Akikuuliza unajua unaongea na nani nawew mwambie kwani mimi nani.... hatokuelewa atabaki anaduwaa
Aisee usinikumbushe...kuna siku nilikua bar moja kule kigamboni kuna jamaa akaja akawa anaongea ovyo, nikajifanya kumwambia aongee taratibu tunaangali mpira....jamaa akaniuliza kama namjua yeye ni nani, mimi si nikamjibu mbovu...yalaa, nilichezea kichapo, na msamaa nikamuomba. Kumbe jamaa ni mjeshi tena mwenye vyeo.
Kuna hii tabia ya watu kuingia kwenye maofisi ya watu, hawataki kufuata utaratibu ukimuuliza anakwambia unajua unaongea na nani.
Hii tabia inanikumbusha aliyewahi kuwa Waziri wa nishati na madini, siku alipoingia kwenye ATM na kuanza kuongea na simu muda mrefu yule mlinzi alipomfuata "jamaa" akampiga makofi.
Tukio lingine ni aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa mambo ya ndani na hivi majuzi amejiuzulua akiwa Waziri wa Maliasili, huyu jamaa alipita maeneo ya Kijitonyama akiwa kwenye gari linaloendeshwa na dereva wake, walipokuta foleni ikabidi "watanue" askari wa kike alipowasimamisha akajibiwa "unajua unaongea na nani" kisha baada ya hapo yaliyomkuta huyo askari anajua Mungu mawazo yangu kama we ni nani au ni nani unaeshimu taratibu na pia ueshimu kazi za watu bila kujali cheo.
Mungu ni mkubwa hao wote niliowataja walisitisha au kusitishiwa ajira zao baada ya kashfa kwa sasa kuna "jamaa" fulani ambaye ki cheo ni Waziri huyu "jamaa" huwa anakuja sana ofisini kwetu akifika hasalimii watu pale mapokezi ye huingia tu kule back office ambako kuna boss wetu rafiki yake sasa juzi nilifurahi kwa sababu ofisini pale kwenye corridor kulikuwa kumefanyiwa fumigation.
Mheshimiwa alirudi mbio huyo wenzetu wenye vyeo acheni tabia hizi ni za kishamba.
Akikuuliza unajua unaongea na nani mjibu naongea na tone la manii
kuna waziri anaitwa Dr Tizeba jamani Mungu anisamehe huyu jamaa kwakweli mimi ni jirani yangu kwa maana tunatoka kijiji kimoja huko jimboni kwake lakini jamaa ukimpigia cm kwanza hapokei na hata ukituma meseji hawezi kujibu,cm yake iko hewani lakini hata ukipiga kwa nyakati tofautitofauti hapokei, na mara zote anadhani labda unataka kumpiga bomu kwa maana ya kumwomba msaada wakati unataka kumpatia shida za wananchi. Mfano mwaka jana nilikwenda jimboni kwake nikakuta njaa hatari mihogo inaugonjwa kwa takribani mwaka na hakuna msaidizi,nilijitahidi kwenda wilayani kwa DALDO lakini sikupata msaada,nikampigia simu mbunge hakupokea nikamtumia sms kama sita hivi hakujibu nikampigia mdogo wake naye kiburi hakupokea ,HALI HII YA KUJIONA VICHWA KAKA YAKE MBUNGE ALIAMUA KUJITOA CCM NA KUHAMIA CHADEMA akiwa diwani coz hasikilizwi na mbunge, 2015..........KAZI ANAYO......CCM HESABUNI MAUMIVU BUCHOSA mbunge labda kama atajirekebisha kupita watu bila salaam na kulazimi ferry kumsubili jioni nyakarilo hata kama yuko mwanza anakuja eti coz ni mbunge hiyo hata kidogo ni utemi wa ajabu..........hudumia watu utawajua..........
Hakuna kauli nisiyoipenda kama hii... mtu wa aina hii akiingia kwenye anga zangu is nobody to me, cheo chake anakiacha ofisini kwake....