unajua kunywa pombe kiasi ni kunywa namna gani?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,885
hebu chekicheki unaweza kuona sifa zinazolingana na pombe uipendayo.
NO. UJAZO (mililita) NGUVU (asilimia) KIASI CHA POMBE(mililita) WANAWAKE WANAUME
1. 350mls 4% 14.0mls Bia mbili kwa siku. usizidishe bia kumi kwa wiki. bia tatu kwa siku. usizidishe bia 15 kwa wiki.
2. 500mls 4.5% 22.5mls Bia moja na nusu kwa siku. usizidishe bia 15 kwa wiki. Bia mbili kwa siku. usizidishe bia kumi kwa wiki.
3. 500mls 5% 25.0mls Bia moja na nusu kwa siku. usizidishe bia 6 kwa wiki. bia mbili kwa siku. usizidishe bia tisa kwa siku.
4. 500mls 5.5% 27.5mls Bia moja kwa siku. usizidishe bia tano kwa wiki Bia moja na nusu kwa siku. usizidishe bia nane kwa siku.
5. 500mls 6% 30.0mls Bia moja kwa siku. usizidishe bia tano kwa wiki. Bia moja na nusu kwa siku. usizidishe bia nane kwa wiki.
6. 500mls 6.5% 32.5mls Bia moja kwa siku. usizidishe bia nne kwa wiki. Bia moja na nusu kwa siku. usizidishe bia saba kwa wiki.
7. 500mls 7% 35.0mls Bia moja kwa siku. usizidishe bia nne kwa wiki. Bia m oja na nusu kwa siku. usizidishe bia sita kwa wiki.
7. 500mls 7.5% 37.5mls Bia moja kwa siku. usizidishe bia nne kwa wiki. Bia moja kwa siku. usizidishe bia sita kwa wiki.
8. 750mls 8% 60mls nusu chupa kwa siku. usizidishe chupa mbili na nusu kwa wiki. Robo tatu ya chupa kwa siku. usizidishe chupa tano kwa wiki.
9. 750mls 9% 67.5mls Nusu chupa kwa siku. usizidishe chupa mbili kwa wiki. Robo tatu ya chupa kwa siku. usuzidishe chupa tatu kwa wiki.
10. 750mls 10% 75.0mls Nusu chupa kwa siku. usizidishe chupa mbili kwa wiki. Nusu chupa kwa siku. usizidishe chupa tatu kwa wiki.
11. 750mls 11% 82.5mls Nusu chupa kwa siku. usizidishe chupa mbili kwa wiki Nusu chupa kwa siku. usizidishe chupa tatu kwa wiki.
12. 750mls 12% 90.0mls Chupa moja gawa mara tatu na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe chupa moja na nusu kwa wiki. Nusu chupa kwa siku. Usizidishe chupa mbili na nusu kwa wiki.
13. 1000mls(1lita) 12% 120mls Gawa kwa nne na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe chupa(box) moja kwa wiki. Gawa kwa tatu na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe chupa (box) mbili kwa siku.
14. 750mls 18% 135mls Gawa kwa nne na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe chupa moja kwa wiki. Gawa kwa tatu na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe chupa moja na nusu kwa wiki.
15. 100mls 35% 35mls Kinywaji kimoja kwa siku. usizidishe vinywaji vinne kwa wiki. Kinywaji kimoja kwa siku. usizidishe vinywaji sita kwa wiki
16. 200mls 35% 70mls Nusu kinywaji kwa siku. usizidishe vinywaji viwili kwa wiki. Nusu kinywaji kwa siku. usizidishe vinywaji vitatu kwa wiki.
17. 500mls 35% 175mls Gawa kwa tano na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe kinywaji kimoja kwa wiki. Gawa kwa tano na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe kimoja na nusu kwa wiki.
18. 750 40% 300mls Gawa kwa kumi na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe nusu chupa kwa wiki. Gawa kwa saba na kunywa kimoja kwa siku. usizidishe robo tatu ya chupa kwa wiki.
 
wanaume wanashauriwa wasizidishe 40mls kwa siku na 215mls kwa wiki. wanawake wanatakiwa wasizidishe 30mls kwa siku na 142mls kwa wiki.
 
hebu tuambie ukizidisha zaidi ya hapo kuna madhara gani? nyumbulisha tafadhali!
 
hebu tuambie ukizidisha zaidi ya hapo kuna madhara gani? nyumbulisha tafadhali!
unakuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya ini (liver cirrhosis), gout, na ugonjwa wa kusahau sahau. pia kuna hatari ya kuwa mtumwa wa pombe.
 
hayo mavipimo yenu hayanisaidii lolote,mie nakamata hadi napochokea ndo naenda kulala
kuna watu wanamagonjwa na wanashauriwa wasinywe sana sasa wanakuwa wanajiuliza kutokunywa sana kunakuwaje?
 
Mkuu,
Hongera kwa kututisha. Ila umesahau kunukuu source ya data zako. Usikute umejipikilisha?
 
jamani tufanye hivi.....we ukiniona nimezizi niache.....ukiona nimedevera nipotezee.....
 
Mkuu,
Hongera kwa kututisha. Ila umesahau kunukuu source ya data zako. Usikute umejipikilisha?
mkuu tukiandika sources itabidi tufungue uzi wake. mfano hiyo namba kumi na nne source ni chupa ya dompo!
 
hiyo bia 15 kwa wiki manake unajumlisha na jmosi na jpili ama? maana si unajua mahesabu ya jmosi yako tofauti..ikishafika wkend jmosi na jpili kwa ujumla zinaweza fika 20
 
tunahitaji kiwanda kimoja tu cha kutengeneza pombe kwa mwaka kwa dunia nzima.
 
mkuu naomba hesabu za castle milk, mimi huwa naiita 'kahawa' nikipata zangu mbili na bi mkubwa zake reds mambo yanakuwa safi sana
nafikiri namba 5 hapo juu ni castle milk. kama unapiga mbili sio mbaya sana
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom