Unakumbuka mapenzi ya sekondari? ...kipindi hamna simu za mkononi?

dah mkuu!

umenikumbusha kipindi nasoma! basi,kwanza nikiwa dalasa la nne(1983) kunarafiki yangu alimtongoza binti, wakaelewana akampa na pesa (505) basi bwana binti akaanza kuzingua jamaa akaandika barua ya vitisho kwa binti akisema "sofi kama hutaki kunipa ile yekudu(akimaanisha nyekundu) rudisha mia tano na tano yangu" halafu jamaa akaweka kwenye daltari la binti la hisabati! ticha wakati anasahihisha madaftari akaiona jamaa alikula njiti(viboko) mpaka akakojoa make ilikuwa msitarini jioni!
dah ila kwasasa jamaa alishaona na anamaisha poa na yule binti ni nesi!

kheeee mie choki kabisaaa, yaani darasa la nne mlishaanza kuhongana pesa, hiyo mwaka 1983 shs 505 ulikuwa ni mshahara wa mtu tena mwenye cheo cha kati! loh bila shaka huyo rafikio kwao walikuwa matajiri sana. miaka hiyo mi nilikuwa secondary schaool na niliwahi kusafiri toka Dar kwenda Iringa na basi la KWACHA kwa shs. 85/- mamangu alitupa kila mmoja shs 100 tulikata tiketi na pesa ikabaki ya kulakula njiani !
 
umeona eh?mlisumbuaga sana watu kabla ya simu.sa ivi mambo yamekuwa simpooooo kwa wanafunzi sasa ivi.

Hahahahhaaaaaaa
Nakumbuka kipindi nipo Olevel (Seminarini) nilikuwa ndio mwandikaji wa barua za washkaji kwa viburudisho - kisa mwandiko unaovutia. Pia nilikuwa na uwezo wa kuiga mwandiko wa kike.
Wakati flani nilimwandikia mshkaji barua kwenda kwa ampendaye, barua haikujibiwa mwezi mzima (shule zilikuwa majirani tu). Basi mshkaji alikuwa hana amani kabisa. Nikaamua kujibu kwa mwandiko uliotulia kama vile ni yule "manzi"(tulikuwa tunawaita hivyo) amejibu. Jibu lilikuwa ni +ve na anamkaribisha weekend waonane uwanjani kwenye mpira.
Guess what!
Mshkaji alijilipua kwa "jeans" ya kuazima yenye chata ya "Big Up" kwenye goti na tshirt ya "Chicago Bulls" kumtokea manzi. Yaliyojiri huko nilijutia kitendo changu maana mshkaji alitukanwa na manzi hadharani. Niliamua kumtafuta yule manzi na kumweleza ukweli akacheka sana ila nliwakutanisha na wakawa "friends" ndo nikamweleza mshkaji nlichofanya.
Hadi tunagraduate F4 walikuwa freeeeeeeeesh.
 
Hah haaa mdau we ulikuwa kiungo mzuri wa kuunganishia pasi wenzako.
 
kheeee mie choki kabisaaa, yaani darasa la nne mlishaanza kuhongana pesa, hiyo mwaka 1983 shs 505 ulikuwa ni mshahara wa mtu tena mwenye cheo cha kati! loh bila shaka huyo rafikio kwao walikuwa matajiri sana. miaka hiyo mi nilikuwa secondary schaool na niliwahi kusafiri toka Dar kwenda Iringa na basi la KWACHA kwa shs. 85/- mamangu alitupa kila mmoja shs 100 tulikata tiketi na pesa ikabaki ya kulakula njiani !

Nadhani mdau hapa alikosea kuandika, eidha kiwango cha hela alichohonga huyo binti, au mwaka wa masomo, labda ilikuwa mwaka 1993.
 
Huu mchezo nimekuja kuucheza nikiwa Advance, O level nilikua boya boya dizain enzi hizo Tanga tech pale kuna watoto wa kifungilo wakajipendekeza eti wanataka penpals wakaandika majina yao kama kumi hivi na location pia ili tuwasiliane kisha kama vip likizo tuweze kuonana coz wote walikua wanatoka dar...basi bana barua ikafika bwenini (chui domitory) wazee tukajinyakulia majina kila mtu lake kuna jina moja lilikua limekaa kishari shari 'ASHA' kila mtu akawa analikwepa akihisi atakua asha ngedere mcharuko kumbe ndo mzuri kuliko wote, ofcoz me nilichukua hilo jina coz nilichelewa nikakuta majina mazuri mazuri yote wameshayawahi wadau...tukaanza kutumiana na kupokea barua...nakumbuka ule upuuzi eti unaandika kwanza barua kwenye rafu afu ndo unakuja kuiandika vizuri kwenye karatasi zetu zile za kimahaba maua maua nini dizain fresh...basi bana twende na kwenda school kwao kuaanza unoko barua ikifika na kuhisiwa ya malavi davi inasomwa assembly wazee tusiokubali kushindwa tukabuni mbinu ya ki scolfied kila herufi tukaipa symbol kwa mfano A=x, B=j, C=u nk so kama nimeandika 'sdaenfdhbgn' unakuta inamaanisha 'hello baby i missed u' nk, so unakuta barua nzima imeandikwa katika mfumo wa 'djfhsbshwhfhbf' huku kila herufi ikiwa na maana yake na kuiandika ilikua inagharimu almost hata siku mbili...unautuma mzigo hata akiikamata huyo mwalimu wao bado haelewi umeandika nini na dem nae anatumia kama siku mbili hivi kuisoma hadi kuimaliza...ujio wa facebook simu za mkononi kwa wingi umerahisisha sana maisha...nakumbuka unasimama assembly barua zainaitwa yako isipoitwa unahisi ka umepata supplementary core subject...kweli maisha yanachange fasta

Kweli wengi wamepitia vituko vyao. Sasa mlikuwa mnafumbuaje hilo fumbo la barua?
 
Kuna rafiki yangu alikuwa na demu tukiwa primary. Tulivyomaliza shule yule demu akaenda kusoma Mbeya. Mi nikabaki nasoma day na rafiki yangu akaenda bweni huko Mbagala.

Tukiwa likizo rafiki yangu akaniomba nimusindikize akamuone demu wake. Hakuna cha simu wala barua. Na nyumbani kwao yule demu wazazi wake walikuwa wanoko sana. Tulipanga tuende siku ya katikati ya wiki tena mchana. Siku ikafika.. Tukagonga geti akafungua mama yake yule demu, kumbe alikuwa likizo. Maswali yakaanza. Eeh! Karibuni mnashida gani, rafiki yangu akajibu, sisi rafiki zake Emmy. Mama akauliza swali la pili, mlisoma naye??
Tukajibu tunasoma naye. Yule mama akashanga. Kwan kumbe Emmy alikuwa nasoma shule ya Wasichana, alitufukuza na mbwa. Tulirudi kwa aibu tangu siku hiyo sikutaka kumuona Emmy.
 
Duu hii kali lakini nina mashaka kidogo "KEY" ya kufafanua maneno ilisafirishwaje baina ya hivo pande mbili (nitoe shaka kaka)
 
Kuna rafiki yangu alikuwa na demu tukiwa primary. Tulivyomaliza shule yule demu akaenda kusoma Mbeya. Mi nikabaki nasoma day na rafiki yangu akaenda bweni huko Mbagala.

Tukiwa likizo rafiki yangu akaniomba nimusindikize akamuone demu wake. Hakuna cha simu wala barua. Na nyumbani kwao yule demu wazazi wake walikuwa wanoko sana. Tulipanga tuende siku ya katikati ya wiki tena mchana. Siku ikafika.. Tukagonga geti akafungua mama yake yule demu, kumbe alikuwa likizo. Maswali yakaanza. Eeh! Karibuni mnashida gani, rafiki yangu akajibu, sisi rafiki zake Emmy. Mama akauliza swali la pili, mlisoma naye??
Tukajibu tunasoma naye. Yule mama akashanga. Kwan kumbe Emmy alikuwa nasoma shule ya Wasichana, alitufukuza na mbwa. Tulirudi kwa aibu tangu siku hiyo sikutaka kumuona Emmy.
HAh hah,mliumbuka kweupe, Emmy Yuki wapi sasa hivi?
 
Back
Top Bottom