Unakubaliana vipi au unamkatalia vipi Bingwa wa Vikao vya Misiba Tanzania nzima Steve Nyerere kwa hii Kauli yake?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,877
Kwamba Tanzania nzima kwa sasa ' Mastaa ' wapo Saba ( 7 ) ambao ni:

1. Rais Dkt. Magufuli
2. Makamu wa Rais Samia Suluhu
3. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
4. Spika wa Bunge Job Ndugai
5. Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma
6. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
7. Yeye mwenyewe Steve Nyerere


Nawasilisha.
 
umefikiri nini mkuu kutushushia hii

Natamani ungekuwa unamuona Mhusika Steve Nyerere ' Mubashara ' akiwa anajifaragua kwa mikogo yake wakati anasema na anayataja hayo Majina. Tena hadi mwisho akamalizia kwa kusema kuwa ukiona Mtu mwingine zaidi ya Wao Saba ( 7 ) anasema ni Maarufu basi jua ni Muongo na Uwongo mtupu.

Steve Nyerere ni Mtu wa Vituko Vituko sana na kila nikikumbuka Vituko alivyokuwa akivifanya pale Leaders Club mwaka 2012 wakati wa ' Concert ' la Bendi yangu pendwa ya Wenge Musica BCBG chini yake JB Mpiana ilipokuja huku tukiwa na Mtu ambaye ndiyo anamuwezea mno aitwae Haji Londa na Ben Kinyaiya huwa nacheka na nashangaa ni kwanini Steve Nyerere hajapenda au hataki kuwa ' Comedian ' kama akina Joti kwani ana ' Vituko ' ambavyo hata Joti mwenyewe hana.
 
Msiba ndo kitu maarufu zaidi duniani kwahyo kajamaa kapo sahihi kutumia hiyo fursa kuwa maarufu na ki protocol hiyo list kameipanga vizuri sana bila kukosea
 
Back
Top Bottom