Unakumbuka nini enzi hizo hasa ukisikia nyimbo hizi..!!!!

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2008
Messages
260
Likes
7
Points
35

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2008
260 7 35
Maroon Commandos kutoka Kenya - Charonyi ni wasi

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=zqIJNJB73Ug"]http://www.youtube.com/watch?v=zqIJNJB73Ug[/ame]

Mpongo Love - Ndaya

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=6F7lHM90KwI"]http://www.youtube.com/watch?v=6F7lHM90KwI[/ame]


Macho yanacheka Moyo unalia

http://www.eastafricantube.com/media/1414/Taarab_-_Macho_Yanacheka_Moyo_Unalia/


Binafsi nakumbuka mbali sana enzi hizo radio zilikuwa ni National na Philips tu na zilikuwa zinauzwa kwenye maduka ya RTC.

Nakumbuka maduka yale yalikuwa yanaitwa Bora yalikuwa karibu kila mkoa, walikuwa wanauza viatu vikiitwa safari boot, pamoja na raba mtoni zilikuwa zinaitwa Bora.

Nakumbuka enzi hizo daftari za mistari mikubwa na midogo kwa ajili ya kujifunza mwandiko kwa wanafunzi zilikuwa zinapatikana maduka ya Tanzania Elimu Supplies tu.

Nakumbuka pia tulikuwa tunapewa madaftari bure shuleni kila mwaka shule ikifunguliwa na likiisha unakwenda kumuonyesha mwalimu anakupa jingine jipya.

Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na mashirika ya uchukuzi kila mkoa Mwanza ilikuwa KAUMA, Kagera ilikuwa KAGERA RETCO, Iringa ilikuwa IRINGA RETCO, Dodoma ilikuwa KAUDO, wadau mtaongezea.. Morogoro, Rukwa na kule kaskazini yalikuwa yanaitwaje..

Namkumbuka nakumbuka radio Tanzania ya enzi hizo na vipindi vyake kama Kahawa ni Mali, sikiliza Bwana Umeme, TTCL simu kwa Maendeleo, General Tyre, Starehe na BP, Malenga wetu.... wadau ongezeeni vipindi mlivyokuwa mnakumbuka enzi hizo...

Nakumbuka enzi hizo kulikuwa hakuna TV watu walikuwa wanakwenda kwenye kumbi za sinema tu kuangalia movies, Dar zilikuwepo kumbi kama Avalon,Drive Inn n.k Dodoma kulikuwa na N.K Disco Teques

Nakumbuka enzi hizo mabasi yalikuwa yakisafiri usiku tu na kulikuwa hakuna ajali nyingi kama sasa. Nakumbuka pia Mabasi maarufu enzi hizo kama SIRI YAKO, SUPER STAR, NGORIKA na wale mliokuwa Dodoma mtakumbuka mabasi yale ya kwenda Tanga kama SIMBA MTOTO, AMEET na zile honi zao kimadaha.

Nakumbuka pia watu walikuwa na ushirikiano sana, jirani alikuwa ni kama ndugu yako.

Mdau unakumbuka nini enzi hizo...??????

Mwenda Pole
Mdau wa Dodoma
 

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
9,961
Likes
419
Points
180

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
9,961 419 180
Dah mkuu unanitoa machozi, enzi za nmc watu waliiba sana mpaka wakaiita national millionaire company, nakumbuka miaka ya 80 nikiwa sumbawanga meneja wa nmc akiitwa chatanda mpaka akazuiliwa home kwake akituhumiwa ufisadi, Rtc karibu kila mkoa walikuwa na timu za mpira pale sumbawanga kulikuwa na timu mbili pinzani, ujenzi na rtc hawa rtc always wakiwachapa ujenzi. Rtc walikuwa na striker wao akiitwa mpambwe yule jamaa alikuwa akipiga ball si mchezo mpaka simba wakawa wanamnyemelea. Songea nako kulikuwa na timu ya rtc vilevile kuna watu watatu nawakumbuka mpaka leo, kuna striker akiitwa kidimbe jamaa alikuwa lethal vibaya mno, kuna beki ya kulia akiitwa ndumbaro na goalie akiitwa jordan, nilikuwa sikosi mazoezi yao pale ttc matogoro na mechi zao. Bora nishanunuliwa sana viatu na mdingi, nayapenda sana yale maisha ya miaka ya mwalim kweli wabongo tulikuwa km ndugu hakukuwa na tofauti ya maisha sana compared na sasa, mkuu post yako nzuri sana,
 

IronBroom

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2008
Messages
524
Likes
4
Points
35

IronBroom

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2008
524 4 35
Duh,mwendapole acha kabisa.Umenikumbusha mbali saaana.Nimekulia Dodoma.....this song(by Mbongo Love)reminds me of 'things' humo mkoani basi tuuu....by the way nilisoma chamwino shule ya msingi hapo dodoma mjini......

Those days:paradise Cinema,Dodoma Inn,NK Disco etc kwa upande wa soka tulikuwa na CDA Dodoma,Kurugenzi Dodoma,Waziri Mkuu Dodoma na....... dah!.....I really miss home mkuu.
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
8,790
Likes
842
Points
280

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
8,790 842 280
Hiyo nyimbo ya Maron Comandoz ikiwa inakaribia mwisho inatulia flani hv hala fu kuna jamaa anazungumzia ugumu wa maisha na shida zake, basi anasema
''ukitaka unga ni shida''
''ukitaka sukari ni shida''
''Ukitaka chumvi ni shida''

Halafu bendi nziiima wanaitikia...
''shiiiiiiidaaaaaaaaaaaaaa''

Basi unacharazwa mpini hapo balaa...
Solo la kufa mtu...
 

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,457
Likes
117,194
Points
280

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,457 117,194 280
Nyimbo hizi mimi zinanikumbusha Tanzania njema ambayo haikuwa na Viongozi wenye uroho wa utajiri wa haraka haraka na kuifisadi nchi kwa kushirikiana na wapiga debe wao, bali viongozi ambao siku zote waliweka mbele maslahi ya nchi mbele badala ya wao wenyewe.
 

Himawari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
2,234
Likes
733
Points
280

Himawari

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
2,234 733 280
Nakumbuka kipindi cha mama na mwana, ugua pole, katuni ya chakubanga kwenye gazeti la uhuru, sukari kwa foleni duka la kaya na ugali wa yanga (unga wa njano).
 
Joined
May 17, 2008
Messages
46
Likes
0
Points
0

jasaiji

Member
Joined May 17, 2008
46 0 0
Mwendapole umefanya vizuri kutufanya tukumbuke yale ya kale, katika mambo ya mpira kulikuwa na NMC, RTC, Maji kama ilivokuwa mikoa mingine kadhalika kulikuwa na Tmu za Town Stars ilokuwa chini ya Marehem Mkwanda pia Red Angles ilokuwa yamilikwa na Marehemu Vasta bila kusahau Tukuyu Star na Kurugenzi zote za Tukuyu. viwanja vilikuwa na enzi hizo uwanja wa mapinduzi na Magereza pale gereza la mahabusu Ruanda. ole mpira uende gerezani ilikuwa yachukua dakika kadhaa kuupata tena. kulikuwa na wachezaji akina Mtwawa kaparata, makwaza, marehemu Amiri Mwaruka, Pekosi, Kamana, Ababi. na alikuwepo jamaa mmoja mbabe alikuwa akiitwa Kaboso alikuwa mtu wa miraba minne. mabasi kulikua na Kwacha, Nyota, Mbembela, Amina bus, Mbibi, Ntahena, Relwe na Kamata kuondoka mbeya ilikuwa saa 4 asubuhi au saa 6 mchana then kufika Dar siku inayofuata saa 4 au saa 6 mchana.
 

saitama_kein

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Messages
982
Likes
1
Points
33

saitama_kein

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2009
982 1 33
Maroon Commandos kutoka Kenya - Charonyi ni wasi

Binafsi nakumbuka mbali sana enzi hizo radio zilikuwa ni National na Philips tu na zilikuwa zinauzwa kwenye maduka ya RTC.
Mkuu umenipeleka mbali sana wakati ule jamani!!! Tulikuwa na redio yetu National Panasonic "Nyeusi zile na wekundu wa kwa mbali na ilikuwa na redio na tape rekoda...ndefu kidogo" almaarufu sana miaka ya 80.....Pakatokea uvumi mitaa ya kwetu TBR eti uhujumi uchumi " Enzi za Sokoine" wanapita kila nyumba kukagua vitu vyote na kutaifisha...Masikini Mama yangu "Mwenyezi Mungu amrehemu" kwa ujinga na uwonga akajikuta anaifukia ardhini....ndo mwisho wa kutesa na vipindi vya Uncle J, Michezo saa 1.45.....
 

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
255
Likes
6
Points
35

Ntambaswala

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
255 6 35
Duu nimekumbuka mbali sana sana, pale RUVu JKT mwaka 1993 kulikuwa na radio ya kombania inapiga hiyo miziki wacha kabisa. Nakumbuka nyimbo kama JAckie wa Nico Zengekela, nyimbo za Hussein Jumbe akiwa New urafiki Jazz, Salna Brothers. Wakati huo kwenda Mtwara lazima upande basi la wifi nae pale kisutu au mabasi ya jamaa yake Ben Mkapa-aah Achimwene.
 

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
2
Points
35

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 2 35
Enzi hizo chama kimeshika hatamu, nakumbuka tukiwa shule ya msingi lazima mnaimba nyimbo kama vile, chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi, nyerere aah, ajenga nchi, karume aah, ajenga nchi! we acha tu jamani, sio sasa ambapo mafisadi wanajenga kwao!
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,296
Likes
37,962
Points
280

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,296 37,962 280
thread hii imenikumbusha mbali sana, asanteni wachangiaji kwa kuwa kila mnachokiongea kinakikumbusha kitu fulani cha siku za nyuma.
Sijui ni wapi huko ntaweza kupata kitabu cha darasa la pili la zamani cha Juma na Roza
 

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
3,851
Likes
25
Points
145

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
3,851 25 145
......Nimetoka kapa hapa, sikumbuki chochote.

pole sana nakumbuka tulikuwa tunaunga foleni duka la ushirka kupata sabuni,sukari n.k unakaa kwenye foleni ukichoka unaweka jiwe kwenye foleni then unatoka unaenda kivulini,maisha yalikuwa raha sana hata kondomu hazikuwepo.......lol.....
 

Forum statistics

Threads 1,191,696
Members 451,730
Posts 27,717,962