Unajua 'stress' ni nini?

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
3,211
988
Chanzo cha stress na madhara yake mwilini

Hali ya mfadhaiko inasemwa kutokea wakati ubongo unapokabiliana na tatizo la mvurugiko wa akili na kujikuta ukishindwa kuendana na hali zingine zinazohitaji umakini kwa wakati mmoja. Jambo hili linaweza kuuteka ubongo na kudhoofisha uwezo wake. Hatimaye hali hii ya ufadhaikaji katika ubongo inaweza kutengeneza dalili tofauti ambazo zimepachikwa majina mengi kwa mjibu wa sampuli tabia za nje anazozionesha mtu.

Idadi kubwa zaidi ya watu wanazidi kupatwa au wanategemewa kupatwa na aina fulani fulani za mifadhaiko. Baadhi ya aina za mifadhaiko ni hali za asili katika hatua za maendeleo na kukua kwa mtu. Ni katika hali hizi za matumizi ya akili ambamo silika ya mtu hujengwa na uhodari wake wa ndani huhamasishwa. Kwa asili, kushughurika na hali hasi za mawazo ya mtu ni jambo la lazima katika mlolongo wa mambo. Kwa sehemu kubwa hali ya mfadhaiko ni hali ya mpito ikiwa upendo, kujaliana na kutambuana vinapatikana kumwelekeza mwingine katika mwelekeo wa usuluhisho wa mawazo hasi ya ndani.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu uwezo wao ni mdogo kushughurika na woga, wasiwasi na hamaki zinazohusiana na mifadhaiko. Wanapotafuta msaada wa kitaaluma, wanapewa aina fulani za madawa. Wakati mfadhaiko ulipotibiwa mara ya kwanza kwa kemikali, madawa hayo yalikuwa na athari hasi chache. Siku hizi madawa hayo yana nguvu nyingi na wakati mwingine ni ya hatari. Baadhi ya madawa haya hayapatani na wengi wanaoyatumia kudhibiti mihemko yao ya akili kwa wao wenyewe kama ilivyo kwa wengine. Baadhi ya madawa haya yanaweza kuondoa uwezo wa kutambuwa wengine na kufunga (fix) mawazo hasi kwa watu dhaifu. Watu hawa wanaweza kujitumbukiza kirahisi katika vitendo vya kujinyonga wenyewe na wenye kujitenga na jamii.

Kinachoelezwa hapa ni sababu za ukosefu wa ufanisi kwa ajili ya fiziolojia zinazohusiana na mifadhaiko na huzuni. Kinachopendekezwa hapa ni namna ya kuongeza ufanisi wa nguvu za ubongo kushughulika na mifadhaiko akili mikali na matokeo yake ya majonzi. Imejidhihirisha na kujionesha kwa wengine wengi matokeo chanya ya haya yanayopendekezwa hapa.

Patholojia ambazo zimeonekana kuwa na uhusiano na ''mfadhaiko jamii'' – woga, wasiwasi, mashaka, jaziba na matatizo ndani ya ndoa yanayodumu muda mrefu – na kujitokeza kwa mdororo wa fikra ni matokeo ya upungufu wa maji mwilini kufikia hatua ya mahitaji ya maji ya tishu za ubongo yameathiriwa. Ubongo hutumia nguvu za kiumeme zitokanazo na maji. Wakati wa upungufu wa maji mwilini uwezo wa ubongo kutengeneza nguvu hupungua. Ufanisi wa Kazi nyingi za ubongo zinazotegemea aina hii ya nguvu hupungua pia. Tunalitambua tatizo hili la upungufu wa ufanisi wa kazi katika ubongo na kulipa jina la mfadhaiko/stress. Hali hii ya mfadhaisho unaosababishwa na kupungua kwa maji mwilini (dehydration) inaweza kupelekea dalili za uchovu sugu mwilini (chronic fatigue syndrome). Hali hii ni lebo inayobandikwa katika mfululizo wa matatizo mengi ya kifiziolojia yahusianayo na mfadhaiko.

Ikiwa tutayatambuwa matukio yanayotokea wakati wa mfadhaiko, tutaweza pia kuzielewa dalili za uchovu sugu. Baada ya muda kadhaa wa kurekebisha upungufu wa maji mwilini na utata wa kiumetaboli uletwao nao (upungufu wa maji), dalili za uchovu sugu zitapotelea mbali bila kupenda.

Aya zifuatazo zinafafanua matukio ya kifiziolojia na wezekano za kimetaboli ambazo zinaweza kupelekea matumizi yaliyozidi ya baadhi ya hifadhi za mwili ambayo yanaweza kuwa ndiyo tatizo msingi katika uchovu sugu.

Mfumo fidio wa mwanzo mnyamavu uhusianao na upungufu wa maji mwilini;
Wakati mwili unapokuwa umepungukiwa maji (dehydrated), hali za kifiziolojia ambazo hujitokeza huwa sawa na zile hutokea wakati ubongo ukishughulika na mfadhaiko/stress. Upungufu wa maji mwilini ni sawa sawa na mfadhaiko, na mfadhaiko unapoimarika hutokea uhamasishwaji wa utolewaji wa malighafi za mwanzo toka katika hifadhi za mwili. Mlolongo huu hukausha baadhi ya hifadhi za maji ya mwili. Matokeo yake, upungufu wa maji mwilini husababisha mfadhaiko na mfadhaiko husababisha upungufu wa maji zaidi.

Katika mfadhaiko, baadhi ya matendo ya kihomoni huamshwa zaidi. Mwili hujiweka tayari kwa hali ya mtikisiko na kuanza kujihamasisha tayari kwa kupaa ama kupigana. Mwili unaonekana kutotambua hali za mabadiliko za kijamii za mwanadamu. Mwili unayachuja na kuyakadiria matukio yote ya kimfadhaiko katika hali ya kupigana nayo hata katika mifadhaiko midogo ihusianayo na kazi maofisini. Homoni maalumu kubwa hutolewa na kubaki katika hali ya ‘utayari' mpaka hapo mwili utakapotoka katika hali hiyo ya ufadhaikaji. Homoni hizo nyingi ni; endorphini, kortisone, prolaktini, vasopressini na renini-angiotensini.

Endorphini, Cortisone, Prolactini na Vasopressini:
Endorphinsi:
huuandaa mwili kuvumilia mateso na majeraha mpaka mwili utakapojinasua katika hali hizo. Pia hupandisha kiwango cha udhibiti wa maumivu. Kwa majeraha ambayo yangeweza kusababisha maumivu katika kiwango cha chini cha endorphini chini ya ‘mwamvuli' wa endorphini, mwili unaweza kuendelea na kazi zake kama kawaida. Kwa sababu za jukumu la kujifungua mtoto na kuhimili mzunguko wa hedhi wa kila mwezi, wanawake wamewezeshwa kuwa na homoni hii kwa wingi zaidi kuliko wanaume. Kwa sababu hiyo wanawake wana uwezo mkubwa katika kuvumilia maumivu kuliko wanaume.

Cortisone: huanzisha uhamasishaji wa pili wa nguvu na malighafi zilizohifadhiwa. Mafuta huvunjwa vunjwa katika asidi mafuta ili kubadilishwa kuwa nguvu. Baadhi ya protini huvunjwa tena chini katika asidi amino mhimu kwa ajili ya uundaji wa transimita nyurolojia za ziada, protini mpya na baadhi ya asidi amino maalumu kwa ajili ya kuchomwa na mishipa.

Wakati wa ujauzito na kunyonyesha, homoni hii na washirika wake huhamasisha utolewaji sare wa malighafi za mwanzo kwa ajili ya maendeleo ya mtoto. Ikiwa matendo ya cortisone yanaendelea kwa muda mrefu zaidi, hatimaye muda si mrefu baadaye kutatokea kupungua kwa hifadhi ya asidi amino za mwili.

Chini ya ushawishi wa cortisone, mwili huendelea kujitafuna wenyewe. Matendo ya cortisone yamesanifiwa kutoa malighafi za dharura kwa ajili ya uzarishaji wa protini mhimu za mwanzo na transimita nyurolojia kuuwezesha mwili kujinasua toka katika mifadhaiko yake. Cortisone haikusanifiwa kwa ajili ya umetaboli wa malighafi katika hali ya kuendelea juu ya ujenzi wa mwili. Hali hii ndiyo huzalisha madhara yahusianayo na mfadhaiko/stress ikiwa mfadhaishaji anaendelea kushikilia ushawishi wake ambao kimsingi huhitajika kwa nyakati fulani tu.

Prolactini: huakikisha utungaji wa maziwa kwa mama anayenyonyesha unaendelea kama ipasavyo. Huzianzisha seli za tezi kwenye matiti kuendelea na uzarishaji maziwa hata ikiwa kuna upungufu wa maji au mfadhaiko ambao unaweza kupelekea upungufu wa maji mwilini. Huzianzisha tezi za seli kujifufua na kujiongeza katika idadi.

Tunapaswa kukumbuka kuwa, ingawa tunafikiria zaidi juu ya ule mchanganyiko mzito wa maziwa, ni ujazo wake wa maji ambao ndio wenye umhimu wa kwanza kwa kijusi. Kila mara seli inapojigawa, asilimia 75 yake au zaidi ya ujazo wake inapaswa kujazwa na maji. Kwa kifupi, kukua hutegemea upatikanaji wa maji. Wakati maji yanaifikia seli, seli huweza kuvifikia viini lishe ambavyo hubebwa na kusambazwa na maji hayo. Prolactini pia hufanywa katika kondo la nyuma na kuhifadhiwa katika mifuko ya uzazi ya maji chumvi (amniotic fluid) kuzunguka kijusi. kwa kifupi, homoni hii ina matendo ya ‘ki-mamotrophic'. Huzifanya tezi za matiti na mikondo yake kukua. Homoni iliyokwishakua ina ufanano wa karibu na prolaktini hasa kimatendo isipokuwa tu prolaktini hulenga zaidi ogani za uzazi.

Imejionesha katika majaribio kwa panya kuwa kuongezeka kwa uzarishaji wa prolaktini husababisha vivimbe katika matiti. Mwaka 1987 katika mkutano wa kundi la watafiti wa kansa wa kimataifa kama mkufunzi mwalikwa dr.Batmanghelidj aliwasilisha hoja kuwa upungufu sugu wa maji mwilini ndicho kisababisho cha kwanza cha vivimbe mwilini. Uhusiano baina ya mfadhaiko, upungufu wa maji sababu ya miaka, utolewaji wa kudumu wa prolaktini na ubadilikaji wa tishu katika matiti havipaswi kutotiliwa maanani. Urekebishaji wa taratibu wa uchukuwaji wa maji wa kila siku hasa wakati ukikabiliwa na mifadhaiko ya maisha ya kila siku utasaidia kuzuia uwezekano wa kuzarisha kansa za matiti zinazohusiana na upungufu wa maji mwilini kwa wanawake na kansa ya kibofu cha mkojo kwa wanaume.

Vasopressini: hudhibiti kiasi maalumu cha mtiririko wa maji kwa baadhi ya seli za mwili. Pia husababisha kujikaza kwa kapilari inazozichochea. Kama jina lake linavyosomeka (vasopressin) husababisha kukazika kwa mishipa ya damu (vasoconstriction). Vasopressini hutengenezwa katika tezi ya pituitari na kutupwa katika mzunguko. Wakati inaweza kuikaza mishipa ya damu, baadhi ya seli mhimu humiliki nukta pokeaji (receptors) kwa homoni hii. Kutegemeana na matabaka yao, baadhi ya seli zinaonekana kumiliki kiasi kingi cha vasopressini kuliko zingine.

Ukuta wa seli ambao ni kava lililosanifiwa maalumu kuilinda seli, umesanifiwa kiasili katika matabaka mawili. Uma ya tuni (tuning-fork) kama matofali ya saruji yawekwayo pamoja na kunatana kwa msaada wa maji. Katikati ya matabaka haya mawili kuna njia muungano ambamo vimeng'enya husafiri, kwa namna moja vikiathiriana na kusababisha vitendo vipasavyo katika seli. Njia hii ya maji hufanya kazi inayofanana kama handaki la maji (moat) isipokuwa yenyewe ni ukanda uliojazwa maji (water filled beltway) na kila kitu kinapaswa kuelea ndani yake.

Wakati kunapokuwa na maji ya kutosha kuzijaza nafasi zote, handaki la maji (moat) hujazwa na maji huziingia seli. Kutakuja kutokea wakati ambapo wastani wa mtiririko wa maji ndani ya seli unaweza kuwa si wa kutosha na baadhi ya kazi za seli hutokea kuathiriwa. Ili kujikinga dhidi ya balaa liwezalo kutokea kutokana na hali hii, asili imesanifu namna bora kabisa kwa ajili ya uchujaji wa maji kupitia kuta za seli. Wakati vasopressini inapoufikia ukuta wa seli na kufyuzi kwa kipokezi chake kilichosanifiwa maalumu, kipokezi (receptor) hugeuka kama kichwa cha bomba la mvua na kufanya uchujikaji wa maji pekee kupitia vishimo vyake.

Kadiri mahitaji ya kutengenezwa seli mhimu yanavyojitokeza, ndivyo na vipokezi vya vasopressini vinavyojitokeza kwa wingi pia. Vasopressini ni mojawapo ya homoni zinazojihusisha na ugawaji na usambazaji wa maji kutegemea na umhimu wa mpango (priority plan) wakati kunapokuwa na upungufu wa maji mwilini. Seli za neva zinaonekana kutambulisha umhimu wake kwa kuzarisha vasopressini nyingi zaidi kuliko seli za tishu zingine. Seli za neva zinahitaji kutunza njia za maji katika neva zake katika hali ya ufanyaji kazi kamili. Ili kuwa na uhakika kuwa maji yanaweza kupita kupitia vishimo hivi (ambavyo huruhusu mpito wa molekuli moja tu ya maji kwa wakati mmoja), vasopressini pia ina sifa ya kusababisha kujikaza kwa mishipa ya damu na kuweka mminyo kutegemea na ujazo wa kimiminika katika eneo.

Kwahiyo, utokeaji mwingi wa sifa za transimita nyurolojia vasopressini huhitajiwa katika zoezi za uchujaji wa maji kwenda katika seli pale tu mtiririko huru na msambao wake wa moja kwa moja kupitia kuta za seli unapokuwa ni haba. Kwa maelezo zaidi soma maelezo katika kolesteroli.

Alkoholi: huzuia utolewaji wa vasopressini toka katika tezi ya pituitari. Ukosefu wa vasopressini katika mzunguko utatafsiriwa kama tokeo la upungufu wa maji kwa kiwango cha juu kabisa hata katika seli za ubongo. Sasa, ile namna rahisi ya kabla ya kushughurika na upungufu wa kawaida wa maji utatafsiriwa kama janga kuu la ukame kwa seli nyepesi kuhisi (sensitive) za ubongo. Ili kushughurika na aina hii ya upungufu wa maji, sasa homoni nyingine zaidi huamushwa ikihusishwa homoni raibu (addictive) ya mwili wenyewe – endorphini.

Kwahiyo, matumizi ya muda mrefu ya alkoholi/pombe yanaweza kuwa njia ya kushamirisha mwelekeo wa uraibu (addiction) wa kuzarishwa mara nyingi homoni endorphini katika mwili. Wanawake sababu ya jukumu la kuzaa na kutokewa na mzunguko wa hedhi kila mwezi, wanaonekana kupatwa na uraibu (addiction) wa pombe kirahisi zaidi kuliko wanaume. Inajionesha wanawake kuwa katika uraibu (addiction) kwa alkoholi ndani ya wastani wa miaka mitatu tangu wajiingize katika kunywa pombe wakati wanaume huwachukuwa wastani wa miaka saba hivi.

Dalili za uchovu sugu zinaweza kuanza kutokea baada ya unywaji wa kawaida wa vinywaji vyenye kafeina au alkoholi katika nafasi ya maji. Kipokezi cha vasopressini kimesanifiwa kiasili kutunza njia maji ya seli za mfumo wa neva katika hali ya kutosha. Kwa asili katika hali ya upungufu wa maji wa seli za mfumo wa neva, nguvu na akili za kufanya jambo jipya hupungua kwa kiasi kikubwa.

Katika upungufu mkubwa wa maji uliotengenezwa kutokana na mazoea mabaya ya unywaji pombe na kafeina, wakati maji yanapotakiwa kusukumwa kwa haraka na dharura katika njia maji ndani ya neva, mzunguko zaidi wa damu unahitajika pamoja katika mfumo wa neva. Mlolongo (process) huo utahusisha sasa utolewaji wa mkongwe histamini toka katika seli ambazo zimejipanga katika mfumo wa neva. Jambo hili hatimaye katika hatua fulani litasababisha kutokea kuwaka moto au uvimbe hali ambayo hatimaye itapelekea madhara katika seli zingine za karibu kwa hali ya haraka kuliko ziwezavyo kufanyiwa marekebisho (repairments). Matokeo ya nje ya mlolongo huu wa eneo moja yamepewa lebo ya matatizo mbalimbali katika neva (nerve disorders) yakihusisha maumivu mbalimbali ya mishipa (multiple sclerosis-ms). Sasa utibikaji wake unakuwa ni rahisi. Wengi wameshuhudia maji pekee yakifanya maajabu hayo kirahisi tena bila gharama yeyote!.

Mfumo wa renini-angiotensini (RA System):
Renini-angiotensini ni shughuli mfumo saidizi kwa mfumo wa histamini katika ubongo. Mfumo wa RA pia hutambulika kuwa na nguvu zaidi katika figo. Shughuli hizi huamushwa wakati ujazo wa maji unapopunguwa mwilini. Huamushwa ili kuyashikilia maji, na ili kulifanya hilo, mfumo huu huishikilia pia chumvi zaidi (sodium). Upungufu wowote baina ya sodiamu au maji wa mwili huufanya mfumo RA kuamshwa kirahisi zaidi. Mpaka hapo ujazo wa maji na sodiamu wa mwili utakapofikia usawa unaokubalika, mfumo RA pia huleta kujikaza kwa kapilari na mfumo wa mishipa. Mfumo umesanifiwa kufanya hivyo ili kusudi kujihakikishia kuwa hakuna nafasi inayobaki wazi katika mfumo wa mishipa sababu ya kushuka kwa ujazo wa maji. Ukazaji huu wa mishipa unaweza kufikia kiwango ambacho kinaweza kupimika na tunaiita hali hiyo kuwa ni shinikizo la juu la damu (hypertension). Unafikiri usomekaji wa BP 200 ni mkubwa sana?, dr.Batmanghelidj anasema ameshawahi kuona shinikizo la juu la damu la mtu aliyekamatwa akipelekwa kuuliwa katika moja ya magereza ya Iran wakati wa mapinduzi ya nchi hiyo likisoma 300!.

Sababu za kukazwa kwa mishipa hii wakati wa mfadhaiko ni rahisi kuzielewa. Mwili ni jumla ya mifumo mingi changamano iliyofungamana na yenye ustadi madhubuti. Kunapokuwa na mfadhaiko, baadhi ya maji yanayopatikana hutumika kwa ajili ya kuvunjavunja malighafi zilizohifadhiwa kama vile protini, wanga (glycogen) na mafuta. Ili kufidia kiasi cha maji kilichopotea na kuuweka mfumo katika mfumo wa kubana matumizi ya maji, mfumo wa RA utashirikiana kwa kazi hii na vasopressini na homoni nyinginezo. Figo ndio uwanja mahususi wa shughuli za mfumo wa RA.

Figo ndizo zenye majukumu ya uzarishaji wa mkojo na utolewaji wa haidrojeni iliyozidi, potasiamu, sodiamu na taka mwili zingine. Kazi zote hizi zinapaswa kufanywa kwa kuwiana na upatikanaji wa kiasi cha kutosha cha maji kitakachotumika kutengeneza mkojo. Ingawa, uwezo huu haupaswi kutumika kwa kiwango cha juu kila wakati la sivyo jambo hilo linaweza kupelekea madhara katika figo.

Mfumo RA ndio mfumo msingi katika kutafuta utulivu wa ujazo wa kimiminika mwilini. Ni mmojawapo ya mifumo shiriki ya shughuli za histamini katika kubajeti na kusambaza maji. Mfumo huu hudhibiti vipenyo vya mishipa ili viendane na ujazo wa kimiminika katika mfumo wa mzunguko wa damu. Shughuli za mfumo huu hupunguwa kadiri chumvi na maji yanavyopatikana kujaza uwezo wa vimiminika vya mfumo wa mishipa. Katika figo, mfumo huhisi mtiririko wa kimiminika na shinikizo la uchujaji kwa ajili ya mfumo wa kutengeneza mkojo. Ikiwa shinikizo la uchujaji ni dogo kuwezesha uzarishaji wa mkojo na utolewaji wake, mfumo wa RA utaikaza mishipa ya damu katika figo.

Kunapotokea madhara katika figo na kupelekea uzarishaji usioridhisha wa mkojo, mfumo RA huamshwa na kuwa hai zaidi. Huhamasisha uchukuwaji zaidi wa chumvi na kushawishi kiu zaidi. Kuharibiwa kwa figo kunaweza kuwa ni matokeo ya upungufu wa muda mrefu wa maji na chumvi mwilini ambao ndio sababu ya kuamshwa kwa shughuli za mfumo wa RA. Lakini siku za nyuma tulikuwa hatujatambua umhimu wa kujikaza kwa vipenyo vya mishipa (essential hypertension) kama ni ishara za kushuka kwa usawa wa kimiminika mwilini. Sasa, usawa usio sawa wa kimiminika (fluid imbalance) katika mwili unaweza kuwa ndiyo sababu ya kwanza ya kuharibiwa na magonjwa mengi yahusianayo na figo kufikia kiasi cha kuhitaji kubadilisha figo.

Wakati mfumo RA unapokuwa umewashwa kamili (fully turned ON), utaendelea kujiongeza na kujiongeza chaji mpaka mfumo mwingine asili uuzime kamili (turns full OFF). Kundi la swichi za kuuzima kamili mfumo RA linahusisha maji na chumvi – katika mtiririko huo – mpaka vipimo vya kujikaza kwa vipenyo vya mishipa vioneshe wastani wa kawaida.

Tezi za mate zinaonekana kuwa na uwezo wa kugunduwa kushuka kwa kiasi cha chumvi mwilini. Kunapokuwa na upungufu wa sodiamu, matezi haya yanaonekana kutengeneza kitu kijulikanacho kwa kitaalamu kama kinins. Kininsi huhamasisha mwongezeko wa mzunguko wa damu na uundwaji wa mate katika tezi za mate (salivary glands). Uongezekaji huu wa uzarishaji wa mate (kufikia kiasi cha kutoka nje kama udenda) husaidia mambo mawili: kwanza, huulainisha mdomo wakati unakula chakula katika mwili wenye upungufu wa maji, pili, hali yake ya utiririshaji tele wa alikalini husaidia uvunjajivunjaji wa chakula na hatimaye unyweshekaji wake katika tumbo. Katika mfumo mwili wa mwili (integrated sysytem), kininsi za tezi za mate zinaonekana zikiziamsha shughuli za mfumo RA ambao huanza kuziamsha sehemu zingine zote za mwili.

Kwahiyo, kupunguwa kwa sodiamu katika mwili (ambako pia huchangia kupunguwa kwa maji nje ya seli) kunaweza kuanzisha mfululizo wa matukio ambayo mwishowe huwa ndiyo msingi wa kutokea kwa shinikizo la juu la damu na uchovu sugu kwa binadamu. Uhusiano wa kininsi na kushuka kwa kiasi cha sodiamu (kulikosababishwa na kushuka kwa kiasi cha maji) na kuongezeka kwa kiasi cha mate hata wakati mwili hauna maji ya kutosha, ndilo fumbo (paradox) katika usanifu wa asili wa mwili wa binadamu. Ni kuleta janga kubwa kuendelea kushikilia dhana kuwa mdomo uliokauka ndio kiashiria kikuu cha mwili kuhitaji maji!, sababu ya kosa hili rahisi, taaluma ya madawa na utafiti wa kisayansi ni mambo yasiyo na mkazo kwa miaka mingi. Mengi ya marejeo na marudio kwa dhana zilizokwisha kubaliwa tayari vitakuwa ni vitu visivyoepukika. Ngoja tutumaini ‘Ulinzi binafsi' kutokuwa kikwazo katika njia.

Nini hutokea ikiwa tunakunywa chai, kahawa au cola katika nafasi ya maji?, visisimuwaji vya asili katika kahawa na chai ni idadi kubwa ya kaffeina na kiasi kidogo cha theafelini (theophylline). Hivi ni visisimuwaji (stimulants) vya mfumo mkuu wa fahamu mwilini huku wakati huo huo vikiwa ni mawakala wakausha maji mwilini kutokana na matendo yao katika ini ya kukojosha (diuretics). Kikombe kimoja cha kahawa huwa na wastani wa ml 85 za kaffeina. Kikombe kimoja cha chai huwa na wastani wastani wa ml 50 za kaffeina. Vinywaji vya cola huwa na wastani wa ml 50 za kaffeina ambazo sehemu yake nyingine hutumika kusanifisha vinywaji vya cola wakati inatolewa toka katika kokwa za cola akuminata.

Visisimuwaji hivi vya mfumo mkuu wa fahamu huzitoa nguvu za mwili toka katika ghala la ATP na kuzibadili ATP kwenda katika hatua yake ya kuunguzwa ya AMP katika seli. Huitoa pia nguvu kupitia utolewaji wa kalsiamu iliyo katika hali yake ya kuhifadhiwa katika seli. Kwahiyo, kaffeina inaonekana kufanya kazi ya kuchezea nguvu ya mwili. Sisi sote tunayajuwa matokeo haya ya mwisho ya kaffeina, tunachopaswa kujuwa sasa ni matokeo yake ya kuzidi wakati mwili unapokuwa haupo tayari kutoa nguvu kwa baadhi ya matendo. Katika hali hii, baadaye matendo ya baadhi ya homoni na transimita nyurolojia hayatakuwa na kikomo sababu uwezekano wa kushuka kwa kiasi cha chini cha nguvu iliyohifadhiwa. Kaffeina itaendelea kuleta matokeo hasi zaidi mpaka kiasi cha chini cha nguvu kimefikiwa. Vinywaji vya cola vina matokeo yaliyo karibu sawa na kaffeina.

Matokeo ya kaffeina yanaweza kwa wakati fulani kuchukuliwa kama yenye kufaa, lakini uchukuwaji wake wa kudumu kama mubadala kwa maji utanyang'anya uwezo wa mwili kutengeneza nguvu zitokanazo na maji (hydroelectric energy). Kaffeina iliyozidi itapelekea kushuka kwa nguvu katika ATP ya ubongo na mwili kitu kinachochangia katika ukosefu wa usikivu kwa vijana na watoto watumiaji wa vinywaji vyenye kaffeina au kwa dalili za uchovu sugu kama matokeo ya matumizi ya muda mrefu ya kaffeina katika miaka ya uzeeni. Utumiaji uliozidi wa kaffeina hatimaye utaimaliza mishipa ya moyo sababu ya usisimuwaji uliozidi.

Hivi karibuni katika baadhi ya majaribio imejionesha kuwa kaffeina huizuia mifumo vimeng'enya mhimu sana vijulikanavyo kwa kitaalamu kama phosphodiesterase (PDE) ambavyo huhusika katika prosesi za kujifunza na ukuzaji wa kumbukumbu. Katika ripoti za majaribio hayo, kaffeina hudhoofisha uwezo wa kuona na kumbukumbu kwa wanyama waliohusika katika majaribio hayo.

Ni lazima umeelewa sasa ni kwanini watu wenye matatizo ya kupoteza kumbukumbu (alzheimer's diseases) na watoto wenye uwezo mdogo katika kujifunza wasivyopaswa kunywa vinywaji vingine vyovyote isipokuwa maji. Kwa msisitizo ni kuwa hawapaswi kunywa kinywaji chochote chenye kaffeina.

Sasa inafaa kuunganisha taarifa zote hizi katika sura hii na vitu vingine viwili tofauti lakini vinavyoshabihiana, navyo ni shinikizo la juu la juu la damu na uundwaji wa kolesteroli ambavyo kwa pamoja vyote hupelekea matatizo katika moyo.

Mfumo wa uendeshaji wa kuuzoesha mwili kuendana na upunngufu wa maji mwilini (dehydration) ambao ndio hupelekea kujikaza kwa mishipa ya damu (vasoconstriction) ni sawa kabisa na ule wa wakati wa mfadhaiko (stress). Yaani, vitendo vya kuendelea vya vasopressini na vya mfumo RA ndivyo vinavyohusika kuupanga mwili kuishi katika mazingira ya kiukame. Mifumo hii huifunga mishipa kadhaa mingi ya kapilari na kuongeza shinikizo kwa mingine ili kupenyeza maji kupitia kuta zake katika seli za ogani zenye umhimu zaidi.

