Unajua unaongea na nani?

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
2,000
Kuna hii tabia ya watu kuingia kwenye maofisi ya watu, hawataki kufuata utaratibu ukimuuliza anakwambia unajua unaongea na nani.

Hii tabia inanikumbusha aliyewahi kuwa Waziri wa nishati na madini, siku alipoingia kwenye ATM na kuanza kuongea na simu muda mrefu yule mlinzi alipomfuata "jamaa" akampiga makofi.

Tukio lingine ni aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa mambo ya ndani na hivi majuzi amejiuzulua akiwa Waziri wa Maliasili, huyu jamaa alipita maeneo ya Kijitonyama akiwa kwenye gari linaloendeshwa na dereva wake, walipokuta foleni ikabidi "watanue" askari wa kike alipowasimamisha akajibiwa "unajua unaongea na nani" kisha baada ya hapo yaliyomkuta huyo askari anajua Mungu mawazo yangu kama we ni nani au ni nani unaeshimu taratibu na pia ueshimu kazi za watu bila kujali cheo.

Mungu ni mkubwa hao wote niliowataja walisitisha au kusitishiwa ajira zao baada ya kashfa kwa sasa kuna "jamaa" fulani ambaye ki cheo ni Waziri huyu "jamaa" huwa anakuja sana ofisini kwetu akifika hasalimii watu pale mapokezi ye huingia tu kule back office ambako kuna boss wetu rafiki yake sasa juzi nilifurahi kwa sababu ofisini pale kwenye corridor kulikuwa kumefanyiwa fumigation.

Mheshimiwa alirudi mbio huyo wenzetu wenye vyeo acheni tabia hizi ni za kishamba.
 

foshizzle

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
374
0
Yule aluyekua waziri wa afya sijui ndo anaitwa ponda alienda psi alipofika mapokezi akataka aende moja kwa moja kwa boss. Yule dada akamwambia subiri nipige simu kumuuliza unaenda kumuona kama ana nafasi. Akamwambia usipige simu kwani unajua unaongea na nani niangalie. Yule dada kwamwangalia kamwambia sikufahamu, jamaa kasema wewe mtanzania wa wapi yaani hunijui mimi ponda??..yule dada mawazo yakampeleka kwa mponda yule alopigwa risasi morogoro. Akasema eti kumbe ndo wewe pole sana unaendeleaje? Jamaa alikosa jibu.
 

Eddy Love

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
13,140
2,000
Yule aluyekua waziri wa afya sijui ndo anaitwa ponda alienda psi alipofika mapokezi akataka aende moja kwa moja kwa boss. Yule dada akamwambia subiri nipige simu kumuuliza unaenda kumuona kama ana nafasi. Akamwambia usipige simu kwani unajua unaongea na nani niangalie. Yule dada kwamwangalia kamwambia sikufahamu, jamaa kasema wewe mtanzania wa wapi yaani hunijui mimi ponda??..yule dada mawazo yakampeleka kwa mponda yule alopigwa risasi morogoro. Akasema eti kumbe ndo wewe pole sana unaendeleaje? Jamaa alikosa jibu.

ha ha ha ha ha hii kali kuliko zote
 

Kozo Okamoto

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
3,392
1,500
ni kweli mkuu,kuna watu wana dharau kinyama,kuna siku katibu mkuu wa ccm alikuja ofisini kwetu akaniuliza hivyo hivyo baada ya kumwambia afuate taratibu,kaniuliza "kwani hunijui?"nikamwambia sikujui labda nimuite bosi wangu akutambulishe kama anakujua.alinyamaza kimya na kufuata taratibu kama inavyotakiwa.
 

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
773
195
Cheo ni dhamana! Mtaje huyo waziri asiye na maadili ya kitanzania/kiafrika ya kusalimiana hata tupishanapo barabani, ili tumpe mbofu mbofu zake live bila chenga kupitia jamvini JF.
 

kimpe

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
895
1,000
Daah nakumbuka kuna kipindi nilimpeleka dogo shule alikuwa anaenda kuanza kidato cha kwanza nimemshika mkono njuka wangu tunelekea kwa cashier kulipa vimichango foleni ilikuwa ndefu kipindi hicho hamna kulipia bank bado watu wawili nifike dirishani akatokea jamaa mmoja kumbe ni mwalimu wa shule ileile akapitiliza moja kwa moja dirishani nikamuuliza vp mbona hufati utaratibu akanijibu mimi ni mwalimu wa hapa natakiwa nilipe kwa haraka ili nikamfundishe huyo mwanao sikumchelewesha nikampa kubwa hapo hapo nikamwambia kama wewe ni mwalimu wa hapa sisi ndo tumeleta mshahara wako unaweza fundisha bila mshahara wewe akawa mdogo ticha ikabidi aombe radhi.........nilipofika dirishani cashier akanambia umefanya vizuri mana huyo mwalimu anachukua pesa za watu waliopo nyuma anaowafahamu anakuja kuwalipia bila utaratibu.........wenye vitabia hivi wapo wengi ila tatizo wafanyakazi wengine wakimuona mtu maarufu wanaanza kupapatika umashuhuri ofisini kwake na kwa mkewe kwengine ni utaratibu tu
 

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,540
1,225
^^
Kuna watu vyeo vinawapa shida sana!
Yuko radhi aue hata mzazi wake ili apate dawa ya kuabudiwa.
Mwenye stahili ya utukufu ni Mungu.
^^
 

nameless girl

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
4,153
2,000
Hakuna kauli nisiyoipenda kama hii... mtu wa aina hii akiingia kwenye anga zangu is nobody to me, cheo chake anakiacha ofisini kwake....
 

Ablessed

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
4,616
2,000
Kiburi cha madaraka ni cancer kwa jamii. Kuna watu wakiwa na madaraka utafikiri wamepewa nafac ya kuongoza ulimwengu wanasahau kuwa cheo ni dhamana wakati wowote unaweza kayapoteza hayo madaraka na kuwa mtu wa kawaida.
 

gwakipanga

JF-Expert Member
Dec 1, 2011
626
250
Mimi mtu akiniuliza unajua unaongea na nani? Hua na jibu sitaji kujua naongea na nani? Ila ninachoitaji muda huu, ni utaratibu ufuatwe.
 

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,031
2,000
Akikuuliza unajua unaongea na nani nawew mwambie kwani mimi nani.... hatokuelewa atabaki anaduwaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom