Unajua maana ya kushuka kwa bei za hisa?

Mkoba Mfuko

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
307
500
Kutokana na Covid19 makampuni mengi yametangazwa bei zake kushuka kwa kasi, hasa nchi zilizoendelea. Kushuka kwa hisa mambo kadhaa kwa wanunuzi wa hisa, lakini pia huashiria kitu kwa kampuni husika ambayo hisa zake zimeshuka

Hisa zikishuka bei huwa, watu hawana hela ya kununua hisa, hela huwa inaenda kufanya mambo mengine kwa wakati huo. Wanouza hisa hulazimika kushusha bei ili walau watu wavutiwe kununua hisa, na hapo hisa hushuka bei.

Lakini pia, hisa ni uwekezaji ambao mtu hutarajia faida kutoka kwenye kampuni ambayo ana hisa zake. Inapotokea matarajio ya kampuni kupata hasara au kufa, basi watu huacha kununua hisa na hivyo bei hushuka kwa kasi

Kwa kipindi hiki cha Covid19 makampuni mengi yanatarajiwa kupata hasara na ndio sababu ya hisa kushuka bei.
.
Kumbuka, inashauriwa kusoma taarifa za fedha ya kampuni kabla haujanunua hisa zake,
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,980
2,000
Na je, ni kwanini mtu anunue hisa zinazouzwa wakati ziko juu ?


Mleta mada amezungumzia kushuka kwa bei ya hisa na sababu zake,

Je msingi wa swali lako umeegemea kwenye muktadha wa maudhui hayo au ni nje ya kile alichoeleza mleta mada?

Je unataka kusema pamoja na kwamba inasemekana bei za hisa za makampuni kuanza kushuka lakini pengine kwa mtazamo wako bado unaona bei ziko juu?

Kwamba hata sasa bado bei bado ziko juu au siyo?

Kama na takuwa nimekuelewa vizuri.

Vinginevyo useme swali lako halijaegemea kwenye maudhui aloleta mleta mada.

Ambapo ikiwa hivyo nitaweza kukujibu pia kwa sababu za upande huo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkoba Mfuko

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
307
500
Na je, ni kwanini mtu anunue hisa zinazouzwa wakati ziko juu?
Mtu anaweza kununua hisa wakati ziko juu, kama anatarajia zinaweza panda zaidi. Ni sawa na biashara nyingine yoyote.
Kama hiza zinaonekana kupanda kila siku basi mtu huvutiwa kununua kwa bei yoyote ile, lakini pia hutegemea na ufanisi wa kampuni husika, kama mtu anaona kampuni husika haitarajiwi kupata hasara basi haoni tabu kununua kwa bei juu.

Kma kampuni haipati hasara, kuna uwezekano mkubwa hisa zikapanda tu so watu watanunua hivyo hivyo na zikaendelea kuwa juu

Angalia bei ya hisa za tbl na makampuni ya sigara
 

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,146
2,000
OEDIPUS,

Kinachofanya bei ya hisa fulani kushuka ni “Suppy and demand”. Hii ni kwa hisa ambazo zipo sokoni.
Kampuni inaweza kushusha bei kabla ya IPO.

Kuna sababu nyingine kama company issues additional stock(dilution)na kadhalika.
 

Mkoba Mfuko

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
307
500
OEDIPUS,

Kinachofanya bei ya hisa fulani kushuka ni “Suppy and demand”. Hii ni kwa hisa ambazo zipo sokoni.
Kampuni inaweza kushusha bei kabla ya IPO.

Kuna sababu nyingine kama company issues additional stock(dilution)na kadhalika.
Hii pia ni sababu, lakini kushuka kwa demand ya hisa, kunategemea sana na perfomance ya kampuni, na hata supply yake pia.

Mtu atavutiwa kuuza akiona kampuni imeanza kufanya vibaya ili isije kumchachia,

Ila zikiwa kwenye IPO, ni kampuni inataja bei kutokana na mhitaji yao, najua bei zinakuwa na fluctuations nyingi zikiwa kwenye secondary market huku kuliko kwenye Primary
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom