UMMA UMTENDEE HAKI EDWARD MORINGE SOKINE, TUNAYO HAKI YA KUJUA NI NANI WALIOKUWA NYUMA YA KIFO CHAKE, JE NI KWELI KAWAWA? MSUYA? NA NANI WALE? TUNAPENDA KUUFAHAMU UKWELI MAANA KAMA NI KWELI ALIUAWA BASI TUWAANGALIE VIONGOZI WETU WA ZAMA HIZO WALIOKUWA NA SURA ZA KIBEPARI NA KUJIFANYA WAJAMAA, NILIKUWA KIJANA WA MIAKA 11 BY THEN BUT NAIKUMBUKA HALI YA MVUA NZITO KULE KIJIJINI KAMA ILIVYOKUWA 2WEEKS HIZI HAPA DAR,YALIKUWA NI MAOMBOLEZO TOKA ROHONI TOKA KWA WATOTO MPAKA WAZEE,NI MAUMIVU YA KWELI,ndio maana ninahamu ya kuangalia TBC1 kama wana lolote kwa kutwa ya kesho hao wengine sitarajii maana wengine ni matunda ya kifo cha Sokoine ila wanajifanya wanataka haki sasa na kusahau walichoifanyia Tanzania zama zao.
Kalamu, tatizo hawataki kuzungumza; yaani kuweka historia yetu kwenye maandishi ni kazi sana..
Ni kweli lazima akane Bwana. Unajua kilichompata Dr. Fupi wa Morogoro ambaye alifanya postmoterm? Hii ndiyo Tanzania, hata hivyo katika Tanzania hii tunao viongozi wenye uchungu halisi nanchi yao ambao kwasasa hatunao tena. Wish them RIP.
Mzee wa Kijijini.
Namkumbuka vilivyo huyu jemedari Moringe Sokoine wakati wa vita vya uhujumu uchumi alikuwa imara kweli kutetea wanyonge.Huyu hastahili kusahauliwa katu kwa kazi yake njema maana amekuwa piawaziri mkuu ktk nchi hii tena kwa vipindi viwili tena wakati chama kikiwa hiki sisiem.Yaani mwaka 1977-80 na Mwaka 1983-84.Huyu jemedari hakuangalia uso wa mtu,kwa kweli tulipoteza mwarubaini wa Taifa hili.
Wakati wa kifo chake Moringe sokoine nakumbuka yule Kijana wake wa kwanza aitwaye LAZARO alikuwa anasoma Cuba.Toka hapo sijasikia kama naye kaingizwa NEC au hata jumuia ya vijana ya sisiem ili kukumbuka mchango wa huyu jemedari.Nyerere akifufuka na kukuta sisiem hii atakufa tena maana imekuwa ya mke na mme na watoto wote NEC.
Wako wapi hawa watoto?huyu LAZARO NA MWINGINE ALIIITWA JOSEPH MORINGE SOKOINE?
Wake zake pale Monduli juu sijui kama wako safi kimaisha maana kipindi kile hakikuwa na mwanya wa kupora kama tunavyoona wake wa marais na mawaziri wakuu wanavyotengeneza mafuko ya fedha ya kuleta maendeleo na pia fursa sawa kwa wanawake wote(ha ha ha),ngoja nicheke kidogo.
Tudumishe mema yote ya MORINGE SOKOINE
Prof Shaba ndie alifanya postmortem ya kifo cha sokoine na hakufa labda kama kafa hivi karibuni maana mara ya mwisho nimemwona 1998.Na waliosoma Muhimbili watakuwa wanamjua maana alikuwa akifundisha hapo.
CCM NI NGO YA WAKUBWA
Kalamu, tatizo hawataki kuzungumza; yaani kuweka historia yetu kwenye maandishi ni kazi sana..