Unajua Kura Yako Ilikoishia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unajua Kura Yako Ilikoishia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Acha Uvivu, Sep 27, 2012.

 1. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni chaguzi nyingi zimepita tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini. Kuna watu wengi humu JF ambao licha ya kushiriki kupiga kura katika mfumo wa vyama vingi pia wana historia ya kupiga kura katika mfumo wa chama kimoja. Enzi hizo mpigaji kura aliweza kupigia mtu (Mgombea) au kivuli. Na katika mazingira ya chama kimoja mpiga kura aliweza kujua kuwa kura yake imeenda kwa kivuli (imepotea) kabla hata matokeo hayajatoka au kujua kabisa kuwa kura yake imeenda kwa mgombea halali (mtu halali) ambaye lazima ataibuka mshindi.

  Lakini katika zama hizi za vyama vingi tangu kuanza ni vigumu mtu ambaye amepigia chama tofauti na CCM kujua kuwa kura yake imehesabiwa kwa aliyempigia kura. Asilimia kubwa ni kwamba hiyo kura huwa imeibiwa, na mwizi akiwa CCM.

  Katika uchaguzi wa 2010 kama ulipiga kura unaweza kurudisha mawazo nyuma, je kura yako ilihesabiwa kihalali au iliibiwa. Kuhesabiwa kihalali au kuibiwa kwa hiyo kura kunategemea mahali ulipopigia kura, wakala aliyesimamia zoezi la upigaji kura, msimamizi mkuu katika kituo cha kupigia kura, mkurugenzi wa NEC wa jimbo la uchaguzi na uongozi wa NEC Taifa, kwa upande mmoja na uchungu wa wapiga kura kusimamia matokeo na msimamo wa mgombea katika eneo husika, kwa upande mwingine.

  Mfano, katika jimbo la Segerea ni moja ya maeneo ambayo wengi wa waliyopigia upinzani wanaamini ziliibiwa kura. Lakini watu wa Karatu, Arusha Mjini, Mbeya Mjini, Lindi Mjini n.k wengi wana uhakika kuwa kura zao zilihesabika kulingana na malengo yao.
  Ni wakati sasa turudishe nyuma fikra, je kura zetu zilihesabiwa kihalali. Kama sio ni mazingira gani yalifanya hivyo? Na je unadhani nani wa kumlaumu? Na marekebisho gani kifikra na kimipango yafanyike ili kura yako au ya jirani yako isiibiwe katika uchaguzi ujao?

  Karibu wana bodi tuongee kimipango zaidi ili kuimarisha mfumo wa upigaji kura na kusimamia hasa miungoni mwetu wenyewe halafu tume ya uchaguzi na zisichakachuliwe katika chaguzi zijazo.
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mie watu km nyie ndio nawapenda na Mara nyingi huwa nawauliza maswali ila mnaishia mitini, swali langu ni hili kura huwa zinaibwajwe? Toa jibu la ufasaha na usi pepese macho
   
 3. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unapouliza swali kama hilo, maana yake wewe huamini kuwa kura zinaibiwa. Au we umewahi shiriki katika uizi sasa unataka kuambiwa jinsi mnavyoiba ili mtafute mbinu zingine.

  Kwanza mnakimbia na maboksi yaliyojaa kura.
  Pili, mnaongeza au kubadilisha kura mnazokuwa mmezijaza na zile halali mlizopigiwa hapana. Hata mara nyingine kufuta kabisa kura yoyote iliyoenda kwa upinzani.

  Mfano, Lipumba aliwahi sema katika kituo alichoenda kupiga kura yeye na mke wake, matokeo yalivyotoka akapata sifuri. Sasa zile mbili za hao wawili zilienda wapi? Je maboksi yalizimeza zisionekane?
   
Loading...