Usisahau, upungufu wa maji mwilini (dehydration), ndio mfadhaishaji namba wani wa mwili wa binadamu au kiumbe hai kingine chochote.

kwahiyo tunaweza kusema kuwa mfadhaiko/stress ni chanzo cha magonjwa mengi bila idadi.

Watu wengi wanaishi na mfadhaiko kwa sababu mfadhaishaji mkuu tumemjuwa kuwa ni upungufu wa maji mwilini (dehydration) sababu ya mazoea yetu ya kusubiri kiu ndipo tunywe maji.

Mtandao wa mfadhaiko wa marekani (American Institute of Stress) umeyataja katika tovuti yake baadhi ya magonjwa 50 yawezayo kusababishwa na mfadhaiko yakiwemo; kuumwa kichwa mara kwa mara, shinikizo la juu la damu, kisukari, homa za mara kwa mara, kufunga choo, kiungulia, maumivu ya tumbo, matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kuharisha, kupungua kinga ya mwili, hasira, kujitenga, kupungua au kuongezeka uzito bila kula, magonjwa ya akili, magonjwa ya ngozi, kupungua au kuongezeka njaa na magonjwa mengine mengi zaidi ya 50.

Mfadhaiko kiasi gani? Wowote tu wa kawaida hata ikiwa kondakta wa daladala ataendelea kukataa haujampa 1000 ili akurudishie chenji yako ya shilingi 700 baada ya kusahau akiendelea kuchukuwa nauli kwa wengine we ukidhani atakumbuka kukurejeshea, unaweza kuupelekea mwili kujingiza katika menejimenti ya mfadhako.

Kwa hiyo utagunduwa sasa ni mfadhaiko kiasi gani huupata mtu anapopima virusi vya ukimwi huku akikumbuka aliambiwa ukimwi hauna dawa!.

Nani haogopi kufa?

Kwa maelezo tuliyosoma hapa, mtu anapoambiwa tu ameambukizwa virusi vya ukimwi hata kama haumwi chochote maelezo ya sura hii yanathibitisha mtu huyo atakuwa tayari katika mfadhaiko ambao tumesema hupelekea mwili kuishiwa zaidi na maji.

Nini dawa ya mfadhaiko? Maji na chumvi.

Rejea:
=======

Ni muhimu kutambua kuwa; Ni sawa kutokuwa sawa (It's okay not to be okay) na Stress inaweza kumpata kila mtu

'Stress' inaweza kuathiri utendaji katika shughuli za kila siku. Ikiwa unapitia Hali hii, inashauriwa kupumzika, kuzungumza na watu wako na karibu, au kuonana na Wataalamu ili kusaidiwa

Ifahamike kuwa, dalili za Stress zinaweza kutofautiana kati ya Mtu na Mtu. Inawezekana unachopitia wewe si ambacho wengine wanapitia

Unapopitia 'Stress' kutokana na sababu mbalimbali, unakuwa na hali gani? Unafanya nini kurudi katika hali ya kawaida?

STRESS NA CHAKULA

Wakati Watu wengine hukosa kabisa hamu ya kula kwasababu ya #Stress, unajua kuwa wapo Watu ambao hukabiliana na hali hiyo kwa kula?

Ulaji unaoambatana na Msongo wa Mawazo (Stress Eating) unapotokea mara kwa mara, unafanya Mtu aone chakula kama njia mojawapo ya kukabiliana na hisia zake

Unapokuwa na 'Stress' ulaji wako unabadilika? Je, hutamani kabisa kula? Unakula kawaida, zaidi au unapendelea aina fulani ya chakula?

Elimu zaidi:

Everything to Know About Stress: Causes, Prevention, and More
 
Stress mbaya sana na mbaya zaidi ni kuwa unawezakuwa stressed bila wewe kujijuwa. Zaidi ya magonjwa 50 yanaletwa kama tokeo la mfadhaiko/stress mwilini!
 
Ameen Mungu azidi kukuweka udumu milele ili uendelee kutupatia maarifa haya adimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom