Unakula nini kupunguza kasi ya kuzeeka haraka?

kiboboso

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
8,151
2,000
Ukilenga kula vizuri kwa ajili ya afya, mambo mengine yatakaa sawa yenyewe.
Binafsi sihofii sana uzee, ila maradhi yanayoweza kusababishwa na kula vibaya.

Kwanza, nna ratiba mbovu ya kula. Naweza nisile siku nzima nikapata korosho na chai au maji tu

Mara nyingi napenda asubuhi nikiweza nipate chai sio nzito sana ( chai isiyo na sukari au iwepo kwa mbali na mkate, ikienda na korosho au karanga) ili mchana niwe na ham ya chakula ( hapa napendelea wali maharage na mbogamboga bila kukosa juice).
Nikipiga hivyo usiku siwezi kula tena, itakua maji au matunda.

Kwa ufupi napunguza sana nyama na milo mizito. Nisipokula mchana, jioni ntapenda supu ya kuku au mchemsho wa ulimi wa ngombe.

Tatizo lipo kwenye ratiba mbovu ya kulala na kula, nachelewa kulala na hii imekua ni mazoea. Naweza kukaa siku tatu nakunywa maji tu.
Hapo kwenye supu ya ulimi wa ng'ombe mkuu una roho ngumu kinoma.
 

mazojms

JF-Expert Member
Sep 22, 2017
1,528
2,000
Kwa mimi ukiacha chakula naamini uzee ni lifestyle.
Kuna watu wanakula vizuri tu hawajanenepeana lakini ukiwaangalia maisha yao utasema wamekuzidi miaka kumbe umewazidi pakutosha.

Siri ya kuu ya kutokuzeeka ni kujipenda. Vaa vizuri upendeze, toka jichanganye na watu, kataa stress.
Kabisa! kufikiria namna ya kutozeeka mapema ni stress tosha kukufanya uzeeke mapema zaidi
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
29,541
2,000
Kula nyagi, gonga gambe, kata -vant bana, life's too short you know....
Sinyie ndio mnasema beer tam, ama...😕
 

Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
275
1,000
View attachment 2030898

Hili swali linaweza kuzua shauku, lakini pengine likawa chachu ya kufahamu pia kuwa uzee au kuzeeka ni suala la chakula tunachokula.

Tukiweka kando maumbile na mambo ya jenetiksi kwa baadhi ya watu waliobarikiwa, kwa asilimia kubwa mtindo wa maisha ambao unahusisha vyakula tunavyokula unaweza kukufanya ukazeeka haraka au ukachelewa kuzeeka.

Sasa tujuzane, umri wako na mwenendo wa mwili/akili/hisia vinaenda sambamba? Je, unajihisi unakua kijana zaidi au unapata hofu ya umri kukutupa mkono? Unajisikiaje?

Kama unajihisi kuzidi kuwa kijana, basi huu ni uwanja rasmi wa kutueleza unakula nini au unafanyaje kupunguza kasi ya kuzeeka haraka.

Karibuni kwa mjadala.
Acha woga kuzeeka si ugonjwa! Kula chakula moyo unapenda ili mradi uwezo unaruhusu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom