Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetilia mkazo sheria ya ardhi na upangaji miji ambayo inamtaka kila mkazi katika eneo lake anapotaka kufanya ukarabati wa nyumba yake, kupaka rangi ama kujenga uzio lazima awe na kibali kutoka halmashauri.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli amesema kibali hicho hakitolewi bure bali kinalipiwa, kwamba kuhusu kiasi inategemea na aina ya ukarabati unaofanya.
Amesema kuwa watu wamezoea kufanya kazi kwa mazoea bila usimamizi wa sheria, kwamba sheria hiyo kwa sasa inatekelezwa.
==========================
Kwa mujibu wa Vifungu 124 na 125 vya Kanuni za Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Udhibiti Uendelezaji), Sura 288 (GN 242 ya mwaka 2008), Ujenzi wowote ndani ya Mamlaka za Upangaji ambazo ni Mamlaka za Miji Midogo, Halmashauri za Miji, Manispaa na Ma-jijini lazima upate kibali cha Ujenzi kutoka kwenye Mamlaka husika.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 35 (i) cha Sheriaya Mipangomiji Na. 8 ya mwaka 2007,Mamlaka ya Upangaji inatakiwa kutoa kibali cha Ujenzi katika kipindi kisichozidi siku 60 kuanzia tarehe mwombaji alipowasilisha maombi yake. Aidha, ndani ya muda huo mamlaka inatakiwa kumjulisha mwombaji kuwa amekubaliwa au amekataliwa ombi lake na kutaja sababu zilizopelekea ombi lake kukataliwa.