kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Tulimsikia Rais Samia akitoa mfano wa Zanzibar wa kuruhusu wasichana wanaopata mimba kurudi kuendelea na elimu ya sekondari kwenye shule za umma.
Lakini ambacho hakutaka kusema ni ufaulu hafifu wa muda mrefu wa Zanzibar kwenye mitihani ya kufuzu elimu ya sekondari. Ilifikia hatua hadi kudai kuna kuihujumu Zanzibar huko NECTA.
Lakini mungefanya utafiti nina hakika mungekuta kuwasomesha watoto wazazi kunapelekea wao kushindwa kufanya vizuri kwa kua wametangulizwa kwenye mambo ya mapenzi na uzazi kabla ya muda wao kwenye maisha.
Badala ya kuleta utaratibu huo bara nadhani huko Zanzibar ndio kuna tatizo halifai kuigwa.
Katika mambo tunakosea ni hili la kutaka kuwachanganya watoto wa kike wazazi katika shule za kawaida za umma.
Kwanini hatujaangalia nchi zingine zinafanya vipi? Maana hata hizo nchi zinazowachochea hao wapiga debe wa suala hili nchini kwao watoto wazazi hawasomi shule za umma wakishakua wazazi.