Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Jul 14, 2008
1,820
1,031
Wazalendo;

Moja ya sehemu ya maisha yangu ambayo kamwe sitasahu ni kupitia JKT.

Nilijiunga na JKT Ruvu na baadaye nikaenda Service Buhemba Lwamkoma.

Sitosahau kamwe mafunzo ya ukakamavu, kwata, mchaka mchaka, disko na vitimbi mbalimbali kati ya Makuruta na Maafande. Nilikuwa Combania E.

Moja ya vituko vya kukumbuka ni simulizi kutoka- Operation OKOA, kulikuwa na huyu jamaa alikuwa ni mweusi sana anaitwa afande Lucas, badala ya kuwaaamsha kuruta kwa filimbi, alikuwa anaingia na kuvuta Sigara. Kuruta inatakiwa ukisikia harufu ya Sigara uamke na kufoleni nje. Usipotoka in time unakula mijeledi.

Basi siku moja Kuruta wakapanga wamfanyizie na wakatoka mapema nje na kujificha huku ndani kwenye Bweni wakiyaviringisha mablanketi mithili ya mtu amelala. Afande alipomaliza sigara hakuna aliyetoka akajua siku hiyo kuruta wamegoma kuamka na kuanza kuchapa viboko yale mablanketi yaliyovingirishwa. Alishtukia kaanza kushambuliwa yeye na kuruta toka nje ambao walikuwa na fimbo kibao mpaka akakoma.

Kisha kuruta wakafoleni nje. Nakumbuka Mkuu wa Kombania alipata habari na kulikuwa na drill si kawaida na mpaka push ups za kunusa mkojo katika nyasi walizokuwa wanakojoa kuruta usiku. Hata hivyo yule afande naye alikoma kwani hakurudia mchezo wa kuwaamsha watu kwa sigara.

Kwa waliokuwa Ruvu Operation Okoa:

Na miss
  • Ugali na korosho mnapojongo kambini
  • Mihogo ya Vibwende kwa Babu
  • Wali na Maembe
  • Uji wa Mestin ya Jeshi
  • Bukta na Green Vest
  • Kuokota kuni
  • Bustani
  • Michezo
  • Disco
... Ama Johnnnnn ambaaaa ambaaa John, amba Johnnn waTanzania. Arusha Mbali, Arusha Mbali, tukumbukane kwa Barua nk...

Nakumbuka pia siku moja sikuimbisha disco vizuri na kipindi kile 1985 bado kulikuwa kuna ubaguzi wa rangi Africa Kusini, basi afande akanipiga mkwala na kuniambia.

"Kuruta nitakutemea mate yenye sumu usoni upofuke macho, na sijui utatibiwa wapi kwani mipaka yote Afrika Kusini imefungwa. . . (Kana kwamba hakukuwa na hospitali ya kutibu mate ya sumu hapa bongo"

Jamani mliokosa JKT, mlikosa mengi, japo tulipata tabu lakini tulijifunza mengi katika maisha.

Je, wewe unakumbuka nini?

Soma pia:

1) JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?
 
Umenikumbusha mbali sana mie niliudhuria ile miaka ya mwishoni ya themanini (1989/90) Pale kambi ya Ruvu kombania ya B kuna afande alikuwa anaitwa Nyundo. Huyu afande hatukubahatika kumuona akiwa amefurahi kila siku sura yake ili kuwa ya kazi kazi.

Mwenyewe alikuwa anajiita ndio handsome wa kwao. Nakumbuka moja ya wimbo ambao alitufundisha muda wa disco ulikuwa wa Malela.... na mwingine ulikuwa nadhani wa kishona kama sijakosea unaitwa Kule kule kwa chinoma....
Kitu kingine nakumbuka ni ufugaji wa kuku kule phase 2 pamoja na kusimamisha minazi serengeti muda wa jioni.
 
