Unakemea ubaguzi wa kikabila Rorya halafu wewe unabagua majimbo ya wapinzani

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Amani iwe kwenu wakuu!

Jana mgombea kiti cha Urais kupitia CCM akiwa Musoma mkoani Mara alionya vikali UKABILA ndani ya jimbo la Rorya akidai kwamba Waluo hawataki kuchagua Wasuba na kwamba mara zote Wabunge wametokea upande wa Waluo.

Ukweli ni kwamba hayo madai si kweli hata kidogo kwa mujibu wa wakaazi wa Rorya. Kama kabila la mtu linatambulishwa na lugha anayoiongea basi madai ya mgombea huyu ni kweli ila kama lugha ya mtu haimaanishi kabila lake basi suala hili ni uongo mtupu

Mfano kabla ya mbunge mstaafu Oyombe Aila mbunge alikuwa MSUBA akitokea Tarafa ya SUBA, baada ya hapo mbunge akawa Oyombe Aila (Mluo) akitokea kowaki Tarafa ya Luo imbo, baada yake mwaka 1995-2000 mbunge akawa Mabere Marando (Msuba/Mrieri) akitokea kata ya Nyambori, miaka kumi iliyofuata mbunge akawa Prof Sarungi ( Msuba/ Mtegi) wa Tarafa ya Girango na kufuatiwa na Lameck Okambo Airo (Msuba/Mtegi) wa Girango kwasasa mgombea wa ccm ni Msuba wa Tarafa ya SUBA na wa chadema ni Wenje ambaye huenda naye ni Msuba wa shirati au mluo.

Kinachochanganya watu na kilichomchanganya mheshimiwa mgombea ni Lugha. Ukweli ni kwamba kijaluo kinaongelewa na makabila karibia yote yanayoishi Rorya na kwasasa hata Wakurya wa Tarime wanajua kijaluo tena si rahisi umseme asikuelewe. Babu yake Sarungi au Airo huenda hawakujua kabisa kijaluo enzi zao ila baada ya ujio wa waluo lugha yao ilimezwa.

Akina Sarungi na Airo ni wasuba kabisa kama alivyo mgombea wa ccm isipokuwa wao walimezwa kabisa tofauti na wasuba wa karibu na Musoma na sababu hasa ni kwamba Hawa wemetengwa na mto Mori kwa upande moja, Mlima Rorya kwa upande mwingine pamoja na ziwa Victoria upande wa Musoma ndiyo maana lugha yao imeendelea kubaki hai ila mpaka muda huu naandika ukienda KIBUYE, KINESI ,NYAMAGUKU na mialo yao wasuba wanaongea kijaluo kama kawaida. mgombea wa CCM hajui tu kijaluo kwasababu hakukulia huko. Mimi ninayeandika hapa wazazi wangu ni watu wa Masasi mtwara wakifanya kazi Rorya lakini huwezi kunisema kwa kiluo.

Kule Rorya kuna wasukuma ,kuna wakurya na makabila mengine ila wamesahau lugha zao kabisa na kama wanazijuia hawaziongei kabisa maana wamemezwa na waluo. Kwa utafiti wangu waluo Rorya ni jamii ya watu wachache sana na wengi wako luo imbo (kowaki na buturi), kamageta na bugire (Girango) na kakseru (Nyancha). Hawa walikuwa hawatahiriwi kabisa ( kwasasa kidogo wemeanza tohara) pili walikuwa wanatolewa meno mbili za mbele .

Wasuba wa Utegi (wategi), wakine , warieri, waregi na wasuba wengine walisahau lugha zao kitambo na wote wanaongea kiluo

Lakini tukubaliane kuwa waluo ni wakabila na hawataki kuwachagua wasuba kwenye ubunge kwani ubaguzi wa kikabila na ubaguzi wa kivyama vina utofauti gani?. Kusema huwezi kumchgua mtu kwasababu si kabila lako na mwingine akasema siwezi kuleta maji au barabara hapa kwasababu hamkumchagua mtu wa upinzani utofauti uko wapi, jibu ni kwamba wote ni wabaguzi na wote hamfai. Mwl Nyerere alisema ubaguzi ni sawa na kula nyama za watu ukiacha hauachi.

Kama tukiamua kuchukia ubaguzi basi tuchukie ubaguzi wa kila aina, ubaguzi wa kikabila, kidini na kivyama yote ni ubaguzi bila kujali yanafanywa na nani. Tuishi yale tunayoyahubiri jamani.

Kindikwili.
 
In short ni kuwa Meko kachanganyikiwa. Haamini jinsi alivyopoteza ushawishi kwa watanzania
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
In short ni kuwa Meko kachanganyikiwa. Haamini jinsi alivyopoteza ushawishi kwa watanzania
Miaka mitano anaongea pekee tu akajua ameshaua upinzani akanunua wabunge sasa haamini anachokiona mbele yake
 
Back
Top Bottom