wazazi Meta imebomoka; hospitali pekee iliyo karibu ni zile za Songea au Malawi
  • Kambi za Jeshi Uyole, JKT Nzovwe zote zimeharibika
  • Rais yuko nje ya nchi safarini
  • Bunge liko katika kuahirishwa
  • n.k
Unaweza kupata picha ya uharibifu unaoweza kutokea. Nafahamu mtu mwingine anasoma hayo na haamini yanaweza kutokea Tanzania kwa sababu sisi nchi yetu ni ya "amani, umoja, utulivu na mshikamano"; kwamba tuna kaupendeleo ka aina fulani mbele za Mungu! Hivyo anajisemea "huyu mwanakijiji anataka kutuchulia"!

NB: Makala ifuatayo ni ya hadhara. Chombo chochote cha habari chaweza kuitumia kwa kuichapa bila kubadilisha jina la mtunzi na lifuatalo:

Mwandishi ni Mtanzania anayeishi Marekani, na ni mwandishi wa makala mbalimbali za kisiasa na kijamii zinazohusu Tanzania na ni mwanachama mwandamizi wa mtandao maarufu wa JamiiForums.com.
 

Attachments:

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
19
Points
135

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 19 135
La kuzingatia ni kuwa tetemeko linaweza kutokea popote. Ila wakubwa will not care, si hata TMA wameshatoa angalizo kuhusu mvua? Tusubiri tuone............
 

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
655
Likes
19
Points
35

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
655 19 35
mwanakijiji....una uhakika ilikuwa ni mwaka 1910?
Hata mimi hapo mwanakijiji ameniacha hoi. Hii ni fiction ila ingepelekwa miaka ya mbele kidogo. Kwani katika kipindi hicho hata reli ya Tazara ilikuwa bado haijajengwa, halafu SMS, mara CNN, mara magazeti asubuhi. Kipindi hicho Tanganyika ilikuwa bado chini ya Mjerumani sasa hizo zipi tena MMk?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,749
Likes
7,623
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,749 7,623 280
Hata mimi hapo mwanakijiji ameniacha hoi. Hii ni fiction ila ingepelekwa miaka ya mbele kidogo. Kwani katika kipindi hicho hata reli ya Tazara ilikuwa bado haijajengwa, halafu SMS, mara CNN, mara magazeti asubuhi. Kipindi hicho Tanganyika ilikuwa bado chini ya Mjerumani sasa hizo zipi tena MMk?
inaonekana huamini kuwa miaka 100 iliyopita lilitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Rukwa!.. someni basi hiyo attachment jamani..
 

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
655
Likes
19
Points
35

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
655 19 35
inaonekana huamini kuwa miaka 100 iliyopita lilitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Rukwa!.. someni basi hiyo attachment jamani..
Ni kweli kulitokea tetemeko. Nimeisoma makala yako kwa upande mmoja(nadharia) ipo sahihi kabisa, ila katika utendaji ni mpaka yatufike.

Mfano: watu wanauliza hawa zimamoto wanafanya kazi gani kama hamna moto. Si heri tuwenao wa kujitolea. Watu wengi (waTZ) wanafikiri maswala ya disastor prevention/recovery sio muhimu. wengi wanafikiri ni kupoteza resources kuwakeep hawa jamaa. Lakini wakiangalia umuhimu baada ya janga ndo utawasikia "oooh!".

Kwa ujumla kungekuwa na Insurance Policy inayosimamiwa vizuri, ingekuwa ni rahisi sana ku-implement idea zako. Ila sisi tumezidi ujanja ujanja ambao ndio unaoturudisha nyuma.

Swala hili linapaswa kufundishwa tangu shule za msingi. Tatizo kubwa kwa Tanzania watu sio rasilimali (Human is not a resource). Tunajidharau, tunadharauliana, ubinafsi umetuzidi.

Hayo ndio matatizo makubwa katika jamii yetu. Hata hii amani tunayoiimba ni kutokana na ubinafsi. Kila mtu ni mnafiki, pale anapokula anajifanya hali halafu anajifanya kuna amani.

Aaaagh! Watu wanamipango, Taifa halina ramani!
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,749
Likes
7,623
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,749 7,623 280
Mmh.MUNGU epushia mbali.
haya ndiyo yananisumbua kichwa; haijalishi kama tutasali hivi, tufatunga au tutapiga magoti na kuvaa magunia. Mungu ameziweka sheria za ulimwengu ziutawale ulimwengu. Tetemeko kama hili litatokea siku moja Tanzania. Na hofu yangu yawezekana siyo mbali kama watu wanavyotaka kuombea.
 

Obi

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
376
Likes
4
Points
35

Obi

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2009
376 4 35
MMK heshima mbele,

Uyasemayo ni kweli naungana nawe kwa asilimia miamoja. Pale chuo kikuu cha DSM kuna kitengo kinachogihusisha na maswala ya matetemeko ya ardhi na majanga ya tabia nchi (Geohazards).

Data zao zinaonyesha kuwa kuna active faults in Northen and western African Rift System yenye uwezo wa kuamsha tetemeko wakati wowote ndani na nje ya nchi yetu.
Cha msingi ni Tanzania kufanyia kazi tafiti za wataalamu wake ili angalau kukabiliana na madhara yatakayotokea.

Tetemeko halizuiliki ila tahadhari ni muhimu zaidi.
 
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
24
Points
0

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 24 0
Nakubaliana na wewe.Ni muhimu kumuomba MUNGU kwani nchi yetu iko nyuma mno katika kujiandaa na majanga(disastare preparedness) hasa makubwa kama haya.Tunashindwa kuwahi kwenda kurescue moto kwa muda maufaka tena nadani ya majiji sembuse majanga ya matetemeko.Tumelala mno kiutekelezaji ingawa mipango yetu imekaa vizuri mno.We ona hata jinsi ya kusaidia wenzetu Kilosa hali ilivyosuasua.Eti viongozi wetu wengine ndio wameenda juzi.,wakati tukio lilitokea kitambo mpaka baadhi ya watu wameshasahau.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,749
Likes
7,623
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,749 7,623 280
Nakubaliana na wewe.Ni muhimu kumuomba MUNGU kwani nchi yetu iko nyuma mno katika kujiandaa na majanga(disastare preparedness) hasa makubwa kama haya.Tunashindwa kuwahi kwenda kurescue moto kwa muda maufaka tena nadani ya majiji sembuse majanga ya matetemeko.Tumelala mno kiutekelezaji ingawa mipango yetu imekaa vizuri mno.We ona hata jinsi ya kusaidia wenzetu Kilosa hali ilivyosuasua.Eti viongozi wetu wengine ndio wameenda juzi.,wakati tukio lilitokea kitambo mpaka baadhi ya watu wameshasahau.
nyie subirini tu.. tutaambiwa hapa oh "wanatuchulia"!
 

Forum statistics

Threads 1,204,152
Members 457,147
Posts 28,143,294