Unajua ni kwa nini mara ya kwanza na pekee hadi sasa Taifa Stars ilicheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika?

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,636
8,774
Mara ya kwanza na pekee hadi leo Taifa Stars kucheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (kipindi hicho yakijulikana kama Kombue la Mataifa Huru ya Afrika) ilikuwa ni mwaka 1980. Kipindi hicho kulikuwa na mashindano makubwa matatu ya soka nchini:
1. Ligi kuu
Ilichezwa kwa mtindo huu:
Kutafuta Bingwa wa Wilaya (timu za kata kwenye wilaya husika zilicheza kupata bingwa wa wilaya; baada ya bingwa kupatikana wachezaji walioonyesha kiwangonbora kutoka timu zilizoshindwa walikuwa huru kujumuishwa kwenye timu bingwa).

Kutafuta Bingwa wa Mkoa (klabu bingwa za wilaya kwenye mkoa husika zilichuana kupata bingwa wa mkoa. Bingwa wa mkoa pia alikuwa na hiari ya kuimarisha kikosi chake kutoka kwenye timu zilizoshindwa kwenye msimu husika)

Kutafuta Bingwa wa Kanda. (Mikoa kadhaa iliunda kanda moja, na mabingwa wa mikoa husika walicheza kutafuta bingwa wa kanda).

Kutafuta Bingwa wa Taifa (mabingwa wa kanda walicheza kwenye kituo kimoja kwa mfumo wa ligi na aliepata points nyingi ndie aliekuwa klabu bingwa wa Tanzania.

Kombe la Taifa
Kila mkoa uliunda timu (kutokana na wachezaji wazawa wa mkoa husika; mtindo wa mtoano ulitumika na kocha wa timu ya Taifa aliyatumia mashindano haya kuteua wachezaji wa Taifa Stars)

UMISETA
Mashindano ya shule za sekondari (kuanzia wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa). Kombaini ya UMISETA Taifa ilicheza na kombaini ya shule za sekondari za Zambia. Ndipo kina Kalusha Bwalya walipojulikana.

Mfumo huu ulikuwa rahisi kuuendesha na timu hazikuwa na ulazima wa kuuza mechi kwa kuwa gharama za uendeshaji hazikuwa kubwa.

TFF rudisheni mfumo huo. Ushahidi ni kuwa tangu tuachane na mfumo huo Taifa Stars imekuwa kichwa cha mwendawazimu. Brazil haina mfumo wa home and away pia. Tusiwaige Waingereza na vinchi vingine vya Ulaya ambavyo:
(a) eneo ni dogo kwa hiyo timu kusafiri upande mmoja kwenda mwingine hauchukui muda mrefu hata kuathiri performance ya wachezaji
(b) miundo mbinu yao na sponsorships ni more advanced.
I rest my case.
 
Umepoteza nguvu nyingi kuelezea hadithi za kale zisizoendana na wakati uliopo,wakati uliopo uimara wa Timu za Taifa unategemea Sana idadi na viwango vya wachezaji wa kimataifa ulionao na wala si ubora wa ligi ya ndani,na wakati uliopo utatengeneza wachezaji wa kimataifa wa kulipwa wanaocheza sehemu mbalimbali duniani kwa kuwa na mfumo wa kuandaa vijana wangali wadogo kucheza football yaani Football Academy

Hata hivyo tunakushukuru kwa kuleta habari toka jumba la makumbusho,acha zibaki kama historia.

Niwie radhi nimetumia lugha yenye kukera kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Korea Kaskazini ina wachezaji wangapi wanaocheza nje ya nchi yao? By the way; hujaelewa msingi wa kile nilichoandika.
 
Korea Kaskazini ina wachezaji wangapi wanaocheza nje ya nchi yao? By the way; hujaelewa msingi wa kile nilichoandika.
. Kwani Wana Nini cha maana? Kufuzu kwao Ni kutokuwa na wababe kwenye bara lao
 
I was referring to financing model and not field tactics. Kwa mtazamo huo hujaelewa kitu.
Unaandika sentensi 200 zinaelezea mfumo wa ligi wa ki primitive unaoanzia ngazi ya wilaya kisha unasema sentensi moja kuzungumzia unafuu wa kifedha then unasema I was referring to Financial Model unajielewa kweli wewe??Ulimwengu wa Leo nani anayeendelea kwa mipango ya gharama nafuu??Nasisitiza unawaza kizamani sana,mawazo yako yanastahili kuwekwa ktk jumba la makumbusho.

BTW, mfumo wa kombe la FA yaani Azam Sports Confederation Cup unakidhi mahitaji unayotaka hivyo hakuna haja ya Tanzania Premier League kuchezwa kimwaka 1965

Kama umeshindwa kuelewa concept iliyopo kwenye post yangu sio kosa langu. Maybe it requires too much of efforts on your limited intellectual capacity to perceive it. Kuwa na tatizo la uelewa by itself sio dhambi, lakini ni a very serious mental problem kulazimisha tafsiri yako (itokanayo na perception yako ambayo ni limited by a number of factors) kwenye post ambayo hukuiandika, ukashindwa hata kupokea ufafanuzi (simply tu kwa kuwa huelewi).

Btw; hii concept yako kuwa mfumo aghali ambao hauna adequate financial backing ni more appropriate kuliko ule ambao ni efficient ni unbelievably ridiculous.
 
Back
Top Bottom