Unakerwa na nini kwenye mabasi yaendeayo mikoani?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kwenye safari kwa sisi ambao bado tunatumia usafiri wa Umma, kuna kero mbili ambazo zinatukabili wasafiri. La kwanza ni ukosefu wa vyoo kwenye njia tunazotumia kusafiria matokeo yake hujisaidia maporini kwa mtindo wa kuchimba dawa. Kwa kweli hii staili inakera ingawa kwa wengine huwa ni kama faraja kwao kwani huitumia kwa kunyoosha miguu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukaa muda mrefu wakiwa wamekunja miguu!!

Kero nyingine ni ya hawa abiria wenzetu ambao wanapenda kula kula lakini hawana uwezo wa kuhimili misuko suko ya safari matokeo yake huishia kutapika garini wakati safari inaendelea. Unakerwa na nini unaposafiri na mabasi yaendayo mikoani??
 
Harufu mbaya za vikwapa, harufu za uvundo uvundo ambao hata sijui ni wa nini, mavumbi, uchakavu wa mabasi, na tabia ya baadhi ya watumishi wa hayo mabasi kuuza ama kupangia siti moja kwa zaidi ya mtu mmoja.
 
Nakereka sana nikikaa siti moja na mwanaume mwenzangu au mmama/mbibi!!!
Napataga faraja sana nikikaa na dada duu!!
 
Harufu mbaya za vikwapa, harufu za uvundo uvundo ambao hata sijui ni wa nini, mavumbi, uchakavu wa mabasi, na tabia ya baadhi ya watumishi wa hayo mabasi kuuza ama kupangia siti moja kwa zaidi ya mtu mmoja.
Mkuu hapa niko kwenye basi jamaa jirani kikwapa kinatema kama beberu!na ndio kwanza mafinga naelekea songea!kingine haya mabwasi kama movie si ya majuto basi itakuwa kingwendu daily
 
Mkuu hapa niko kwenye basi jamaa jirani kikwapa kinatema kama beberu!na ndio kwanza mafinga naelekea songea!kingine haya mabwasi kama movie si ya majuto basi itakuwa kingwendu daily
Hapo kwenye movie tuko pamoja!! Kuna baadhi ya mgari utadhani wameloglezewa movie za Kanumba January to December wao na "The great"!
 
me nakereka na uchafu wa mabasi, utakuta basi chafu mpaka kuna mende. si ajabu hata kunguni na chawa wakawemo. suala la mikanda ndo kabisa, wenye mabasi wengi hawazingatii usalama wa abiria. wao wanajali pesa tu. . .
 
Ukikaa siti za nyuma kulazimishwa kwenda mbele mnapofika kwenye mizani ili basi lisionekane limezidisha uzito.
 
me nakereka na uchafu wa mabasi, utakuta basi chafu mpaka kuna mende. si ajabu hata kunguni na chawa wakawemo. suala la mikanda ndo kabisa, wenye mabasi wengi hawazingatii usalama wa abiria. wao wanajali pesa tu. . .
Yaani mabasi mengine utafikiri jalala! Hata lile tangazo linalosema kwamba mbu wa Maleria huambukiza usiku wa manane naona watengenezaji wake hawajaingia kwenye haya mabasi, maana wakati mwingine unakutana na mbu kibao!!
 
Acheni kupanda mabasi jamani, pandeni ungo kama mimi. Mkitaka wasilianeni na wakati ndio sasa na Katavi mzee wa Lyamba lya mfipa, kule kule kulikoungua shoka mpini ukabaki.
 
Last edited by a moderator:
Nakerwa na hizo movie zao wanaziita za Bongo movie, nyingi hazijali mazingira.
Nyimbo za Bongo Fleva za kurudia rudia, hususani za mapenzi tu (nakerwa na nyimbo za mapenzi).
Baadhi ya magari kutokuwa na mapazia kwani mtu anaungua na jua ile mbaya.
Watu kupiga/kupokea simu kwa makelele.
Wasafiri, hususani wanaume, kunywa pombe kali na kukoroma + kutoa harufu ya pombe.
 
Back
Top Bottom