Mie nilianzia Msange JKT na kumalizia hapo - OPERATION program ya chama. Tulikuwa na Afande Mohamed, Mrope, Odo, Mandevu, Matron Gwimo, Magege, na wengine kibao ila majina yashaanza kunitoka. Hii ilikuwa mwaka 1989/90.

Leo ntaweka kituko kimoja tu kutoka kwa jamaa mmoja aliyekuwa akienda kwa jina la Ukunu au Pepo. Huyu Matron Gwimo alikuwa na tabia ya kuja na kuingia bweni la wavulana na kuamsha bila ya kutoa warning.

Hiki kitendo kilituudhi sana na siku ya mkutano watu wakapania kumsemea. Wengi wakawa wanalalamika ila wanaogopa kumtaja Matron huyo ni yupi. Ukunu alisimama na kusema Matron huyo ni Gwimo.

Hapo niliona sura za Ma-afande zikianza kuwa nyekundu kwa hasira na nikajua kuwa wakitoka hapo watauwa mtu. Jamaa akaendelea ".. huyu afande alishasababisha mgomo kumbaini B watu wakakataa kula.

Huyu alifanya ..... na afande unajua kuwa sisi wanaume tukilala, asubuhi tunapoamka huwa tunakuwa na MIGOGORO........" Lohhh, watu walicheka hadi wakalala na mkutano ukawa umefia hapohapo maana hata afande mwenyewe machozi yalikuwa yakitoka kwa kucheka.

Mkutano ulifungwa na Sajenti Manyilizu na luteni Mohamed alijikaza kwa shida kupigiwa saluti. Alipovua tu kofia akaangua tena kicheko.

Ikawa kila siku wasichana wakimuona asubuhi wanamuuliza ".. kaka Manara, vipi leo mgogoro ulikuwaje?". Ila maajabu yalikuwa kuona wanawake na wanaume wakioga UCHI katika umbali wa mita kama 5 hivi.

Na unapatwa na mshangao unapochota maji, vilikuwepo vi-plastic sijui vilikuwa vya nini, basi watu wakawa wanatekea maji kisimani. Sasa anakuja dada na kusema "..... na mimi naomba hicho kikondom cha tembo nichotee maji" Kweli wanawake wakimaliza JKT huwaambii kitu. Tofauti yao na wanaume tuseme ukweli haipo.
 
Sanctus,

Mimi niliamua kukwepa kwenda Tabora na kuamua kwenda Oljoro kwasababu nilikuwa na kakangu mjini Arusha. Nikajua nikitoroka nitakuwa na sehemu kwa kubugia ugali.

Basi kufika Oljoro, tukamkuta afande Dauda, (sijui kama linaandikwa hivyo) alikuwa ndio mkuu wa mafunzo. Akasema mwaka jana alitoa kibali cha kuua kruta watano, akasema aligundua haikutosha, anawaamrisha maafande mwaka huu kuua kruta mpaka 15.

Kesho yake watu kibao wakatoroka na kwenda ku report kambi zingine. Isingelikuwa kuwa na brother hapo mjini na mimi ningelirudi kule Tabora usiku huo. Baada ya muda tukaja gundua kumbe Dauda ndiye alikuwa afande poa kuliko wengine wote.

Tulikuwa na afande mmoja Mhehe alikuwa anaitwa Mduda. Alikuwa anajifanya anajua jeshi kweli kweli. Akaopoa mtoto wa maana sana. Siku moja tumemaliza jeshi tuko mlimani, akaingia mlimani hall D na magwanda, kaja kufuata mtoto wake. Maskini yule msichana alikuwa terrified, akajificha. Jamaa akasubiri pale wee, mpaka akaamua kujikata. Alifikiri yale ya jeshini yanaendelea uraiani. Tulimsanifu kweli siku hiyo.

Looh! ni miaka karibu 20 toka wengine tuondoke JKT lakini naona michapo yake inakuja tu. Waswahili tungelikuwa tunaandika vitabu, tuna mengi ya kusimulia.
 
