Kabla ya vyama vingi kuja Rais wa Zanzibar alikuwa moja kwa moja ni makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Vilipoanza vyama vingi ilibidi kubadili katiba tume ya Bomani (RIP) ikapendekeza kuwe na makamu wawili na wagombee pamoja uchaguzini na watoke chama kimoja.
Mapendekezo yakasema kwamba Rais wa Zanzibar asiwe tena makamu wa Rais kama ilivyokuwa.
CCM wakapokea mapendekezo hayo, wakayakubali na Julius Nyerere.
Lakini kumbe mapendekezo yale wana CCM wa Zanzibar hawakuyapenda. Sababu ni kwamba walitaka Rais wa Zanzibar aendelee kuwa Makamu wa Rais.
Wazanzibar walikasirika hadi wakashinikiza yasipitishwe na hayakupitishwa mwaka 1992.
Hatimaye Nyerere akakasirika hadi akaandika kitabu kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA.
Katika kitabu kile alisema mfumo wa Rais wa Zanzibar akiwa moja kwa moja makamu wa Rais hata kwa wakati ule ingeweza kuleta shida.
Kwamba kazi ya makamu wa Rais ni kwamba Rais akiondoka madarakani kwa sababu yoyote kama kifo au kujiuzulu au ugonjwa basi makamu wa Rais anachukua Urais.
Sasa tungeendelea na mtindo wa Rais wa Zanzibar kuwa makamu basi siku Rais wa muungano akifa au lolote basi huyu makamu na Rais wa Zanzibar anarithi Urais.
Nyerere akasema hilo lilikuwa ni tatizo kwa sababu Rais wa Zanzibar anachaguliwa na wazanzibar tu.
Sasa huyu akiwa Rais wa muungano wakati watanganyika hawakumchagua itakuwa tatizo.
Hoja hii ya Nyerere ndiyo ilisababisha wazanzibari wakubali kwa shingo upande, hata hivyo Salmin Amour aligoma kuhudhuria baraza la mawaziri hadi anaondoka madarakani.
Hivyo iko siku tutaona ukweli wa alichosema Nyerere. Iko siku Rais wa muungano ataweza kupata tatizo ikabidi makamu wa Rais achukue Urais ndipo wazanzibari wenye akili ngumu waelewe.
Jadili