Unakumbuka nini kutoka kwa Mama yako

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Unakumbuka nini kutoka kwa mama yako?

Nakumbuka siku alipokubali kurudiana na mzee wangu aliyekuwa mlevi kupindukia ili tu aturehe wanae tuliokuwa bado wadogo,(mzee alikwishapagawa maaana hakuwa na kitu tena baada ya kuachana na mama)

Kwa kweli mama yangu alipoitwa kusuluishiwa Ndoa yao iliyovunjika takribani miaka mitatu nyuma alikuwa na msimamo mmoja tu atarudiana nae kwa sababu yetu sisi wanae ila anaomba mzee aache pombe na ni kweli ,

Kwa maneno ya mama na tuliyoyapitia mzee aliacha pombe,aliacha kuvuta sigara na kila kitu ninavyozungumza sasa Baba yangu ni mwanadini mkubwa na Mama yangu kipenzi,

Wapo na maisha yao ya kila siku na Ndoa yao ina furaha.


Nakupenda sana Mama yangu.

CC Zero IQ
 
Anayo password ya akili na moyo wangu. Kuna vitu hua anavijua bila mimi kumwambia. Akiniangalia tu, anajua huyu mtu hajala au kuna kitu kinamsumbua kichwani au kuna jambo limenifurahisha. Kuna wakati anapiga simu, ananiambia nimeota unalia, nini kinakusumbua? Basi ntazuga kila kitu kiko sawa, ila deep down najua kuna kitu kinasumbua. Sijui hua anawezaje asee!
 
Nakumbuka mengi sana hasa la kupenda kusoma na akaniambia ww soma hadi uchoke mwenyewe maana Mimi mama yako sijasoma, napenda wewe mwanangu usome sana.

Kitu kingine ni kunitabiria, saizi nimepiga marufuku mambo ya kutabiriana maana huwa yananipata sana. Hadi akaniambia uache ubishi ndy nitaacha kukutabiria.

Nakupenda Mama, siwezi eleza
 
Back
Top Bottom