Wengine tulikosa jeshi kwasababu ya sheria kuwa ilishafutwa lakini hapo Same Secondary napo ilikuwa kama jeshi tu.

jmushi1, wakati ni ukuta na kila kitu na zama zake.

Ila kwa kweli wachache tuliobahatika tuna mengi sana ya kukumbuka kwa kuwa kila siku ilikuwa nis siku ya visa vipya kabisa na ilimfanya kila mtu awe mbunifu. Hakukuwa na mtoto wa mkubwa wala mdogo, wote ilikuwa ni kwata mtindo moja.

Utamsikia jamaa anang'aka . . . "Kuruta, nimewaambia mkae chini nyie MNA-OBEY OBEY tu, sasa mtaipata fresh" (OBEY akiwa na maana mnagoma) . . . .

"Sasa mtakula Push-Ups mpaka MTASHAA (Mtakoma) . . . Nikisema UP mnakwenda chini, na nikisema DOWN mnakwenda juu" of course wanaojua UP na DOWN ni nini wanafanya tofauti hapo ndo mtaona kazi. Atawaita na wenzake mtakula drill mpaka basi kwa kuwa MNA OBEY OBEY.

Jamaa atapiga mkwala kuwa natka uzunguke uwanjaa huu mara mbili, NIKISEMA GO TU, UWE UMESHARUDI . . . . Du, JKT, I love it and I miss it.
 
Wengine tulikosa jeshi kwasababu ya sheria kuwa ilishafutwa lakini hapo Same Secondary napo ilikuwa kama jeshi tu.

Dogo huku-miss kitu:

I hate that d@mn thing JKT. Dakika za mwisho nilikuwa Ruvu JKT. Unavaa nguo zinazofanana na mtoto wa waziri au Brigedia wa jeshi na wewe unaisi mko kwenye ligi moja. Lakini ngoja Jeshi limalizike uone wenzako wako wapi na wewe huko wapi?
 
Mtu wa Kawaida,

Haaa haaa "Kule Kisimani mama kuna sitorudi tena . . . matumbili na manyani yanaogelea . . . . " Duuu, raha tupu mkuu!

Mkuu, kule kwenye kufuga kuku, watu walikula sana mayai mabichi.

Yeah, Jioni kabla ya Disco, kulikuwa na hizi za kwenda serengeti . . . kwa wadada na foleni za kwenda kula jikoni . . . . "Siyame Twende kula siame oyaaaa oyyaaa" na hapo wote waliojongo wanaunga bogi.

Ila kwa kweli hakukuwa na tofauti kati ya akina dada na akina kaka. Wote ndani ya Bukta na Green Vest za kijani. Nilikuwa nawaonea huruma sana.
 
Sikonge,

Mkuu sijakupata, unatunyima raha, kama ni blue print fafanua kwa lugha ya uungwana tuelewe.

Umenikumbusha mambo ya kuoga na Mestin pale maji yanapokosekana na bado unatakiwa utakate. Ni kweli watu hawakuwa na aibu ya utupu.

Siku moja kamanda moja mwenye nyota mbili sikumbuki jina, alikuwa na binocular wakati tunakata kuni. Akaniambia " Kijana tunajua mambo mengi sana mnayo fanya ila tunamezea wakati mwingine" nilipomwuliza kwa nini akanipa binocular na kulielekeza wapi niangalie, huwezi amini, kulikuwa na askari kuruta wa jeshi wa kike na kiume wakifanya kamchezo kabaya . . . baada ya kukata kuni. Du, nilibaki hoi sana
 
Mtanzania,

Mzalendo Mtanzania,

Umenichekesha sana juu ya kibali cha huyu bwana cha kuua watu . Na umenikumbusha Court Marsha moja Ruvu JKT ilimuhukumu afande moja kifungo kwa kuwa siku za nyuma alimwamuru kuruta ashike kinyesi. Jamaa alisota sana Lupango.

Du, huyu afande aliyefuatilia uraiani ndo kanimaliza sana. Hajui watu walikuwa wana namna zao za kupunguza makali ya jeshi. Kama unakumbuka ukiwa na C, unakuwa mlinzi wa Hanger.

Nakumbuka Jeshini nilibuni taaluma ya kuwa fundi wa kutengeneza vitanda vobovu mambo yanapokuwa magumu. Nilipokuwa Buhemba nikabuni kuwa Mimi ni Kocha wa Basket Ball. Jamaa wakanishtukia baada ya muda na kunipeleka Lwamkoma kulima Pamba. Ndugu yangu si mchezo, kuna mashamba yanaitwa EMBAKASI (Kwa maana ya Airport), unapewa tuta ukiwa katikati mwanzo huoni wala mwisho. Chakula mnaletewa huko huko.

Bro, nilitaka kutoroka jeshi kwa machungu. Kuna huyu afande wa Kimasai anaitwa Moreli akanidaka nilikuwa na mahindi ya kuchoma ya shamba la jeshi, alikuwa na kiboko cha kama chuma chembamba, jamaa alinipiga kama mwizi. Mkuu nilitaka nirudi home kwa miguuu nikagundua isingwezekana. Sasa hivi nikikumbuka naona raha tu. Someone should write a book of all these stories.
 
Hapo nitapenda kuwakumbusha wale tuliokuwa wote pale Mafinga JKT Kombania F chini ya OC Rweikaza na yule afande invisible aliye julikana kwa jina la Master Follow-up. Tutamkumbuka afande kijana aliyeitwa Mwakyosi. Nakumbuka siku moja tuliamshwa saa kumi alfajiri kama ilivyokuwa kawaida kukata mifagio wakati tukielekea huko porini kukata mifagio kwa mchaka mchaka tuliambiwa twende tukiimba, nikaanzisha wimbo "...Siasa yetu hapana mbaya. Isipokuwa maafande ndiyo wabaya..." Jamaa kusikia mistari ile akaamuru wote kuchuchumaa chini na kuruka kichura chura.

Upande wa Afande Master Follow-up au Afande Mlimbila ambaye sasa ni marehemu, nakumbuka siku moja alimuuliza kuruta mmoja kwamba alipataje kovu lililo katika paja karibu na nyonga. Tamko lile lilizua kilio kwa binti yule na binti alikwenda moja kwa moja kwa CO T N Mlay kutoa taarifa kuhusu mauza uza aliyoyaona usiku ambapo alisema alikuwa akiota kuna mtu amevinjari naye usiku kucha na iweje afande atamke kuhusu kovu wakati ni kweli analo na alijuaje wakati hajawahi kuwa naye kwa makubaliano.

Kifo cha Master Follow-up: Siku hiyo kulikuwa na mkutano mkuu wa wakuu wa vikosi Ma-CO nchini wakati huo Mlimbila alipangiwa kulinda kituo kidogo cha JKT kilichoitwa Sao Hill ambako kulikuwa na mradi wa kuchoma mkaa. Jamaa akakaimu kazi hii kwa mtu mwingine yeye akabaki kikosini. Pale kikosini kulikuwa na afande mmoja Mngoni aliyekuwa na mkewe dogo dogo aliyeishi karibu kabisa na apartment au hanga la Mlimbila.

Na afande huyu Mngoni alipangiwa kulinda geti dogo karibu kabisa na nyumbani kwake na inaelekea alishapata fununu za mtoto (Mkewe) kuvinjari na Mlimbila. Muda wa saa mbili usiku bwaloni kukiwa na dance la kumalizika kwa mkutano afande Mngoni akaaga kwenda nyumani kwake "kukagu". Inasemekana alifika akagonga mlangoni bila kufunguliwa, kisha akaenda kuchungulia dirishani na kumuona Mlimbila akiwa ameketi kitandani akiwa mtupu na mke wake afande Mngoni. Alilenga SMG kupitia upenyo wa dirisha na kumkuta Mlimbila katikati ya paji la uso kuona vile binti alikimblia sebuleni na kufungua mlango na kukimbia.

Mngoni aliingia na kuuchakaza mwili kila sehemu kwa risasi. Alibakiwa na risasi kama tisa tu. Mwili wake ulipelekwa Mafinga Hospital kujazwa pamba ili angalau uso wake uweze kutambulika. Haya ndiyo nayakumbuka sana ninawakumbuka kuruta wenzangu akina Tarama Mamkwe, Ndubula Msaki, Rachel Mapande, na wengineo.
 
Du mmenikumbusha mbali sana.

Nilikuwepo Mafinga Danger coy wakati wa ukuruta na Sir major Mulembo na afande Nusu mungu (Daniel Muungwana) alikuwa anadai eti mama yake alalamika kwa mwaka mzima alikuwa hajampelekea kichwa cha kuruta.

Baadaye nikamalizia Itende JKT na detach yake ya itaka kwenye mashamba ya mahindi yaliyoitwa mbuga. Itende alikuwako afande Bokassa siku moja tulikuwa tuweka mbolea kwenye mikahawa basi kukawa na dalili zote za kunyesha mvua. Tukamwambia hali ya hewa ni mbaya afande; akasema hapana hali ya hewa ni nzuri endeleeni lazima ng'ombe atue A coy. maana CO alishatangaza kombainia itakayoshinda kwa kilimo itapata ng'ombe.

Basi mvua ikaanza kunyesha wakati mifuko iliyojaa mbolea ikiwa shambani, akaanza kumalisha chukueni mbolea mpeleke kwenye kibanda isilowane tukamwambia hapana afande hali ya hewa ni nzuri. ilibidi aanze yeye kubeba kwa kuogopa adhabu kikosini. tukamwambia hatutaki ng'ombe sisi. tulipofika kikosini tukatuta order ya CO- Bokasa amehamishwa kombania.
 
Kwa kweli nimesisimka sana kwa yote; kwani limepelekwa mbali sana na kila mchangiaji.

Mimi nilianzia mgombo-kabuku tanga na kumalizia maramba; 1989\90.lamsingi kwa wadau wote ili historia isipotee; ni vyema ifanyike documentation na hatimaye itayarishwe video series\film.
Hapo tutakuwa tumejitendea haki wadau wote na jkt kwa ujumla.

Napendekeza iundwe team ya kukusanya matukio na habari zote zilizotokea; ili iandikwe healthy script itakayotoa best and exciting picture of what really happened in those camps.
 
Jibaba Bonge,

Du! Mzalendo umenichekesha sana mpaka nimetoka machozi . . . Huo mkwala wa afande wa kumpelekea mama yake kichwa cha kuruta ni mzito sana . . .

I hope we have more to share.
 
yaan ndgu umenikumbusha mengi sana,nilianzia mafinga jkt op miaka 20 ya azimio la arusha(june 1987-june 1988) baada ya kumaliza form VI pale milambo sec tabora,nilipangiwa jkt mafinga nlikuwa na school mate wangu anthony thomas(tony lover) ,gosbert john(mwamba) wote hawa nilikuwa nao O-LEVEL Azania sasa hivi wote ni marehemu.

Nnakumbuka jinsi nilivyojifanya mimi ni usalama wa taifa na maafande kuniogopa kwa kunipa kazi ndogondgo,nawakumbuka afande lubega,masoli hawa co watu ni wanyama kabisa.

Service YANGU nilikuwa buhemba,kule kdgo ilikuwa safi lakini kuna afande mausha alinikera sana kwani mwanamke(service woman) aliyemtaki yeye alikuwa gf wamgu kwahiyo tulikuwa hatuivii kabisa.
 
Back
Top Bottom